SERIKALI imejipanga kuitangaza sekta ya utalii hapa nchini kwa kupitia michezo na kwa sasa imeweka mkakati wa kutoa matangazo ya utalii katika viwanja vinane vya soka ulimwenguni vinavyotumiwa na timu za ligi kubwa duniani.
Jumla ya sh5billioni zitatumika kwa zoezi hilo kuitangaza Tanzania katika ligi za England, EPL, Hispania- La Liga, Italia- Seria A, Ufaransa- Lique 1 na Ujerumani- Bundesliga.Mbali na viwanja hivyo pia nafasi hiyo itatumika kuutangana utalii wa Tanzania katika nchi za Ureno, Uholanzi pamoja na Uturuki.
Tamko hilo lilitolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mechi baina ya Drake Univesity ya Marekani na Conadeip ya Mexico uliopigwa ndani ya dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Maige alisema kuwa mbali na wizara yake kutoa matangazo mbalimbali ya utalii katika viwanja mbalimbali vinavyochezwa Ligi Kuu ya England mwaka huu wamejipanga kutangaza vivutio vya utalii katika viwanja vinane vya soka.
Hata hivyo, alisema kuwa wizara yake imejipanga kutenga sh5 billioni kwa lengo la kutangaza vivutio hivyo katika bajeti ya mwaka huu huku akisema kuwa ingawa kiasi hicho cha fedha ni kidogo tofauti na nchi nyingine kama Kenya na wamekuwa wakitenga sh30 billioni kutangaza vivutio vyao.
Hatahivyo, alisema kuwa ugeni wa wanamichezo wa kimarekani 195 si haba kwani utasaidia kuitangaza Tanzania duniani na kusisitiza kuwa siri ya ujio huo ni amani na usalama ambao umetawala hapa nchini
No comments:
Post a Comment