Search This Blog

Monday, September 16, 2013

SD TV: MBWANA SAMATTA & THOMAS ULIMWENGU ARE ON FIRE!

EXCLUSIVE: SUALA LA KUBEBA UNGA - "MABONDIA TUNAPONZWA NA NJAA ZETU ZA MAISHA "


Asili ya mabondia wengi duniani wanatoka katika familia duni kwa mfano hapa kwetu ni aghalabu kumkuta bondia ametoka upanga,oysterbay, au masaki ushuwani.nikiwa na maana mabondia wengi wanatoka uswahilini ni watu wa hali duni wengi wetu hatujakalia madawati ya shule wengine tuliojitahidi tumefika darasa la tano au sita kama wazazi walikomaa ndio tunamaliza la saba. 

Baadhi yetu tukiwa na umri wa kuanzia miaka sita nyumbani huwa tunaanza kupewa uzoefu wa kuuza visheti,maandazi,vitumbua,karanga nk na vikibaki nyumbani hauli chakula mpaka viishe, shuleni mwalimu mkali, darasani hafundishi mpaka usome tuisheni ndio unapata kufundishwa kidogo na ukishindwa maswali yake viboko vya ghazabu, hapo ndipo tunapoamua kuachana na shule na kutinga mitaani. 

 Michezo yetu ni katika madampo na vichochoroni na tukifikia umri wa kuanzia miaka 12 na kuendelea tunajua jinsi ya kutafuta pesa kwa kuuza njiwa, kucheza kamari, malani, kuiba kuku na bata, na kwa wale walio watukutu zaidi kuuza na kuvuta bangi ni sehemu ya maisha ya kawaida tu huku mitaani kwetu. Mara nyingi mlo kwetu ni mmoja tu kiubishoo au kuwa wageni ndio tunakula milo miwili. 
Katika maisha yetu muda mwingi tupo huru na michezo kuliko kusoma hasa kolokolo, ngoma, mpira na ngumi, mpira tunacheza mabarabarani, vichochoroni na madampo wakati ngumi tunajifundisha katika makamali vichochoroni au uwani kwa kina masta, begi au tairi limefungwa juu ya mti tizi linaendelea bila vifanyio vya mazoezi vilivyo rasmi mwendo mdundo tunasonga na tunashinda au kufanya vizuri katika mashindano yetu tunayoshiriki na hali yetu duni hii hii ya kimaisha, na majina yetu kutangazwa sana katika vyombo vya habari na kupata umaarufu mkubwa nchini, nchi jirani na hata nchi za ulaya, lakini ukibahatika kututembelea na kuangalia tunapoishi na familia zetu na umaarufu tulionao maisha yetu mabovu yanasikitisha.

Siku za hivi karibuni kuna vimaendeleo kidogo baadhi ya mabondia tunafanya mazoezi katika vilabu vya pombe kwa kuwalipa kodi ya mazoezi wenye bar, naweza sema Tanzania hakuna sehemu rasmi za kufanyia mazoezi ya ndani zilizotengwa na serikali kwa ajili ya raia wake wapenda michezo na kama zipo ni chache katika makambi ya jeshi kwa masharti magumu kwa raia wa kawaida. Siku za nyuma wakazi wa mjini kama vile kisutu, gerezani na kariakoo walikuwa wanafanya mazoezi pale anatoglu, siku hizi huwezi kusikia kuna mwanamichezo katokea gerezani au kariakoo, iliyobaki kwao ni kuuza na kutumia madawa ya kulevya na kukimbizana na wafanyabiashara wa maeneo hayo, naweza ilaumu serikali kwa kutoendeleza michezo bali ilishiriki kuua kabisa michezo maeneo hayo na mengineyo zaidi.

Kwa sisi tulionza kukuwa kimchezo Pambano la ngumi likiandaliwa huwa tunalipwa kuanzia shilingi elfu 5 mpaka 20 kwa mapambano haya madogomadogo na iwapo kutakuwa na pambano kubwa na kupata bahati ya kucheza unaweza lipwa shilingi elfu 40 mpaka laki moja. Mapambano makubwa yanaweza kuwa moja, mawili au matatu kwa mwaka hayazidi hapo, haya mapambano madogo tunaweza pata mawili mpaka sita kwa mwaka. Msiwaone mabondia wakicheza mkadhani wana kipato kikubwa la hasha, ni wale tu wachache waliobahatika kupata wadhamini au waratibu wenye uwezo wa kipesa ndio kidogo hutoka.

Kwa sisi wengine ukiangalia elimu ya kusoma hatuna kazi hakuna na mchezo wa ngumi tunaupenda na pengine tuna vipaji na kwa kufanya vizuri katika mapambano yetu, hivyo mchezo ndio huwa kama ajira zetu kwa sababu tunapata chochote kidogo kupitia mchezo huo kuliko kuiba au kukimbizana na mapolisi katika kamari na kuishia jela.

Kwetu sisi mabondia huona ni jambo la kifahari na hufurahi mno pale tu tunapopata pambano la nje ya nchi na hufurahia kupanda ndege na vile vimisosimisosi tunavyopata tukiwa mahotelini ugenini, tukihadisiana mambo ya safari uswahilini kwetu tunahisi tunakosa mambo mengi ya raha,

Hapo ndipo mawakala wa ngumi hutupata na mabondia huwa wanadiriki kukubali kwenda kucheza popote tukijua tutapanda ndege tunakula raha bila kujali na wala kuhoji tuendako tutalipwa kiasi gani cha pambano nitakalocheza wala kujua usalama wangu.

Ukiangalia umbumbumbu na maskini tulionao mabondia, hapo wajanja wenye pesa zao, wafanyabiashara na baadhi ya viongozi wanatumia udhaifu tulionao mabondia kutuhadaa kwa kutupatia safari za nje za kimichezo au matembezi ya kwenda kufanya mazoezi ughaibuni na hatimae kutubebesha mihadarati(madawa ya kulevya) bila kujua kwa kutuwekea katika mizigo tunayosafiri nayo. Pindi kuna baadhi ya wafanya biashara hao wenye pesa zao hutuweka wazi wakati unaenda pigana umbebee mzigo wake na atakulipa pesa nyingi, hapo ndipo tunapobanwa ukiangalia nyumbani tunalalia telemka tukaze tunashindia tembele mlo mmoja msosi wa kengele tena kwa masimango, mfukoni sina kitu na wala sina kazi itakayonipatia pesa ya kula kwa sasa (hapo sijaingiza mambo ya kodi), demu wangu namlinda vipi?

Hii njaa na umaskini tulio nao mabondia, hapo ndio vigogo wanapoamua kututumia kwa kutubebesha madawa ya kulevya kusafirisha nje wakijua wazi hatuwezi kataa kutokana na dhiki tuliyo nayo, tutakubali tu kwani hakuna apendae kulala njaa, kulala pachafu au kuvaa midabwada.

Siwezi acha dili la pesa kama hili wakati jina langu kubwa kila kona linatajwa mitaani na vyombo vya habari lakini mimi binafsi nauli ya daladala sina, siku ya tatu leo nakula mlo mmoja kwa siku, watoto hawapo katika hali nzuri, mazoezi yenyewe sifanyi kwa raha nafikiria nitapata wapi mshiko, leo unaniletea ishu ya pesa niikatae si nitakuwa kichaa’wadau wenzangu wa ngumi ,wapambe wao, na walio karibu na sisi mabondia wana nguo za bei kubwa wanapendeza , wana magari, ukiangalia mimi bondia ndie mtendaji wao mkuu nipo ovyo sina kitu mfukoni wala tumboni madeni kibao yaani majanga matupu

Ushauri wangu kwa serikali au taasisi zinazohusika na wanaolichukia jambo hili kiukweli maana wengine hujifanya kulichukia mdomoni pembeni ndio watendaji wakuu wa kuwatumia wanamichezo au wasanii kwa faida zao. Mabondia au wanamichezo tuboreshewe maeneo yetu ya michezo ikiwemo katika vilabu vyetu na maeneo ya mazoezi, vifaa viongezwe ikiwezekana kodi ya vifaa vya michezo ipunguzwe ili viwe vingi nchini mabondia wasibabaike na vya kuazima au kuangalia katika tv vifaa nya wenzetu. Serikali iwajali mabondia, isaidie kudhamini semina za walimu wa ngumi ili wawaongoze vema vijana wao.magym ya makusudi yajengwe na maeneo ya wazi wasigawane wenye pesa na viongozi kwa faida zao wajenge sehemu za michezo ya ndani(indoor), na kama pia itatumika njia ya kutoa madarasa matupu katika mashule yetu kwa ajili ya kutuachia sehemu ya mazoezi ya jioni itasaidia sana kukuza mchezo na walimu wenye taaluma kufundisha vizuri kuliko mabondia kufundishana vichochoroni na kutokuwa na nidhamu ya mchezo wala maisha

Na
IBRAHIM ABBAS KAMWE
manager and boxing trainer of Bigright boxing
Local Promoter via Bigright Promotion
Mwananyamala
Dar es salaam

KOMBE LA DUNIA 2014: IVORY COAST VS SENEGAL, MISRI VS GHANA, TUNISIA VS CAMEROON - NANI KWENDA BRAZIL??????

MABINGWA wa soka wa Afrika, Nigeria wamepangwa na timu isiyopewa nafasi sana, Ethiopia, wakati Ghana imekabidhiwa shughuli pevu mbele ya Misri katika mechi za mchujo za kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani Brazil. 
Droo ya mechi hizo imefanyika muda mfupi uliopita
Ivory Coast vs Senegal, Ethiopia vs Nigeria, Tunisia vs Cameroon, Ghana vs Misri, Burkina Faso vs Algeria. Mechi za kwanza za mchujo huo zinatarajia kufanyika kati ya Oktoba 11 na 15, wakati marudiano zitakuwa kati ya Novemba 15 na 19 mwaka huu.

KIBADENI ALIDHISHWA NA KIWANGO SIMBA, MECKY MEXIME AKUBALI KIPIGO


Kocha wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar, Mecky Mexime amekubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na mtandao huu mara baada ya mchezo huo, Mexime ambaye ni nahodha wa zamani wa Taifa Stars amesema, timu yake ilicheza vizuri lakini uwezo ulioonyeshwa na Simba uliwafanya wastahili kupata ushindi.

Alisema kikosi chake kilijitahidi kadiri ya uwezo wake kuweza kupata ushindi lakini makosa mawili waliyofanya yaliiwezesha Simba kupata mabao mawili na kuibuka na ushindi.

“Nimekubali kwamba nimefungwa na Simba kihalali kabisa katika hali ya kawaida ya kimchezo, wenzetu walitumia vyema nafasi walizopata na kuweza kufunga mabao mawili yaliyowawezesha kupata ushindi.

“Timu yangu haikucheza vibaya japokuwa tumefungwa mabao mawili, kilichotokea ni hali ya mchezo ambayo inaweza kuikuta timu yoyote iliyo imara na kutokana na matokeo haya tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo unaofuata ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye ligi,” alisema Mexime.

Kwa upande wake, Kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni alisema kikosi chake kimecheza vizuri hadi kikaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa hali inayompa faraja ya kuwa na kikosi bora msimu huu.

“Siyo siri nawashukuru vijana wangu kwamba wamejituma ipasavyo na kuweza kupata ushindi huu mnono dhidi ya timu hodari kama Mtibwa. Kila idara ilihakikisha inafanya kazi vizuri japokuwa kulikuwa na makosa madogo madogo ambayo natakiwa kuyarekebisha kabla ya mchezo mwingine,” alisema Kibadeni.

Matokeo ya mechi ya jana yameiwezesha Simba kufikisha pointi saba.

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENZETU MORO - NIKKI WA PILI, MWASITI, MRISHO MPOTO WAZUNGUMZA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi,akifafanua namna anavyonufaika na huduma za NSSF,mara tu walipojiunga kupitia kundi lao la Lekadutigite,ndani ya semina ya fursa twendzetu iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.

Meneja huduma wa Wajasiliamali-Zantel akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwenye semina ya Kamata fursa twendzetu,kuhusiana na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo,Semina hiyo iliofanyika ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi iliwakutanisha wadau mbalimbali.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane,ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja na Iringa.

wakifuatilia 


Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba akifunga semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika mapema leo mkoani Morogoro.

 Semina ikiendelea ndani ya ukumbi . 
 Niki wa Pili akielezea fursa mbalimbali wanazoweza kuzitumia vijana katika nafasi mbalimbali wanazozipata,badala ya kubweteka na kusubiri fursa ziwafuate hapo walipo,na pia amewataka vijana wenzake waache kulalama kila kukicha na kuona maisha ni magumu,badala yake wanapaswa kujituma kwa kila nafasi waipatayo.
 Sehemu ya meza kuu ikifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa na wadau ukumbini humo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MaxMalipo,Bwana Ahmed Lussapi akizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye kampuni yake,na pia namna ya kunufaika nalo,amesema kuwa kwa sasa kampuni hiyo imekuwa ikiisaidia jamii katika wigo mpana kwa kutoa huduma mbalimbali,hivyo amewataka vijana kuchangamkia fursa za namna hiyo ili kujikwamua na ugumu wa maisha.
 Mbunifu wa mavazi kutoka mkoani Morogoro,ambaye pia ni mjasiliamali aliyejitambulisha kwa jina la Diana Magessa akionesha mbele ya washiriki wa semina ya Fursa kwa Vijana (hawapo pichani) baadhi nguo zake alizozidizaini kwa ubunifu wake.
 Mrisho Mpoto akisisitiza jambo.
 Mkali wa kughani Mashairi,Mrisho Mpoto akizungumza na wakazi wa Morogoro waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa twendzetu ndani ya ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi
 Baadhi ya wageni waliohudhuria semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa ukumbini humo.
 Mmoja wa wasanii kutoka kundi la Weusi,Niki wa Pili akizungumza mbele ya wakazi wa Morogoro wakati wa semina ya Fusra kwa vijana ikiendelea ndani ya ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya nane,ikiwemo  Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja na Iringa.

KALI YA LEO: MBWIGA MBWIGUKE ALIMVYOMGARAGAZA SHAFFIH DAUDA KWENYE SHINDANO LA UPIGAJI WA PENATI


Shaffi Dauda [kushoto] na Mbwiga Mbwiguke' wakiwa na mwamuzi wakati wakijadiliana kabla ya kuanza kupigiana Penati katika Bonanza la fiesta soka Lililofanyika Mkoani Morogoro 


Shaffi alipata kura hiyo na kumsakizi Mbwiga aanze kupiga 


Mbwiga akipiga akiwa tayari kupiga Penati ambapo watangazaji hao walipiga penati tano tao kila mmoja.


       
Mbwiga akifunga pelnati ya kwanza 


          Akipiga ya pili ambayo pia 


              Shaffi akipiga Penati


Mbwiga na Shaffih wakipongezana mara baada ya kumaliza kupigiana penati, Mbwiga  alifunga penati 3 na kukosa 2.ShaffihDauda aklifunga penati 1 na kukosa 4 

MINZIRO NA JAMHURI KIHWELU MTAKUWA MAKOCHA WASAIDIZI MPAKA LINI?

‘Ikiwa wewe ni kwanza basi we ni wa kwanza, lakini kama wewe ni pili basi hauna kitu.’
Maneno ya Billy Shankly, Gwiji wa Liverpool


Kwanza ni kwanza, pili sio kitu. Labda haya ni maneno makali sana lakini kwenye soka kuwa namba mbili kunakera na sio kitu kizuri kabisa. Wakati gwiji wa soka la Uingereza, Sir Alex Fergusson alipostaafu, msaidizi wake wa siku nyingi, Mike Phelan hata kwa sekunde hakutajwa kurithi mikoba ya bosi wake. Katika soka, muda mrefu zaidi unavyofanya kazi kama msaidizi, ndivyo inavyozidi kuwa ngumu kupata kazi ya kuwa kocha mkuu.


Nchini Tanzania, kuna makocha wawili wenye mapenzi ya dhati na timu kutoka Msimbazi na Jangwani ambao wamekaa muda mrefu sana kama makocha wasaidizi. Fred Felix Minziro ameitumikia Yanga kama mchezaji na kocha kwa muda mrefu bila kuaminiwa na kupewa majukumu ya kuwa kocha mkuu japo hata kwa msimu mmoja mzima. Akiwa tayari ameshaitumikia katika ngazi ya umeneja wa timu na kocha msaidizi kwa muda mrefu, Minziro hajawahi kuaminiwa moja kwa moja kwamba anafaa kuongoza benchi la ufundi; inaaminika kwamba ni kocha msaidizi mwenye upendo, utiifu na mwenye kujitoa kwa ajili ya klabu. 


Kama ilivyo kwa wafanyakazi watiifu, wenye uwezo na kujituma, Minziro ameendelea kuwa na Yanga kwa raha na shida, ameshamwaga machozi, kavuja sana jasho kwa ajili ya kutetea klabu yake lakini siku zote amekuwa haonekani linapokuja suala la kuwa namba moja katika benchi la ufundi.  Wakati wowote ambapo kunauwa na ubadilishaji wa makocha jangwani, mara nyingi amekuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu, akimtaarishia mgeni mazingira mazuri kwenye uongozi wa benchi la ufundi. Hajawahi kuonekana kama anafaa kushika moja kwa moja nafasi hiyo. Kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba wakati kocha mkuu Tom Seintfiet akiwa jukwaani, uongozi ukiwa umegawanyika, Minziro akapewa jukumu la kukaimu nafasi ya ukocha mkuu 0 na baada ya kipigo hicho inaonekana ndio ndoto za kuwa kocha mkuu zimefutika kabisa. Japo halikuwa kosa lake kabisa kwa kipigo hicho ambacho kilichangiwa na ubora wa Simba ya kipindi hicho na mambo ya nje ya uwanja yaliyokuwa yanaisibu Yanga.


Huku Msimbazi, Jamhuri Kihwelo ni kocha msaidizi wa siku nyingi wa Simba. Ameitumikia klabu hiyo katika ngazi tofauti za uongozi lakini mara nyingi amekuwa akifanya kazi kama kaimu kocha mkuu au msaidizi. Amekuwa akilalamika, akiondoka akiwa amekasirika lakini kama mwanaume ambaye hawezi kukaa mbali na mpenziwe kwa muda mrefu siku zote amekuwa akirudi na kuitumikia ndoa yake na Simba. Damu ya Simba inayotembea mwilini mwake inamfanya awe mgumu kuachana moja kwa moja na klabu hiyo.

Haijalishi nini anasema wakati akiondoka Simba, kitu kimoja siku zote kinabaki; Julio na Simba ni marafiki wa siku maisha yote. Mara kadhaa mahusiano ya Julio na Simba yamekuwa yakiharibika lakini Julio kama mtoto mpotevu lazima arudi nyumbani kwao. Mwaka jana walishindwa kumpa kazi wakati mfaransa, Patrick Liewig alipoajiriwa, safari hii tena mwaka huu Kibadeni aliajiriwa kuwa namba moja na Julio ameednelea kuwa msaidizi kama kawaida yake.

Kwa Minziro na Julio, kila mambo yanavyozidi kubadilika ndani ya Simba na Yanga ndivyo wao wanavyozidi kuwa pale pale. Wanaonekana wanafaa kuwa makocha wasaidizi lakini sio makocha wakuu. Kama Kenny Rogers anavyoimba kwenye ‘A soldier’s King’ some are born to serve, some are born to be great…some are born to be forgotten...some are born to be number two?


Imetasfriwa kutoka Lonestrikertz blog

Sunday, September 15, 2013

PICHA: CRISTIANO RONALDO AKISAINI MKATABA MPYA WA KUENDELEA KUICHEZEA REAL MADRID

JOSE MOURINHO AKARIBISHWA EPL NA KIPIGO - EVERTON IKIFUTA UTEJA KWA CHELSEA

MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM: JKT RUVU YAONGOZA LIGI, SIMBA WASHIKA NAFASI YA PILI

Simba SC 2 - 0 Mtibwa Sugar
Mbeya City 1 - 1 Young Africans
Kagera Sugar 1 - 1 Azam FC
Coastal Union 0 - 0 Tanzania Prisons
Ruvu Shooting 1 - 0 Mgambo JKT
JKT Oljoro 1 - 1 Rhino Rangers
Ashanti United 0 - 1 JKT Ruvu


Kwa matokeo haya JKT Ruvu Stars inaongoza ligi kuu kwa kufikisha pointi 9 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 7 na Ruvu shooting yenye pointi 6.

ANGALIA PICHA ZA BONANZA LA SERENGETI SOKA FIESTA LILIVYOFANA MOROGORO

 Mashabiki wa liverpool waliounda timu iliyoshiriki Bonanza na Serengeti soka Fiesta Mkoani Morogoro Ikiwa ni maandalizi ya Tamsha Kubwa la Muziki la Fiesta litakalofanyika Mkoani Morogoro Kesho Katika Uwanja wa Jamuhuri.
 Mtangazaji wa Clouds fm The People Station Mbwiga Mbiguke akiwa ndani ya jezi ya Liverpool wakati wa bonanza hilo  lililovutia wakazi wengi wa Manispaa ya Morogoro.Ambapo Mshindi wa Bonanza hilo hujinyakulia kombe.Timu shiriki huundwa na mashabiki wa vilabu za ulaya waliopo katika moikoa Mbalimbalia hapa nchini.
 Kikosi cha timu ya real Madrid Waliojitokeza kwenye Bonanza hilo
 Mchezaji wa Zamani Mzee Kondo akiwa katika jezi ya Timu ya Manchester United wakati wa bonanza la serengeti soka fiesta Mkoani Morogoro leo.Bonanza hilo limewavutia wakati wa manispaa ya Morogoro wa Rika Mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wa timu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza.
 Wachezaji wa zamani wa timu ya polisi ya Morogoro Mokil Rambo Kushoto Na Delta Thomasi wakiwa katika bonanza hilo leo ambapo walichezea timu ya Manchester United
 Mashabiki waliounda timu ya Ac Milan wakati wa bonanza la Serengeti Soka Fiesta Mjini Morogoro
 Timu ya Arsenal Iliyoshiriki katika Bonanza hilo
 Mashabiki wa Chelsea waliounda timu iliyoshiriki katika Bonanza hilo 
Mashabiki wa bingwa wa ligi kuu England Manchester United waliounda timu iliyoshiriki katika Bonanza La Serengeti Soka Fiesta Mkoani Morogoro
 Mchezaji wa zamani wa Timu ya Sunderlanda na Shujaa Mzee  Sadick Mwambeta naye akivaa tayari katika Bonanza na Serengeti Soka Fiesta
                              
Mashabiki waliounda Timu ya Bayern Munich

Saturday, September 14, 2013

FRANCIS CHEKA APONGEZWA NA MKUU WA MKOANI WA MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akiwasili Kwenye Uwanja wa Shujaa Mkoani morogoro Akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Said Amanzi Wakati  wa hafla fupi ya kumpongeza Bondia Francis Cheka aliyeiletea sifa nchi kwa kushinda ubingwa wa dunia kwa Kwa kumchapa  bingwa wa dunia Mmarekani Bondia Williams 
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akimpokea Bondia Francis Cheka wakati akiwasili uwanjani  katika halfa ya kumpongeza Bondia huyo aliyenyakua Ubingwa wa Dunia Kwa Kumchapa bondia kutoka Marekani.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Akikabidhiwa Mkanda wa Ubingwa wa Dunia kutoka kwa Bondia Francis Cheka Leo Mjini Morogoro
Bondia Francis Cheka akitoa neno la Shukrani na Pembeni yake Ni Mke wa Bondia Huyo
Kocha wa Bondia Huyo Aliyefahamika kwa jina la Komando Akisema Machache wakati wa Halfa hiyo leo
Mkuu wa wilaya ya Mvomero na rais wa Riadha Tanzania Mh Antony Mtaka Akisema machache
Akizungumza katika hafla Mkuu wa Mkoa Mh Joel  Bendera alisema  ushindi wa Cheka ni sifa kwa tanzania katika  mchezo wa ngumi. Bondia Francis Cheka amezawadiwa kiwanja  mabati, na Tani moja ya saruji  Picha na MATUKIO NA MICHAPO BLOG