Search This Blog

Monday, September 16, 2013

MINZIRO NA JAMHURI KIHWELU MTAKUWA MAKOCHA WASAIDIZI MPAKA LINI?

‘Ikiwa wewe ni kwanza basi we ni wa kwanza, lakini kama wewe ni pili basi hauna kitu.’
Maneno ya Billy Shankly, Gwiji wa Liverpool


Kwanza ni kwanza, pili sio kitu. Labda haya ni maneno makali sana lakini kwenye soka kuwa namba mbili kunakera na sio kitu kizuri kabisa. Wakati gwiji wa soka la Uingereza, Sir Alex Fergusson alipostaafu, msaidizi wake wa siku nyingi, Mike Phelan hata kwa sekunde hakutajwa kurithi mikoba ya bosi wake. Katika soka, muda mrefu zaidi unavyofanya kazi kama msaidizi, ndivyo inavyozidi kuwa ngumu kupata kazi ya kuwa kocha mkuu.


Nchini Tanzania, kuna makocha wawili wenye mapenzi ya dhati na timu kutoka Msimbazi na Jangwani ambao wamekaa muda mrefu sana kama makocha wasaidizi. Fred Felix Minziro ameitumikia Yanga kama mchezaji na kocha kwa muda mrefu bila kuaminiwa na kupewa majukumu ya kuwa kocha mkuu japo hata kwa msimu mmoja mzima. Akiwa tayari ameshaitumikia katika ngazi ya umeneja wa timu na kocha msaidizi kwa muda mrefu, Minziro hajawahi kuaminiwa moja kwa moja kwamba anafaa kuongoza benchi la ufundi; inaaminika kwamba ni kocha msaidizi mwenye upendo, utiifu na mwenye kujitoa kwa ajili ya klabu. 


Kama ilivyo kwa wafanyakazi watiifu, wenye uwezo na kujituma, Minziro ameendelea kuwa na Yanga kwa raha na shida, ameshamwaga machozi, kavuja sana jasho kwa ajili ya kutetea klabu yake lakini siku zote amekuwa haonekani linapokuja suala la kuwa namba moja katika benchi la ufundi.  Wakati wowote ambapo kunauwa na ubadilishaji wa makocha jangwani, mara nyingi amekuwa akikaimu nafasi ya kocha mkuu, akimtaarishia mgeni mazingira mazuri kwenye uongozi wa benchi la ufundi. Hajawahi kuonekana kama anafaa kushika moja kwa moja nafasi hiyo. Kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba wakati kocha mkuu Tom Seintfiet akiwa jukwaani, uongozi ukiwa umegawanyika, Minziro akapewa jukumu la kukaimu nafasi ya ukocha mkuu 0 na baada ya kipigo hicho inaonekana ndio ndoto za kuwa kocha mkuu zimefutika kabisa. Japo halikuwa kosa lake kabisa kwa kipigo hicho ambacho kilichangiwa na ubora wa Simba ya kipindi hicho na mambo ya nje ya uwanja yaliyokuwa yanaisibu Yanga.


Huku Msimbazi, Jamhuri Kihwelo ni kocha msaidizi wa siku nyingi wa Simba. Ameitumikia klabu hiyo katika ngazi tofauti za uongozi lakini mara nyingi amekuwa akifanya kazi kama kaimu kocha mkuu au msaidizi. Amekuwa akilalamika, akiondoka akiwa amekasirika lakini kama mwanaume ambaye hawezi kukaa mbali na mpenziwe kwa muda mrefu siku zote amekuwa akirudi na kuitumikia ndoa yake na Simba. Damu ya Simba inayotembea mwilini mwake inamfanya awe mgumu kuachana moja kwa moja na klabu hiyo.

Haijalishi nini anasema wakati akiondoka Simba, kitu kimoja siku zote kinabaki; Julio na Simba ni marafiki wa siku maisha yote. Mara kadhaa mahusiano ya Julio na Simba yamekuwa yakiharibika lakini Julio kama mtoto mpotevu lazima arudi nyumbani kwao. Mwaka jana walishindwa kumpa kazi wakati mfaransa, Patrick Liewig alipoajiriwa, safari hii tena mwaka huu Kibadeni aliajiriwa kuwa namba moja na Julio ameednelea kuwa msaidizi kama kawaida yake.

Kwa Minziro na Julio, kila mambo yanavyozidi kubadilika ndani ya Simba na Yanga ndivyo wao wanavyozidi kuwa pale pale. Wanaonekana wanafaa kuwa makocha wasaidizi lakini sio makocha wakuu. Kama Kenny Rogers anavyoimba kwenye ‘A soldier’s King’ some are born to serve, some are born to be great…some are born to be forgotten...some are born to be number two?


Imetasfriwa kutoka Lonestrikertz blog

1 comment:

  1. Nadhani kuna mambo mengi ya kuandika kuhusu soka letu lakini sio kwa huu utumbo ulio andika hapa,sasa una walaumu au ndo unataka watoke kwenye hizo timu,je minziro haja wahi kuwa kocha mkuu wa timu za tanzania na julio pia,acha ubabaishaji,how mwanafunzi ana maliza shule na chuo na mwisho wa siku anakuja kufundisha nae lkn hawi mwalimu mkuu vp hawa mbona hauwataki nao walilie uwalimu mkuu.by kuntah kinte.

    ReplyDelete