Search This Blog

Thursday, June 2, 2011

JACK WILSHARE - JINSI YA KUWA KIUNGO MZURI


Jack Wilshare ni moja ya viungo wazuri kuwahi kutokea katika katika historia ya soka katika vikosi vya Arsenal na England.

Wilshare ambaye msimu huu amejitokeza kuwa moja viungo wazuri na kuisaidia Arsenal kushika nafasi ya nne katika ligi kuu ya England anaelezea ni mbinu ambazo zinamfanya awe kiungo wa kutumainiwa.

KUJIPANGA UWANJANI
"Kiungo mchezeshaji mzuri anapaswa muda wote kupokea mpira, hapa Arsenal nina bahati kuwa pamoja na Febregas ni mchezaji ambaye utapenda kucheza nae kwa sababu muda wote anakuwa kwenye nafasi na anakupa mpira ukiwa katika nafasi, ananipa muda wa kufikiri jinsi gani anapaswa kutoa pasi na kuendeleza aina ya mchezo wetu"

KUJITAMBUA
"Angalia wenzako pindi mpira unapokujia.Inasaidia kujua nini kinaendelea katika duara lako, kujitambua huku kuna kuruhusu kujua mienendo ya adui na kukufanya ujue.

KUFIKIRIA MBELE
"Ni bora na muhimu kujua nini utafanya utakapopokea mpira kabla haujakufikia.Kabla haujaumiliki unakuwa tayari umeshafikiria nini cha kufanya na mpira unapokujia unaweza ukapiga one touch au ukaupiga mpira kwa mwenzio aliye kwenye nafasi nzuri zaidi"

KUCHEZA KWA NGUVU
"Aina ya mchezo wa Arsenal inanifaa sana kwa style ya kucheza kwangu, inanijengea mazingira mazuri ya kucheza vizuri.Tuna kiungo mmoja mkabaji na wawili wachezeshaji kwa hiyo mfumo wa wa 4-3-3 ni mzuri zaidi katika kuwezesha mchezo kwa kiungo mchezeshaji"

No comments:

Post a Comment