Waziri wa Michezo, Mh. Kadutu pamoja na Naibu waziri wa Michezo George Nkini wakiwa na wawakilishi wa timu zitakazoshiriki michuano ya PRO-LIFE leo, Wakwanza kulia ni Kocha mkuu wa timu ya chuo.
Uongozi wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUTSO), leo kupitia kwa Wizara yake ya Michezo na Burudani imepanga makundi ya mashindano ya PRO-LIFE itakayoanza kutimua vumbi mnamo tarehe 05/11/2011 ambapo fainali zake zitakuwa ni tarehe 11/12/2011. Michuano hiyo inashirikisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa kikapu, Volleyball na Netball.
Upangaji huo wa makundi ulishirikisha viongozi wa wizara pamoja na viongozi na baadhi ya wachezaji wa timu husika ambapo jumla ya timu 12 zitashiriki katika michuano hiyo kwa upande wa mpira wa miguu. Kwa mara ya kwanza mwaka huu michuano hiyo itashuhudia timu ya Chuo kikuu cha Afya Bugando kikishiriki, huku timu ya BSCP nayo ikipata nafasi yakushiriki kama timu inayojitegemea tofauti na awali ambapo walikuwa wakishirikiana na BBA.
PRO-LIFE ni michuano inayofanyika kila mwanzoni mwa mwaka mpya wa masomo katika chuo cha Mtakatifu Agustino ambapo timu zinazoshiriki hundwa na wachezaji wote wa mwaka wa kwanza mpaka wa tatu/nne. Na muasisi wa mashindano haya ni Padri Aidan Msafiri ambapo nia kubwa ni kuwafanya wanafunzi kutoutumia muda wao wa mwisho wa wiki vibaya pamoja na kujenga umoja na afya za washiriki.
Timu 12 zitakazoshiriki ni Bachelor of Science in Procurement and Supply Chain Management (BSCP), Bachelor of Laws (LLB), Advanced Diploma in Accountancy (ADA), Bachelor of Education, Bachelor of Tourism, Engineering and Agriculture (Combine), Bachelor of Business Administration, Bugando, Bachelor of Arts in Public Relations and Marketing (BAPRM), Bachelor of Arts in Economics (BAEC), Bachelor of Arts in Mass Communication (BAMC), Certificate of Journalism and Accountancy (Combine) and Bachelor of Sociology (BASO).
Aidha Kocha mkuu wa timu ya Chuo hicho amesema kuwa atatumia michuano hiyo kuangalia wachezaji wa timu ya chuo ambao watatengeneza kikosi kamili cha chuo hicho, ambapo vigezo vitakavyozingatiwa kwa mchezaji ni nidhamu na kujituma uwanjani.
No comments:
Post a Comment