Search This Blog

Tuesday, August 14, 2012

MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI SIMBA HANS POPE ATOA YA MOYONI - ASEMA YANGA WALIANZA NA BAHANUZI, KAVUMBAGU, TWITE, NA SASA WANAMUWINDA PASCAL OCHIENG

Said Bhanuzi na Didier Kavumbagu wakitambulishwa na Msemaji wa Yanga Luis Sendo - wachezaji hawa wawili Simba inadai Yanga imefanyia uhuni kama ilivyokuwa Mbuyi Twite.

Usajili wa Mbuyu Twite aliyejiunga Yanga, huku Simba nayo ikiingia naye mkataba, umeendelea kuwa 'kivutio', ambapo sasa Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka na madai mapya.
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili klabu ya Simba, Zacharia Hans Pope ameilaumu Yanga kwa kuuingiza mchezo wa soka kwenye machafuko.

Pope amesema kitendo cha wenzao kuwazunguka na kumshawishi Twite kurejesha fedha walizompa ili asajili Simba, kinaweza kuleta uhasama usio na ulazima."Tumepata taarifa kuwa baba mzazi wa Mbuyu (Twite) amemkataza mwanaye kuja kuichezea Yanga kwa hofu maisha yake."

"Mzee Twite anataka Simba na Yanga zikutane kufanya mazungumzo kwa lengo la kuweka mambo sawa kisha ndipo amruhusu kuja Tanzania," alisema Pope.

"Unadhani kwa kitendo walichofanya Yanga, mashabiki wa Simba watafurahi? Baba yake mzazi (Twite) amechukizwa na hali hiyo, anahofia usalama wa kijana wake," alisema Pope.
"Vita ya soka haina tofauti na ile ya siasa au dini. Kwa hiyo baba mzazi wa Mbuyu ameomba Yanga na Simba kumaliza suala hili mwanaye aweze kucheza soka kama ilivyo kazi yake."

Katika kusisitiza ukweli wa madai yao, Pope alisema tayari uongozi wa Yanga umeomba kukutana nao ili kuzunguza na kumaliza suala hilo.
"Ukweli ni kamba, hatuna tatizo na Yanga. Nafikiri siyo mara yao ya kwanza wala mwisho kutufanyia mchezo huu mchafu. Ni kawaida yao."

"Wameomba [Yanga] tukutane ili kumaliza utata wa suala hili, vinginevyo Twite hatakuja siyo kujiunga na Yanga au Simba, bali haji kabisa."
Aliongeza: "Tulianza mazungumzo na Bahanuzi (Said)wakatuzunguka na kumsainisha, ikawa hivyo tena kwa Kavumbagu (Didier) na sasa wametuma viongozi Kenya kutaka kumsainisha Pascal Ochien ambaye yupo na timu Arusha."

Pascla Ochieng - mchezaji mpya wa Simba ambaye Hans Pope Yanga wameshaanza kumuwinda.

"Nafikiri Yanga kama wanataka kulipa kisasi cha mabao matano tuliyowafunga, wacheze mpira na siyo kutuzunguka na kusajili wachezaji wetu."
"Hata sisi tunaweza mchezo huo mchafu---ni kweli tunaweza kuwafanyia, lakini hatuoni sababu ya kufanya hivyo," alisema zaidi Pope.


Source: Mwananchi.co.tz

7 comments:

  1. Acha usimba wako Shaffih kama umekopi mwananchi kwanini hujakopi story yote umeweka tuu inayohusu simba?sasa ngoja nikusaidie kumalizia ulipoachia.

    HIKI KIPANDE KIPO KNY HILO GAZETI LA MWANANCHI AMBALO KWA UNAZI WAKO UNAPOTOSHA UMMA KWA KUWEKA STORY NUSU

    Alipoulizwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, aliyefanikisha usajili wa Twite, Abdallah Bin Kleb, alikana kuwapo na makubaliano ya kukutana na Simba kuzungumza suala la mchezaji huyo.
    Bin Kleb aliibeza kauli ya Pope na kusema inalenga kuwaziba mdomo mashabiki wa Simba ili wasahau kuzungumza suala la usajili wa Twite.

    "Hakuna makubaliano ya sisi [Yanga] kukutana na Simba ili kuzungumza suala la Twite. Kwanza kwa nini tufanye hivyo wakati mchezaji tumemsajili kwa kufuata taratibu," alihoji Bin Kleb.
    "Kama Simba wana matatizo na mchezaji ni wao, sisi hatuna matatizo na Twite wala mzazi wake, sasa iweje leo ashindwe kuja kujiunga na timu aliyopenda kuichezea?," alisema.

    Alisema, Twite anatarajia kuja nchini wiki ijayo akitoka Kongo alikokwenda kuwasalimia wazazi wake ambao hakuonana nao muda mrefu.

    Wakati huohuo, mshambuliaji mpya wa Simba George Ochan kutoka Kenya tayari ameshajiunga na wenzake, Arusha, huku Sihaune Abdulaziz kutoka Ghana akitarajia kutua leo

    ReplyDelete
  2. Hana lolote huyo,kama wanaweza why Rage alilia,waache siasa zao haya mambo yanatokea sana,mfano ni wao walipo msajili redondo,moura na man u mbona man u hawajawatisha PSG?hilo la ochieng halipo kabisa kwa sababu beki ya kati inawachezaji wa 3 hadi mbogo katolewa kwa mkopo,hans pole

    ReplyDelete
  3. Kuhusu Bahanuzi napingana na Hans Pope, habari za uhakika ni kwamba Juma Kaseja alimpeleka Bahanuzi Simba, akapendekeza kwa viongozi asajiliwe lakini viongozi wakamkataa kwa madai uwezo wake mdogo. Yanga wakamnasa mwisho wa siku kila mtu ameona. Tatizo la Simba na Yanga ni kwamba usajili wao unafanywa KIENYEJI sana, Kocha angekuwa anahusishwa kusingetokea timu ikasajili mchezaji leo kesho anaachwa

    ReplyDelete
  4. Acha unazi kwa nini hukumalizia story???

    Alipoulizwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, aliyefanikisha usajili wa Twite, Abdallah Bin Kleb, alikana kuwapo na makubaliano ya kukutana na Simba kuzungumza suala la mchezaji huyo.
    Bin Kleb aliibeza kauli ya Pope na kusema inalenga kuwaziba mdomo mashabiki wa Simba ili wasahau kuzungumza suala la usajili wa Twite.

    "Hakuna makubaliano ya sisi [Yanga] kukutana na Simba ili kuzungumza suala la Twite. Kwanza kwa nini tufanye hivyo wakati mchezaji tumemsajili kwa kufuata taratibu," alihoji Bin Kleb.
    "Kama Simba wana matatizo na mchezaji ni wao, sisi hatuna matatizo na Twite wala mzazi wake, sasa iweje leo ashindwe kuja kujiunga na timu aliyopenda kuichezea?," alisema.

    Alisema, Twite anatarajia kuja nchini wiki ijayo akitoka Kongo alikokwenda kuwasalimia wazazi wake ambao hakuonana nao muda mrefu.

    ReplyDelete
  5. Shaffih,mbona gazeti la mwananchi lilimhoji bin kleb,hili lako mwananchi gani la upande mmoja?acha unazi hadi unakata habari

    ReplyDelete
  6. Hatuna shida na Pascal Ochieng hata kwa mkopo

    ReplyDelete
  7. MIMI NAWASHANGAA SANA HAWA WASHABIKI WA YANGA, WANAVYOSHANGILIA USAJILI UTADHANI WAMESHINDA UWANJANI. HII NI SAWA NA KUCHEKELEA MIMBA BADALA YA KUSUBIRIA MTOTO.

    WAMESAHAU MWAKA 2009 WALIJIGAMBA SANA NA AKINA JAMA MBA, WALITUMIA MILIONI 500 LKN KUJA KWENYE UWANJA ZERO.

    NINA UHAKIKA KUWA HAYO YANAWEZA KUJIRUDIA. TUSUBIRI TUONE KAMA WANAWEZA KUDHIHIRISHA KWAMBA WANA THAMANI YA PESA WALIZOLIPWA

    ReplyDelete