Search This Blog

Thursday, August 16, 2012

KAMA BIN KLEB NA MBUYI TWITE VILE!

TAIFA STARS VS BOTSWANA KTK PICHA !


 Mshambuliaji wa Taifa Stars Mrisho Ngassa akijaribu kumtoka beki wa timu ya Botswana, Zebras Oscar Neenga wakati wa mechi Kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Molopolole mjini Gaborone Bostwana, timu hizo zilitoka Sare ya kufungana mabao 3-3.

Mabeki wa timu ya taifa ya taifa stars wakimwangilia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Botswana akifunga bao la tatu wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Molepolole mjini Gaborone

ARSENAL IPO TAYARI KUMUUZA ALEX SONG KWA FC BARCELONA.

Tweets 

Arsenal ready to give green light for £15m Song move to Barcelona: The Spanish giants have agreed to meet the Gunners! Tweet Sponsored @Zanteltz

QUIZ: TAJA JINA LA MCHEZAJI WA MWISHO KUHAMIA MAN UTD AKITOKEA ARSENAL.

TAKWIMU MBALI MBALI ZA RVP KWA KIPINDI ALICHOKAA ARSENAL.

KUTOKA KWA MDAU Pirmin Mzenga

Habari kaka....napenda kuwapongeza mashabiki wote wa Man Utd kwa kufanikiwa kumsajiri RVP.......bila shaka rejeo la mail yangu ni kuwaeleza umma wa watanzania na mashabikia wote dunia nzima, its coming back of the REDS! Kaka Shaffih nimefarijika sana namwenendo wa bwana Brenda Rodgers kiukweli nategemea kuiona Liverpool mpya, mambo mapya,na mataji mapya............................bila shaka tutafanya vizuri pia mashabiki wote wa Liverpool inawapasa wawe wavumilvu, wampe muda Rodgers atatufikisha tunapotaka....."YOU WILL NEVER WALK ALONE"

HUYU NDIO MTANGAZAJI TV MAARUFU SHABIKI WA ARSENAL ALITISHIA KUJIUA ENDAPO VAN PERSIE ANGEONDOKA ARSENAL.

Mtangazaji maarufu wa kituo cha CNN raia wa Uingereza Piers Morgan ambaye anatambulika kwa mapenzi yake aliyonayo juu ya klabu ya Arsenal FC - Piers Morgan jana alitoa mpya katika mtandao wa Twitter.

Huku kukiwa kumebakiwa na masaa kadhaa kabla ya Arsenal kuthibitisha kwamba wamekubalina bei ya ada ya uhamisho wa Robin van Persie kwenda Manchester United, Piers Morgan alikuwa akitoa kauli za kuomba nahodha wao asiondoke klabuni kwao, na hata kama ikiwa anaondoka basi asiuzwe kwa klabu ambayo anadai ni wapizani wao nchini Uingereza.

Baada ya mfululizo wa tweets za namna hiyo baadae kama alifikiria nini kitatokea baada ya muda mchache akaandika tweet iliyokuwa na ujumbe wa moja kwa moja kwenda Van Persie ukisema "Sio kama nakupa presha Van Persie - lakini ikiwa utaondoka #Arsenal then nitaenda kujirusha mwenyewe kwenye daraja la ya Santi Monica."



MAREKANI YAIFUNGA MEXICO KWA MARA YA KWANZA NCHINI KWAO

Baada ya mechi 24 ndani yamiaka 75 ya upinzani wa jadi kati ya Mexico na Marekani, hatimaye watoto wa Obam a walifanikiwa kupata ushindi wao kwanza kabisa katika ardhi ya Mexico jana katika mechi ya kirafiki iliyofanyika katika dimba la Azteca - Mexico.

PICHA YA SIKU: HIZI NDIO HASIRA ZA MASHABIKI WA ARSENAL DHIDI YA VAN PERSIE

Muda mchache baada ya vilabu vya Arsenal na Man United kuthibitisha kwamba vimekubalina ada ya uhamisho wa mchezaji RobinVan Persie kujiunga na mashetani wekundu - baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakipost picha mitandaoni kuonyesha namna walivyopokea taarifa za nahodha wao kwenda Old Traford. Wapenzi wa Arsenal vipi? KAMA YOYOTE AMBAYE ANATAKA KUONYESHA HASIRA ZAKE KAMA HAWA ATUME PICHA AU MAONI KWENYE EMAIL HII - shaffidauda@gmail.com

MRISHO NGASSA AIOKOA STARS NA KIPIGO BOTSWANA - YATOKA SARE YA 3-3

Taifa Stars imetoka sare ya mabao 3-3 na wenyeji Botswana (Zebras) katika moja kati ya mechi kadhaa za kirafiki za kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) zilizochezwa leo (Agosti 15 mwaka huu) usiku.
 
Hadi mapumziko kwenye mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Molepolole ulioko Kilometa 40 nje ya Jiji la Gaborone, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2. Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 lililofungwa kwa penalti na beki Erasto Nyoni.
 
Mwamuzi Lekgotia Johannes Stars alitoa adhabu hiyo baada ya beki Oscar Obuile Ncenga wa Zebras kumuangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyekuwa akimkabili kipa Mompoloki Sephekolo.
 
Bao hilo halikudumu muda mrefu, kwani Zebras walisawazisha dakika ya 26 baada ya shuti kali lililopigwa na
Lemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja. Dakika tano baadaye kiungo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars bao la pili kwa shuti la mbali.
 
Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37. Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi kutoka wingi ya kushoto uliopigwa na Tebogo Sembowa ambaye kabla alimtoka beki Aggrey Morris.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa Kocha Kim Poulsen wa Stars kuwatoa Frank Domayo na Salum Abubakar na nafasi
zao kuchukuliwa na Shabani Nditi na Athuman Idd. Safari hii Zebras ndiyo walioanza kufunga dakika ya 69 ambapo kiungo Michael Mogaladi aliifungia bao la tatu kwa kichwa akiunganisha krosi fupi iliyotokana na mpira wa kurusha.
 
Dakika 13 za mwisho Stars walicheza pungufu baada ya beki Erasto Nyoni kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu mshambuliaji Lovemore Murirwa.
 
Mrisho Ngasa ambaye alikuwa nyota kwenye mchezo huo aliisawazishia Stars dakika ya 84 baada ya kugongeana one-two na mshambuliaji Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Moshi.
 
"Licha ya timu kucheza vizuri, tatizo kubwa lilikuwa kwenye safu ya ulinzi ambapo mabeki waliruhusu mipira mingi ya krosi na kuwaacha washambuliaji wa Botswana wakifunga bila bughudha. Mabeki hawatakiwi kuruhusu mipira ya krosi, wakiruhusu ni lazima wahakikishe wanawadhibiti washambuliaji wa timu pinzani.
 
"Kwa upande wa washambuliaji, Said Bahanuzi alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars tangu nilipomjumuisha kwenye timu kwa mara ya kwanza. Kuna makosa madogo madogo ambayo niliyatarajia, hivyo nitamrekebisha polepole," alisema Kocha Poulsen mara baada ya mechi hiyo.
 
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo/Shabani Nditi,
Mrisho Ngasa, Salum Abubakar/Athuman Idd, Said Bahanuzi/Simon Msuva, Haruna Moshi/Ramadhan Singano na Mwinyi Kazimoto.
 
Zebras; Mompoloki Sephekolo, Tshepo Motlhabankwe/Tshepo Maikano, Edwin Olerile, Oscar Obuile Ncenganye, Mompati Thuma, Patrick Motsepe/Jackie Mothatego, Lemponye Tshireletso, Michael Mogaladi, Tebogo Sembowa, Ntesang Simanyana na Galabgwe Moyana/Lovemore Murirwa.
 
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inarejea nyumbani kesho (Agosti 16 mwaka huu) ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.

ROBIN VAN PERSIE NA CESC FABREGAS - WALIVYOFANYA TAREHE 15 AUGUST KUWA MBAYA KATIKA HISTORIA YA ARSENAL


Tarehe 15 ya August itaendelea kuwa tarehe ya maumivu kwa washabiki wa Arsenal milele.
Kwanini?


Kwanini?

Msimu uliopita mnamo tarehe 15, mwezi kama huu yaani August, Arsenal walimuuza nahodha wao na kiungo wa kutegemewa Cesc Fabregas waliomsajili na kukaa nae kwa takribani miaka 8. 


Pia tarehe kama ya leo (15th August) Arsenal wanakubaliana ada ya uhamisho na mahasimu wao Manchester United kwa ajili ya nahodha na mshambuliaji wao wa kutumainiwa Robin van Persie kujiunga na Mashetani wekundu.



Kwa maana hiyo Cesc Fabregas na Van Persie ambaye nae amekaa Arsenal kwa miaka nane toka 2004-2012 wanaifanya tarehe hii (15th August) kuwa kumbukumbu mbaya kwa mashabiki wa klabu yao ya zamani - Arsenal.


UFANANO WAO
1: Wote wemakaa Arsenal kwa miaka nane, Fabregas kutoka 2003 - 2011, Van Persie 2004-2012.

2: Wote walikuwa manahodha wa Arsenal mpaka wakati wanauzwa.

3: Wote wameondoka Arsenal katika tarehehe moja. 

R.I.P TO ARSENAL - RVP MANCHESTER UNITED

By Aidan Seif Charlie

Wednesday, August 15, 2012

HAYA NDO MAJEMBE MAPYA YA SIMBA!

Mohamed Nassor (kushoto) akimshuhudia mshambuliaji  wa klabu ya Simba, Daniel Akuffo akisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo. 

 
Mohamed Nassor (kushoto) akimshuhudia beki mpya ,Paschal Ochieng akisaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo.
Ochieng kulia na Akuffo kushoto

SIMBA B YAIRARUA AZAM FC NA KUTINGA FAINALI SUPER8 CUP



Timu ya soka ya Simba B imeifunga timu ya Azam katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Super 8 katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yalifungwa na wachezaji na wachezaji Rashid Ismial na Haroun Athumani wakati goli la kufutia machozi la Azam lilifungwa na beki wake wa kutumainiwa Saidi Morad.

Kwa ushindi huo Simba itacheza fainali ya Super 8 siku ya Jumamosi dhidi ya wakata miwa wa manungu Mtibwa Sugar ambao mapema leo waliwafunga Jamhuri ya Pemba mabao 5-1.

Simba leo waliwakilishwa na kikosi cha Abuu Hashimu(18), Miraj Adam (19), Omary Salum (11)/William Lucian ‘Gallas’, Hassan Isihaka (5), Hassan Hatibu (15) Said Ndemla (13), Haroun Athumani (7), Abdallah Seseme (17), Rashid Ismail (8), Edward Christopher (9)/Ramadhan Mzee na Frank Sekule (4)Ibrahim Ajibu.
Benchi; Saleh Malande (1), Ramadhan Mzee (2), William Lucian ‘Gallas’(3), Kenny Alex (12), Mohamed Salum (16), Ibrahim Ajibu (20) na Jesse Nyambo (14).
Makocha: Suleiman Matola. Msaidizi; Amri Said.

Azam FC - Wandwi Jackson (18), Ibrahim Shikanda (21), Samir Hajji Nuhu (11), Said Mourad (15), Luckson Kakolaki (5), Abdulhalim Humud (24), Sunday Frank (12), Jabir Aziz (25)/Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba (17)/Zahor Pazi, Abdi Kassim (20) na Kipre Herman Tcheche (27)Hamisi Mcha.

Benchi; Aishi Mfula (1), Omary Mtaki (2), Himid Mao (23), Khamis Mcha (22), Kelvin Friday (28). Abdulghani Gullam (14) na Zahor Pazi (9).
Makocha: Boris Bunjak (Serbia). Msaidizi; Vivek Nagul (India).

PAMOJA NA KUFANYIWA OPERATION YA MOYO - MADAKATARI WAMWAMBIA MUAMBA HAWEZI KUCHEZA SOKA TENA - ATANGAZA KUSTAAFU



Hatimaye mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ametangaza kuachana na soka leo hii kutokana na ushauri wa daktari.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Congo, alipata mshtuko wa moyo wakati wa mechi ya FA Cup dhidi ya Tottenham, amesema ana uchungu mkubwa kuachana na kucheza soka lakini hana budi zaidi ya kuweka mbele afya yake.

Muamba ameishukuru sana timu ya madaktari kwa kuokoa maisha yake na ameshukuru kwa maombi na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa wapenzi wote wa soka duniani.

Moyo wa Muamba ulisimama kwa saa 78 baada ya kudondoka kwenye dimba la White Hart Lane baada ya kupatwa mshtuko wa moyo hali iliyopelekea kufanyiwa matibabu na kuweza kuokoa maisha yake.

Alikaa mwezi mzima Hosptali lakini aliwashangaza madaktari kwa jinsi alivyopata nafuu kwa haraka huku akisistiza anataka urudi kwenye dimba aendelee kucheza soka.

Kiungo huyo wa Bolton na England alienda mpaka nchini Ubelgiji wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuweza kuwa fiti kwa ajili kurudi uwanjani.


Mchumba wake Shauna ali-tweet kuwaambia mashabiki wa Muamba kwamba operation imeenda vizuri na atarudi kucheza soka kwa nguvu kuliko ilivyokuwa mwanzoni, lakini siku moja baadae madaktari wakampa taarifa mbaya kwamba kurudi kucheza soka kutahatarisha maisha yake kwa kuwa moyo wake hauwezi kuhimili.

Kabla ya kutangaza kustaafu Mumba aliwaambia mashabiki wake waendelee kutabasamu na kila kitu kitakuwa poa.

Historia yake ya soka na kuanza kujulikana ilianzia katika academy ya soka ya Arsenal mwaka 2002 kabla ya kuhamia Birmingham na baadae akaenda Bolton mwaka 2008.

SIKU YA MWISHO YA USAJILI TANZANIA: YANGA YAWASILISHA MAJINA YA WACHEZAJI WAO WALIOWASAJILI MSIMU HUU

Young Africans imewasilisha jumla ya majina ya wachezaji  28 kwa shirikisho la soka nchini TFF, kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu nchini inayotazamiwa kuanza mapema septemba mosi.

Katibu mkuu wa Young Africans Mwesigwa Selestine amesema wamepeleka majina ya wachezaji wote 28 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu, na hii ni kutokana na benchi la ufundi kuridhia kuwatumia wachezaji wote.


Aidha katika usajili huo uliowasilishwa leo, umeambatana na usajili wa wachezaji wa timu ya vijana U-20 ambapo majina ya wachezaji mahiri wa timu ya Taifa Saimon Msuva na Frank Domayo.
Usajili  kamili kwa timu ya wakubwa ni kama ifuatavyo:
Walinda Mlango:
Yaw Berko, Ally Mustafa 'Barthez' na Said Mohamed 
Walinzi wa pemebeni:
Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika
Walinzi wa kati:
Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo
Viungo wa ulinzi:
Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif Kijiko na Salum Telela
Viungo wa pembeni:
Nizar Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme 
Viungo washambuliaji:
Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari 
Washambuliaji:
Said Bhanaunzi, Hamis Kiiza 'Diego', Didier Kavambagu na Jeryson Tegete

Majina hayo yanakamilisha jumla ya 28 ya wachezaji kwa timu ya wakubwa.
Kikosi cha U-20 kina jumla ya majina 22 ambao ni:
Walinda Mlango: Geofrey Nyalusi na Yusuf Abdul
Walinzi: Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said
Viungo: Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah 
Washambuliaji wa pembeni: Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum, Rehani Kibingu
Washambuliaji: Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo 
NB: Frank Domayo & Saimon Msuva usajili wao umepelekwa katika usajili wa U-20 lakini wataitumikia timu ya wakubwa 

www.youngafricans.co.tz

WANAJESHI WA STARS WAPIGA TIZI USIKU KUHAKIKISHA WANAWAFUNGA BOTSWANA



Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa mazoezini katika Viwanja vya benki ya Botswana kujiandaa na mechi dhidi ya The Zebras ya Botswana ambayo inatarajiwa kupigwa leo jioni nje kidogo ya Mji wa Gaborone.

KAULI YA SIKU: MOURINHO - NIPO PEKEE YANGU KWENYE SOKA

"Mimi ndio kocha pekee ambaye nimeshinda makombe ya ligi katika nchi tatu kubwa tofauti. Hivyo nafikiri, itabidi badala kuniita "Special One" muanze kuniita "Only One"."
Aliongea maneno haya kocha wa Real Madrid akitambia mafanikio yake.

PAMOJA NA KUKAMATWA NA COCAINE KILO SITA NA KUFUNGWA, MCHEZAJI AENDELEA KUKIPIGA URAIANI

Mwaka 2010, mcheza soka wa kirusi Maksim Molokoedov alikamatwa huko Santiago, Chile kwa kujaribu kuingiza kilo sita za madawa ya kulevya aina ya Cocaine kupitia vitabu vya watoto vya kusomea. Alihukumiwa kwenda jela miaka 3 na siku moja japokuwa akiwa bado na mwaka mmoja wa kifungo chake , amepewa ruhusa ya kuichezea klabu ya daraja la pili ya nchi Santiago Morning.


Akiwa chini ya ulinzi wa walinzi wa jela, mchezaji huyo mwenye miaka 24 huwa anafanyamazoezi na kucheza mechi mchana na jioni anarudi jela kuendelea kutumikia adhabu yake. Kabla ya kukamatwa kwake, alikuwa akiichezea klabu ya Pskov-74, timu ya daraja la pili nchini Urusi.

Mapenzi yake na soka yamemfanya Molokoedov ambaye ana kipaji kikubwa - kuendelea kupata special treatment huko jela.

Tuesday, August 14, 2012

kampuni ya bia ya serengeti yamkabidhi Mshindi wake wa gari promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo mjini dodoma leo.

Mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro ambaye ni   mkazi wa Dodoma ambae ni mtaalamu wa mambo ya bomba,akiwasha mchuma wake tayari kuaondoka nalo huku shamra shamra za hapa na zikiwa zimetawala kutoka kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye tukio hilo adhimu kabisa.
Mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro  akiingia ndani ya gari yake aina ya Ford Figo baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru, hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia, wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Allan Chonjo, meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager sambamba na Wanahabari .
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru  akimkabidhi kadi ya gari mshindi wa gari wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia wakiwemo Wanahabari ndugu jamaa na marafiki.
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Bw. Ephraim Mafuru  akimkabidhi funguo ya gari lake mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma. Wanaoshuhudia katikati yao ni Baba yake Mzee Augustine Tengia wakiwemo Wanahabari ndugu jamaa na marafiki.
Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Bwa. Allan Chonjo akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali na wadau wengine kutoka sehemu mbalimbali waliofika kulishuhudia tukio la kukabidhiwa kwa gari aina ya Ford Figo kwa mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro kwenye hafla fupi iliyofanyika jioni ya leo ndani ya bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma.
Mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro akifurahia zawadi hiyo na Mama yake Mzazi ambaye pia alikuwepo kulishuhudia tukio hilo lililofanyika jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma.
Mshindi wa shindano la Vumbua Hazina chini ya Kizibo  Bw. Amin Joseph Maro akizungumza mbele ya Wanahabari waliofika kulishuhudia tukio hilo jioni ya leo kwenye bustani ya Nyerere Square mjini  Dodoma,kulia kwake ni Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia.
Baba yake Mzazi Mzee Augustine Tengia akizungumzia furaha alionayo mbele ya Wanahabari mara baada ya mtoto wake kujishindia gari mpya kabisa aina ya  Ford Figo kupitia promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.

TAIFA STARS YAWASILI SALAMA GABORONE TAYARI KUUMANA NA WABOTSWANA





Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikiwa na wachezaji 17 kimewasili leo asubuhi jijini Gaborone tayari kwa mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji Botswana 'Zebras' itakayochezwa kesho (Agosti 15 mwaka huu).

Stars ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sir Seretse Khama saa 5.45 asubuhi kwa saa za hapa ambapo nyumbani ni 6.45 na kupokewa na viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Botswana (BFA) na Watanzania wanaoishi hapa Botswana.

Baadhi ya wachezaji walioko kwenye kikosi hicho ni Frank Domayo, Ramadhan Singano na Simon Msuva ambao walijiunga na Stars saa chache baada ya kurejea kutoka Nigeria ambapo walikuwa na timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ambayo Jumapili ilicheza mechi ya mashindano ya Afrika dhidi ya Nigeria (Flying Eagles).

Wachezaji wengine kwenye kikosi kilichoko Botswana ni Aggrey Morris, Amir Maftah, Athuman Idd, Erasto Nyoni, Haruna Moshi, Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Mwadini Ally, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Chombo, Salum Abubakar, Said Bahanuzi na Shabani Nditi.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia kwenye hoteli ya Oasis ambayo pia ndipo Zebras imepiga kambi kwa ajili ya mechi hiyo. Mechi itaanza kesho saa 1 kamili usiku kwa saa za hapa na itafanyika kwenye Uwanja wa Molepolole Sports Complex. Uwanja wa Taifa wa Botswana hivi sasa uko kwenye matengenezo.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema mechi hiyo ni muhimu kwa vile timu yake bado
inakabiliwa na mechi za Kombe la Dunia Kanda ya Afrika, na michuano ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) inayotarajia kuanza baadaye mwaka huu.

HUYU NDIO KINDA MPYA ALIYESAJILIWA LEO NA MANCHESTER UNITED BAADA YA KUFUZU VIPIMO


Fighting fit: Angelo HenriquezNew recruit: Angelo Henriquez

 Angelo Henrique

KALI YA LEO: INAWEZEKANA HII NDIO SABABU MOJAWAPO YA BRAZIL KUSHNDA MEDALI YA SILVER KWENYE OLYMPIC

Karibia asilimia tisini ya majina ya wachezaji waliokuwa wakiunda kikosi cha Brazil kilichoshiriki kwenye michezo ya Olympic kwa upande wa soka, majina yao yalikuwa yakihusisha neno"Silva" - Baasi kuna baadhi ya vyombo vya habari huko duniani wamefanya utafiti na kugundua kwamba inawezekana majina ya wachezaji wa timu ni nuksi na ndio maana wameishia kushinda medali ya silva kwenye Olympic. Je wewe una maoni gani?

MSAADA TUTANI: WAZEE WA KUALA LUMPUR NAOMBA MNITAJIE MAJINA YA KIKOSI HIKI CHA MABINGWA WA KAGAME


TAIFA STARS YAONDOKA JANA USIKU KUELEKEA GABORONE - BOTSWANA

Timu ya taifa ya soka ya Tanzania - Taifa Stars usiku wa kuamkia leo imesafiri kuelekea jijini Gbarone Botswana kwa ajili ya kucheza mchezo wa kujipima nguvu na timu ya nchi hiyo.

Nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja akiingia uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kuelekea Botswana

Watoto wa Msimbazi hao, Haruna Moshi Boban na Ramadhan Chombo wakiwa na mabegi tayari kuiacha ardhi ya Tanzania na kwenda Botswana kutetea bendera ya nchi yao.

Mrisho Khalfan Ngassa nae akielekea ndani ya uwanja tayari kwenda kupanda pipa na kwenda Gabarone

Aggrey Morris wa Azam FC NDANI YA UZI WA TAIFA LAKE TAYARI KUKWEA PIPA

MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI SIMBA HANS POPE ATOA YA MOYONI - ASEMA YANGA WALIANZA NA BAHANUZI, KAVUMBAGU, TWITE, NA SASA WANAMUWINDA PASCAL OCHIENG

Said Bhanuzi na Didier Kavumbagu wakitambulishwa na Msemaji wa Yanga Luis Sendo - wachezaji hawa wawili Simba inadai Yanga imefanyia uhuni kama ilivyokuwa Mbuyi Twite.

Usajili wa Mbuyu Twite aliyejiunga Yanga, huku Simba nayo ikiingia naye mkataba, umeendelea kuwa 'kivutio', ambapo sasa Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na madai mapya.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope ameilaumu Yanga kwa kuuingiza mchezo wa soka kwenye machafuko.

Pope amesema kitendo cha wenzao kuwazunguka na kumshawishi Twite kurejesha fedha walizompa ili asajili Simba, kinaweza kuleta uhasama usio na ulazima."Tumepata taarifa kuwa baba mzazi wa Mbuyu (Twite) amemkataza mwanaye kuja kuichezea Yanga kwa hofu maisha yake."

"Mzee Twite anataka Simba na Yanga zikutane kufanya mazungumzo kwa lengo la kuweka mambo sawa kisha ndipo amruhusu kuja Tanzania," alisema Pope.

"Unadhani kwa kitendo walichofanya Yanga, mashabiki wa Simba watafurahi? Baba yake mzazi (Twite) amechukizwa na hali hiyo, anahofia usalama wa kijana wake," alisema Pope.
"Vita ya soka haina tofauti na ile ya siasa au dini. Kwa hiyo baba mzazi wa Mbuyu ameomba Yanga na Simba kumaliza suala hili mwanaye aweze kucheza soka kama ilivyo kazi yake."

Katika kusisitiza ukweli wa madai yao, Pope alisema tayari uongozi wa Yanga umeomba kukutana nao ili kuzunguza na kumaliza suala hilo.
"Ukweli ni kamba, hatuna tatizo na Yanga. Nafikiri siyo mara yao ya kwanza wala mwisho kutufanyia mchezo huu mchafu. Ni kawaida yao."

"Wameomba [Yanga] tukutane ili kumaliza utata wa suala hili, vinginevyo Twite hatakuja siyo kujiunga na Yanga au Simba, bali haji kabisa."
Aliongeza: "Tulianza mazungumzo na Bahanuzi (Said)wakatuzunguka na kumsainisha, ikawa hivyo tena kwa Kavumbagu (Didier) na sasa wametuma viongozi Kenya kutaka kumsainisha Pascal Ochien ambaye yupo na timu Arusha."

Pascla Ochieng - mchezaji mpya wa Simba ambaye Hans Pope Yanga wameshaanza kumuwinda.

"Nafikiri Yanga kama wanataka kulipa kisasi cha mabao matano tuliyowafunga, wacheze mpira na siyo kutuzunguka na kusajili wachezaji wetu."
"Hata sisi tunaweza mchezo huo mchafu---ni kweli tunaweza kuwafanyia, lakini hatuoni sababu ya kufanya hivyo," alisema zaidi Pope.


Source: Mwananchi.co.tz