KUUJUA MWILI WANGU
"Kitu kimoja ambacho kiliharibu uwezo wangu nikiwa na Madrid ni kwa sababu nilikuwa sichezi , muda wote nilikuwa naumia kila siku.Nilipokuja Inter nilibadilisha mazoezi na nikapona, kama nilikuwa sijisikii vizuri niliwaambia makocha na nikawa nafanya mazoezi mepesi.Chini ya Mourinho tulikuwa tunafanya hivi na timu nzima ndio maana hatukuwa na majeruhi wengi.Wachezaji tulipewa muda mzuri wa kupona majeraha."
KUJIANDAA VIZURI
"Kabla ya mechi yangu ya kwanza nikiwa na Inter (match ambayo Inter ilishinda 4-0 dhidi ya AC Milan na Sneijder akawa man of the match) coach staff walinipa video za kuwaangalia wachezaji wenzangu na wapinzani wetu.Haikuchukua muda mrefu kuziangalia lakini ilinipa njia ni jinsi gani napaswa kucheza na my team mates dhidi ya wapinzani wetu, pia niliona udhaifu wa wapinzani na jinsi gani napaswa kuutumia udhaifu huo kuwaumiza.Kwahiyo kupitia kujiandaa kwa kuangalia videoz kabla ya match inakupa mwanga ni jinsi gani unapaswa kucheza."
KUPUMZIKA
"Mimi ni moja ya wachezaji ambao pindi mechi inapoisha huwa nafikiria kitu kingine.Huwezi kucheza kwenye kiwango kikubwa kila wiki kama kila siku unawaza kuhusu soka, inabidi ubadilike muda mwingine.Baadhi ya wachezaji wenzangu wa Inter wanacheza tennis na wengine wanakwenda kuvua samaki, mimi sipendi vitu hivyo ndio maana napenda kutumia muda wangu wa ziada kuendesha baiskeli na kuzunguka mitaani, ni njia nzuri ya kupumzika katikati ya mechi kubwa"
KULALA VIZURI
"Sio kitu ambacho wachezaji wengi wanafikiri kinaweza kudhuru jinsi ya kucheza au mazoezi yako siku inayofuata.Mimi napenda kulala japo masaa saba mpaka nane kwa usiku, chini hapo naweza nisicheze vizuri.Nafikiri ndio maana sio vizuri kufikiria kuhusu mpira muda wote kwa sababu kama utafanya hivyo unaweza kuchelewa kulala.Nafikiri kuchelewa kulala kunaweza kusababisha kiwango kupungua kwa hiyo ni vizuri kuacha kuchelewa kulala."
"Muda wote huwa najiandaa kwa kila mchezo katika njia moja.Najiandaa kwa mechi katika muda sahihi kila mechi, nitafika uwanjani nikiwa nasikiliza muziki wa Hip Hop ya kidachi, then navaa jezi na kwenda kupasha mwili.Sio vitu vikubwa lakini vinanisaidia kutulia kabla ya mchezo na kuwa katika akili nzuri".
KUTOJISAHAU
"Tuliposhinda makombe matatu kila mechi ilikuwa kubwa, tulikuwa tunacheza mechi ngumu kwenye ligi halafu na kwenye Champions League na Italian Cup, lakini Jose Mourinho alikuwa anatuambia msikirie kushinda treble, fikirieni kushinda kila mechi.Naamini ukifanya hivi makombe yote yatakuja.Ukiwa unashindania makombe makubwa hautakiwi kufikiria kuyachukua makombe hayo kwa sababu unaweza ukasahau vitu vidogo katika mechi ambazo zitakuletea makombe hayo, hivyo cheza vizuri na makombe utapata."
No comments:
Post a Comment