Vita kubwa inanukia baina ya wachezaji hao wanne wa safu ya kiungo ya Simba ambao kila mmoja ni bandika bandua na Kocha Moses Basena atakuwa katika mtihani mkubwa wa kuchagua wachezaji wawili wa kutawala katikati.
Simba ambayo inaongoza ligi kwa pointi 18, ilikuwa ikiwatumia wachezaji wawili wa kigeni mara nyingi katika safu ya ulinzi ambao ni Mkenya Jerry Santo na Patrick Mafisango wa Rwanda lakini sasa kazi imekuwa tete.
Shomari Kapombe ambaye amecheza mechi ya mwisho dhidi Mtibwa na kufanya mambo makubwa kwenye kiungo alipochukua nafasi ya Mafisango ambaye hakuchezeshwa kabisa kwenye mchezo huo amemchizisha kabisa Basena.
Lakini kama hiyo haitoshi kiungo mahiri wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto naye ameanza mazoezi na ameonekana kuwa fiti na kumvutia zaidi Basena ambae habari za ndani kutoka kwenye benchi la ufundi zinadai anafikiria kuwachezesha Mwinyi na Kapombe kwenye kiungo kutokana na kuvutiwa na tabia, kujituma na uwezo wao.
Hiyo inamaanisha kwamba Mafisango na Santo watakuwa kwenye wakati mgumu utakaozidisha ushindani kwenye safu ya kiungo ya Wekundu wa Msimbazi ambao wachezaji kama Haruna Moshi, Ulimboka Mwakingwe, Amri Kiemba na Shija Mkina nao wanaweza kuicheza lakini huchezeshwa safu zingine hasa za winga.
Basena alisema kuwa kurejea kwa Kazimoto ni changamoto kubwa kwa Simba lakini akakiri kwamba hakuna mchezaji wa kiungo aliyeko fiti na anamkosha kwa sasa kama Kapombe.
Kauli ambayo inamaanisha Mafisango ambaye hivi karibuni alisimamishwa kwa madai ya utovu wa nidhamu atakuwa kwenye wakati mgumu na huenda akapewa nafasi ya kudumu kwa muda kwenye benchi.
Search This Blog
Saturday, October 1, 2011
VITA YA NAMBA KWENYE KIUNGO CHA SIMBA NI BALAA-KAZIMOTO AANZA MAZOEZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ebwana kaka shaffih tunashukuru kwa kuendelea kutupa uchambuzi wa ukweli ila tunaomba na ligi ya spain uipe kipaumbele kama uingeleza
ReplyDelete