Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo, yupo tayari kurejea Tanzania, kuifundisha timu hiyo iwapo atatakiwa na uongozi wa juu wa nchi.
“Mimi sina tatizo na kama Rais Kikwete (Jakaya) au Pinda (Waziri Mkuu Mizengo), watasema nirudi, nitafanya hivyo bila matatizo kwani ninaipenda Tanzania na nilishiriki kikamilifu kuiunda timu ya Taifa,” alisema Maximo Jumamosi.
Akizungumza wakati wa mkutano wake na ujumbe wa Waziri Mkuu unaofanya ziara nchini hapa, Maximo alisema ingawa anafanya mazungumzo na timu ya hapa ambayo hakutaka kuitaja, lakini mapenzi yake makubwa yako kwa Taifa Stars.
“Najua Tenga (Leodegar-Rais wa TFF), hana uwezo wa kuniita kwa sasa kwa sababu ana mkataba na kocha mwingine (Jan Poulsen), lakini kama Kikwete au Pinda watasema, bila shaka nitatekeleza,” alisema Maximo huku akijawa na furaha kubwa kukutana na Watanzania jijini hapa.
Hata hivyo, alikosoa utaratibu wa sasa wa kutoinua vijana na badala yake kuita katika timu ya Taifa wachezaji wakongwe kwa sababu tu wanaishi Ughaibuni.
“Angalia hivi sasa mnaacha wachezaji vijana ambao wanahitaji kunyanyuliwa na badala yake mnaingiza wachezaji wenye umri mkubwa (anatoa mfano) ambao wana miaka miwili tu ya kucheza soka,” alisema kocha huyo.
Alishangaa kusikia kuwa hivi sasa Mrisho Ngassa anakalishwa benchi katika timu ya Taifa na kuingia baadaye, wakati ni mchezaji mahiri na kusema kuwa kufanya hivyo ni kuua kiwango chake.
“Tunapaswa kuangalia uwezo wa vijana wadogo na kuwainua, angalia mimi ndiye niliyemuibua Mbwana Samatta na kumuingiza Taifa Stars… angalia sasa, anacheza soka la kulipwa nje ya nchi, hayo ni matunda ya kuibua vijana,” alitamba.
Alisema si vibaya kubadilisha wachezaji, lakini ni mbaya kukiuka filosofia ya soka, ambayo inataka soka kuanzia kwa vijana wadogo na kuwakuza kivipaji.
Search This Blog
Tuesday, October 11, 2011
MAXIMO APONDA FALSAFA ZA POULSEN, BADO ANAIPENDA TZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kuhusu mrisho ngaza hilo kweli,kwani kwa sasa Tanzania mrisho ngasa amejitahidi kuonesha kipaji chake.lkn mwisho wa siku tunabaki kusema kocha ndo mwenye maamuzi ya mwisho.
ReplyDelete