Kikiwa bado na ndoto za kupata uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kimeomba kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa nyota wa ndani (CHAN).
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, msemaji wa ZFA, Munir Zakaria, alisema mbali ya kuomba ushiriki huo CAF, pia wametuma maombi ya ushiriki wa michuano ya Nile Basin inayoandaliwa na Chama cha Soka cha Misri.
Zakaria alisema licha ya fainali za Mataifa ya Afrika (CAN), Tanzania kuwa ni moja, lakini wameamua kuomba CHAN kwa kuwa ni michuano ya ndani.
“Tumemtuma Tenga (Rais wa TFF), kuwasilisha maombi yetu CAF na tunasubiri atupe majibu,” alisema msemaji huyo.
Michuano ya CHAN uhuhusisha nyota wanaocheza ligi za ndani tu ambapo Tanzania ‘Taifa Stars’ ilifanikiwa kufuzu fainali za kwanza zilizofanyika nchini Ivory Coast.
Kuhusiana na Nile Basin, Zakaria alisema wamevutiwa na unono wa zawadi katika michuano hiyo hivyo kuamua kuomba kushiriki baada ya kuchelewa kufanya hivyo mwaka jana.
No comments:
Post a Comment