Haya mahojiano yalifanywa siku za nyuma Kutoka kwenye JARIDA LA NUMBER10....
Yanga inaenda kucheza kombe la Shirikisho, ukiwa umesajiliwa kwa kuisaidia klabu hiyo, Yanga watarajie kitu gani kutoka kwako?
Nitatumia jitihada zangu na wachezai wenzangu kuhakikisha tunafanya vizuri katika mashindano hayo, naamini mimi mwenyewe sitaweza kucheza peke yengu, tukicheza kama timu tutashinda michezo hiyo.
Coach Kastodian Papic ndiye aliyekuleta Yanga, unafikiri unaweza kuisaidia klabu hiyo?
Naamini mwalimu Papic aligundua umuhimu wangu na kunihitaji katika timu yake, namthamini mwalimu huyo ameamini uwepo wangu utaisaidia Yanga katika mechi zake za ligi na hata za kimataifa.
Ulikutana wapi na Papic?
Alikuwa kocha wangu wakati nacheza Orlando Pirates 2005/06 kabla sijapelekwa kwa mkopo FC AK.
Umeletwa na Papic, siku akiondoka nawe utaondoka?
Hapana amenileta huku lakini nimeingia mkataba na timu ya Yanga, sitaondoka hadi mkataba wangu uishe, kama kocha akiondoka basi nitabaki na makocha wengine watakaokuja.
Yanga wana upinzani wa jadi na Simba, mzunguko wa kwanza waliifunga 1-0, utaendeleza makali hayo?
Tutashinda mechi zote za ligi kuu tukiwa kama timu, hatutaangalia aina ya timu ya kuifunga, tutafunga timu zote tutakazokutanana nazo.
Yanga msimu uliopita walipoteza ubingwa kwa Simba, sasa wako nyuma kwa pointi 2, (Simba 27 Yanga 25), moja ya lengo la ujio wako ni kurudisha ubingwa, unalifahamu hilo.
Jibu: Nalijua nimeambiwa, na dhumuni hasa tunataka kucheza klabu bingwa msimu ujao, nitatumia uwezo na uzoefu nilionao kufanikisha ushindi kwa timu yangu.
Usingekuwa wanasoka ungekuwa nani?
Kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kimataifa kati ya Zambia na nchi zingine.
VPL ina idadi chache ya mechi za ligi 22, Zambia wana mechi 30 huoni kama umekuja kupoteza kiwango chako?
Sijapoteza kiwango changu, kweli Zambia tuna mechi 30, Tanzania 22, sitapoteza kiwango changu bali nitapata nafasi ya kubaki katika mechi za kimataifa kwani Yanga inashiriki mashindano ya kimataifa ya Afrika (Shirikisho).
Umecheza timu nyingi sana barani Afrika, umekuja Yanga, je ni sehemu ya kupita au kumalizia?
Yanga nimekuja kucheza mpira, kwa mkataba maalumu, endapo mkataba wangu ukiisha nitaondoka, na kutafuta maisha sehemu nyingine, mpira ni maisha yangu hivyo nitacheza hadi hapo itakapofikia mwisho wangu.
Familia yako utahama nayo Tanzania?
Kuhama bado sijafikia wazo hilo lakini wanaweza kuja kunisalimia mara kwa mara na kama itatokea wanaweza wakahamia.
Kweli mkeo ni mwanasiasa?
Ni mwanasiasa wa Republican nchini Zambia.
Jina kamili: Davies Mwape
Kuzaliwa Dec 05, 1986
Urai. Mzambia
Klabu: Police Tiger 2001-2003, Nkwizer FC 2003, Chambishi FC 2004/05 (Zambia), 2005/2006 Orlando Pirates, 2006, FC AK (mkopo), 2007/09 Jomo Cosmos (SA), 2009/2010 Zanaco FC, 2010 Power Dynamos na Konkoro Blades FC.
Klabu ya sasa: Dar Young Africans-Yanga SC
Familia: Mke na Mtoto (Richard)
Duh hizi hulka za wachezaji kujipunguzia umri huwa zinanishangaza sana!! sasa jizee lote hili eti lina miaka 25 yaani ukimuangalia huyu jamaa ana miaka si chini 35. haya bana bila hivyo hupati ulaji. haya ndo ya kina Esien anadai ana miaka 25 anapiwa tiba ya mtoto kumbe yeye ni mzee na anashindwa kupona.!!!!
ReplyDeleteChapaulaya-Sweden