Search This Blog

Thursday, June 2, 2011

DIEGO FORLAN: MY 24-HOUR FOOD DIARY


Kuna washambuliaji wachache sana ambao unaweza kuwaita deadlier strikers katika ulimwengu wa soka ambao wanamzidi Diego Forlan. Records za Atletico Madrid hitman zinaongea zenyewe, amejishindia Pichichi mara mbili, amepata kiatu cha dhahabu cha ulaya, na amekuwa mchezaji bora ywa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010 akiwa kapteni wa Uruguay.

Anasema siri ya kucheza bila kuchoka na kuwa nguvu muda wote wa mchezo ni vyakula anavyokula kila siku.

Breakfast: Saa 2 asubuhi

Naianza siku kwa sahaniya mananasi, napenda vitu vitamu kwasababu vinauamsha mwili wangu.Baada ya kula matunda kinachofuata nakula brown bread pamoja na yoghurt. Muda mwingine napata mayai ya kukaanga na juisi nzuri ya machungwa, na hiyo inanipata nguvu ya kufanya vizuri mazoezi.

Lunch: Saa mchana

Baada ya masaa mawili au matatu ya mazoezi naenda moja kwa moja kupata chakula cha mchana, sometimes nakula lunch klabuni au katika mgahawa mjini Madrid nikiwa na marafiki na familia yangu.Kwa kawaida nakula tambi au wali na kuku wa kuchoma.


Saa 10: Afternoon snack

Baadae jioni, kawaida huwa napata matunda tofauti kama vile machungwa na mananasi


Saa 3 usiku: Chakula Cha Usiku

Nakula chakula cha mwisho cha siku muda huu, kawaida napata samaki na saladi, napenda sana nyanya na mboga za majani.Nakula vyakula hivi kwa sababu najua ni vizuri kwa afya ya mwili wangu, muda mwingine baada ya dinner napata maziwa kama kinywaji kwasababu mimi sinywi pombe, nilijaribu nilipokuwa mdogo lakini nilishindwa

No comments:

Post a Comment