Wakati mechi za Simba, Yanga na Azam FC ikiwa imesimama kupisha michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki mataifa ya Africa mwakani nchini Gabon na Equatorial Guniea. Si vibaya kupata takwimu mbalimbali za ligi hiyo msimu huo.
MSIMAMO WA LIGI.
Simba SC ndio inaongoza ligi wakiwa na point 18 wakifuatiwa na Azam FC wenye point 15, wakati Yanga ikiwa nafasi ya 6 wakiwa na pointi 12. Coastal union ndio wa Mwisho wakiwa na point 4 wakifuatiwa na Villa squad wenye point 5 baada ya kucheza michezo 8.
MSIMAMO WA WAFUNGAJI.
Mshambuliaji wa Moro United Gaudence Mwaikimba pamoja na wa Azam FC John Bocco wanaongoza kwa kufumania nyavu wakiwa wameziona mara 5. Wakifuatiwa na kiungo toka Rwanda anaecheza Simba Patrick Mafisango mwenye magoli 4.
Mfungaji bora wa msimu uliopita Mrisho Khalfani Ngassa Bado hajaziona nyavu baada ya kupata nafasi ya kuteremka uwanjani mara 6 akicheza kwa dakika zaidi ya 500.
MORADI NA AGREY NI ZAIDI YA COSTA NA NYOSO.
Safu ya ulinzi wa Azam FC ndio ya safu imara zaidi baada ya kuruhusu magoli 2 katika michezo nane. Safu hiyo iko chini ya nahodha Agrey Morris na Said Moradi wakati ile ya Simba inayoongozwa na Nyosso na Victor Costa ikiruhusu magoli 4.
Kipa Mwadini Ally wa Azam FC ndie kipa pekee ambayo ajafungwa baada ya kuonekana uwanja katika michezo mitano katika ya 8 timu yake iliyo cheza.
Wakati Moro Utd na Villa Squad zinaongoza kwa kufungwa mabao mengi, Moro imeruhusu mabao 15, wakati Villa imefungwa 13 katika michezo minane iliyocheza kwenye ligi hiyo.
JKT RUVU NA SIMBA HAWAFUNGWA.
Timu ya Simba na JKT Ruvu hawajapoteza mchezo wowote kati ya 8 waliyocheza. Simba SC imeshinda michezo mitano na kutoka sare mitatu, wakati JKT Ruvu wameshinda miwili na kutoa sare michezo 6 kati ya nane waliyocheza.
Azam FC na Jkt Oljoro wamepoteza mchezo mmoja wakati Coastal union wakiwa kinara kwa kupoteza mchezo, baada ya kupoteza michezo 6.
KADI ZILIZOTOKA.
Ikiwa michezo 55 imeshachezwa mpaka sasa jumla ya kadi 223 zimetoka, huku kadi nyekundu zikiwa 15 na njano 208. Simba, Villa Squad, Kagera Sugar na Toto African zimeibuka vinara kwa kadi nyekundu na njano.
Villa imeibuka kinara wa kadi za njano baada ya kumiliki kadi hizo 20, Simba 19 na Toto African 18 huku ikiwa kadi 208 zimeshatolewa na waamuzi wa ligi hiyo kwa michezo 55 iliyochezwa sawa na uwiano wa kadi tatu kila mechi.
Kagera Sugar imeibuka kinara wa kadi nyekundu baada ya kumiliki kadi hizo tatu kati 15 zilizotolewa na waamuzi kwa michezo yake minane iliyocheza.
YANGA NA SAFU KALI YA USHAMBULIAJI.
Yanga ina safu kali ya ushambuliaji baada ya kutikisa nyavu za wapinzani mara 13 ikifuatwa na Moro United iliyotikisa nyavu mara 12 katika michezo 8 waliyocheza. Huku jumla ya magoli 108 yakiwa yamefungwa ndani ya michezo 55 ya Ligi Kuu.
Costal union ina safu butu baada ya kufunga magoli manne 4 katika michezo 8 waliyocheza ikifuatiwa na Villa squad waliotikisa nyavu mara 5.
Azam FC msimu huu safu yake ya ushambuliaji iliyosajiliwa kwa mamillion imeshindwa kutamba baada ya kuingia kwenye nyavu mara 6.
Search This Blog
Friday, September 30, 2011
VODACOM PREMIER LEAGUE STATISTICS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment