Search This Blog
Thursday, June 2, 2011
YANGA NA SIMBA KUPAMBANA AUGUST 20
Wakati pazia la Ligi Kuu Bara likitarajiwa kufunguliwa Agosti 20, watani wa jadi Simba na Yanga wanatarajia kukutana Agosti 13 katika mchezo wa Ngao ya Hisani kwa ajili kufungua pazia la ligi hiyo.Timu hizi pia zilikutana msimu uliopita
katika mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Yanga iliwafunga Simba, mabao 3-1 katika mechi iliyoamuliwa kwa 'matuta' baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya 0-0 katika Uwanja wa Taifa.
Yanga walipata penalti zao za ushindi kupitia kwa Godfrey Bonny, Stephano Mwasika na Isaack Boakye, wakati Simba walipata penalti moja tu iliyofungwa na kiungo wa zamani ya Yanga, Mohammed Banka.
Mghana, Ernest Boakye alikuwa mpigaji pekee wa Yanga aliyeshindwa kufunga baada ya penalti yake kupanguliwa na kipa wa Simba, Ali Mustapha 'Barthez' wakati wachezaji wa Simba waliopoteza penalti zao walikuwa, Emannuel Okwi, ambaye penalti yake ilipanguliwa, Uhuru Selemani aliyepiga juu na Amri Kiemba aliyegongesha mwamba.
Akizungumzana gazeti hili, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura wakati akitaja kalenda ya matukio ya 2011/12 alisema mchezo huo huwa unatakiwa kuchezwa kati ya bingwa wa Ligi Kuu na yule wa Kombe la FA, lakini kutokana ana kutokuwa na FA kwa sasa huwa anacheza na mshindi wa pili.
"Timu za Simba na Yanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani ambao utakuwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao ambayo itaanza wiki moja baadaye", alisema.
Pia alisema kwa mujibu wa kalenda hiyo msimu wa Ligi Daraja la Kwanza kwa mtindo wa nyumbani na ugenini utaanza Septemba 3 mpaka Oktoba 31, Ligi ya Taifa ngazi ya wilaya Septemba 10 mpaka Desemba 31, Ligi ya Wanawake ngazi ya wilaya Septemba 11 mpaka Oktoba 31.
Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yanayoandaliwa na Shirikishola Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yataanza Julai, Ligi ya Mabingwa Julai na Shirikisho Julai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment