Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), limesema haliwezi kumfukuza kazi Kocha Mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Jan Poulsen baada ya kikosi hicho kutolewa kwenye michuano ya kufuzu fainali za Afrika mwakani, kwani ni gharama kubwa kufanya hivyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema wameyakubali matokeo ya kutolewa kwa Stars na kikubwa sasa wanasubiri ripoti ya kocha huyo.
“TFF tunasema wazi kwamba tumekubali matokeo yote ya uwanjani na kikubwa sasa tunasubiri ripoti ya benchi la ufundi likiongozwa na kocha kwa ajili ya kuangalia nini cha kuifanyia timu yetu,” alisema.
Angetile alisema wataipitia ripoti ya kocha huyo na kuangalia kipi ambacho amekieleza na wao kama TFF kwa kupitia Kamati ya Ufundi watakaa na kujadiliana na nini kifanyike.
“TFF haiwezi kusema inamfukuza kocha kwa sababu tumeshindwa kufuzu, tunachosubiria ni ripoti yake baada ya michuano hiyo.
“Tutaangalia nini tulichokubaliana naye kwenye mkataba na kipi kimefanyika na nini ambacho hakijafanyika na kwa sababu zipi.
“Ripoti hiyo ndiyo itakayotoa mwanga na ni jambo la kawaida kwa mwalimu kutoa ripoti yake kila baada ya michuano.
Katika ripoti hiyo, kocha ataainisha kile alichokiona na mipango yake, kwani pengine sisi TFF ndiyo tulioshindwa kutimiza baadhi ya vipengele na kusababisha timu kufanya vibaya.
“Hivyo baada ya ripoti yake tutajua nini cha kufanya, lakini kwa sasa hatuwezi kusema tutamfukuza kocha, kwani kukatisha mkataba ni gharama kubwa,” alisema Angetile.
Wadau mbalimbali nchini wamekuwa wakihoji uwezo wa kocha huyo, huku wakitoa maoni kwamba TFF ikatishe mkataba wake.
Search This Blog
Tuesday, October 11, 2011
T.F.F YAOGOPA KUMTIMUA KAZI POULSEN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
kama ni wao Tff kama anavyosema ndo wanaweza wakawa wamesababisha timu isifuzu jibu liko wazi waachie wao ngazi kwa kutotimiza wajibu huu ni ubabaishaji.
ReplyDeleteKama ni wao TFF wamefanya uzembe kama anavyosema timu isifuzu jibu liko wazi waachie ngazi kazi imewashinda.
ReplyDelete