Katika hali ya kushangaza kocha wa Fulham mdachi Martin Jol amempiga faini mchezaji wake Pajtim Kassami kwa kosa la kushindwa kufunga penati kwenye mchezo wa kombe la Carling kati ya timu yake ya Fulham na Chelsea.
Kiungo huyo ambaye ni raia wa Uswis amepigwa faini hiyo ambayo ni kiasi cha paundi mia tano toka kwenye ambazo zitakatwa toka kwenye mshahara wake kwa makosa mawili ambayo ni kupiga penati ambayo hakupangiwa kupiga na kosa la pili ni kukosa penati hiyo ambayo awali ilikuwa ipigwe na mchezaji mwingine Orlando Sa. Kitendo hiki kinadaiwa kuwachukiza wachezaji wa Fulham ambao wanaonekana kutofurahia maisha chini ya mdachi huyo.
Taarifa zaidi zinadai kuwa Martin Jol ameifanya Fulham kuwa kama kambi ya jeshi na amekuwa akiweka faini kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu ikiwemo kuchelewa mazoezi na kutoroka kambini . Hivi karibuni kocha huyo anadaiwa kukosana na mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo Bobby Zamora , taarifa ambazo hata hivyo zimepingwa na kocha huyo pamoja na mchezaji husika.
No comments:
Post a Comment