Search This Blog

Tuesday, October 4, 2011

UTAJIRI WA AUSTRALIAN OPEN KUVUNJA REKODI

Michuano ya wazi ya Australia maarufu kama Australian open inayofanyika kila mwaka huko Melbourne Australia mwakani itaingia kwenye historia ya michezo kwa kuwa michuano yenye zawadi ya kiasi kikubwa cha fedha kuliko michuano yote ya tenis.

Michuano hii itatoa zawadi ya jumla ya dola za kimarekani milioni 25 ambapo washindi kwa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanawake na wanaume wataondoka na dola milioni mbili.

Michuano hiyo kwa mwakani huenda ikaongezewa ladha na ushiriki wa gwiji la tenis kwa wanawake mswisi Martina Hingis ambaye anatarajiwa kushiriki michuano hii kama sehemu yake ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya olimpiki ambapo atashiriki kwenye upande wa mechi za mchanganyiko ambako atacheza sambamba na mswisi mwenzie Roger Federer.

No comments:

Post a Comment