Search This Blog

Tuesday, May 24, 2011

TFF YATOA TAREHE RASMI YA USAJILI WA VILABU.



Wakati ambapo shirikisho la soka la Tanzania TFF likisema kwamba usajili kwa vilabu vya ligi kuu ya kandanda ya Tanzania bara unataraji kuanza mnamo June mbili, tayari vilabu mbalimbali hasa vile vikubwa vimekwishaanza kuvifanyia marekebisho vikosi vyake.

Nyota mbalimbali wamekuwa wakitajwa sana kutoka sehemu mbalimbali kwenda nyingine, ili mwisho wa siku kujipatia ule mkate uliopakwa siagi ya kutosha kwa malisho safi.

Hata hivyo suala la uweledi wazungu wasema professionalism nalo linachukuwa nafasi yake, hasa pale shirikisho la kabumbu la Tanzania TFF, lilipowahi kusema kwamba soka letu sasa ni nusu ya soka la kulipwa, na zaidi na kutokana na kutopatikana kwa mchezaji bora hadi klabu itoe mkwanja wa kutosha.

Ndani ya chama cha wanandinga wa Tanzania, chama hicho kimewataka wanandinga kuwa waangalifu sana juu ya mikataba yao kuelekea kipindi hiki cha kuelekea kwa msimu mpya.

Said George ni katibu mkuu wa chama hicho anasema kwamba, wao kama watetezi wanataka kuwepo kwa utaratibu maalum kuhusu mikataba hiyo, kwani mara nyingi hata klabu hazitimizi wajibu wao kwa wachezaji wao, na hata soka la kulipwa kama linavyosemwa, bado halipo nchini.

No comments:

Post a Comment