Search This Blog

Thursday, June 28, 2012

ILALA YAENDELEA KUGAWA POINTI COPA


Ilala imeendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Copa Coca-Cola baada ya leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu) kuchapwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi Kigoma katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.

Mabao yote katika mechi hiyo ya kundi A yalifungwa kipindi cha kwanza huku Ramadhan Salum akipiga hat trick (mabao matatu). Alifunga mabao hayo dakika ya 13, 43 na 45. Bao la pili kwa washindi lilifungwa dakika ya 19 na Athuman Rashid.

Wakati Kigoma imeshinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza mpaka sasa katika kundi hilo, Ilala imepoteza mechi zote tatu ilizocheza. Ilala imefungwa na Arusha, Kigoma na Lindi wakati mechi yake inayofuata itakuwa Juni 30 mwaka huu dhidi ya Kusini Pemba.

Nayo Kilimanjaro imeendelea kufanya vizuri katika kundi lake la D baada ya leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu) kuitandika Shinyanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Mabao ya Kilimanjaro ambayo hadi sasa imeshinda mechi mbili na kutoka sare moja yalifungwa na Adam Soba dakika ya 11 na 46 wakati la tatu lilifungwa dakika ya 81 na James Henry.

Katika mechi nyingine zilizochezwa leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu), Temeke na Mtwara zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Ali Makalani alianza kuifungia Temeke na baadaye Adam swaleh akaisawazishia Mtwara.

Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani ulishuhudia Morogoro na Kaskazini Pemba zikitoka sare ya bao 1-0. Amin Kassim aliifungia Kaskazini Pemba dakika ya 51, na Morogoro wakasawazisha dakika ya 75 kupitia kwa Mutalemwa Katunzi katika mechi hiyo ya kundi B.
Mechi zitakazochezwa leo jioni (Juni 28 mwaka huu) ni Lindi vs Arusha (Tanganyika Packers), Manyara vs Mjini Magharibi (Nyumbu), Kinondoni vs Mbeya (Tamco) na Kusini Unguja vs Pwani (Karume).

Kesho (Juni 29 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea tena Juni 30 mwaka huu kwenye viwanja vyote vinne.

VODACOM KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI JUNI 30
Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu.

Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Powered by Sorecson : Creation de site internet

BAADA YA HAZARD, NASRI, SNEIJDER NA BENZEMA SASA NI MODRIC - MANCHESTER UNITED WAFELI TENA KWENYE SOKO LA USAJILI

Kama mwanaume ambaye hapendi kukubali kuwa wa pili kwa ubora, Sir Alex Ferguson lazima atakuwa akiudhiwa sana na namna jinsi amekuwa akiwakosa wachezaji anaotaka kuwasajili hasa kwenye miaka ya karibuni kabla ya kugeukia kwa wachezaji wa plan B.

Mchezaji mpya kuongezeka kwenye listi ya ambao Fergie amewataka lakini akawakosa ni Luka Modric, ambaye Sir Alex  amekuwa akimuwania kwa miaka sasa na alitaka kumsaini ndani ya klabu yake ya Manchester United kwa misimu miwili iliyopita.

Katika mara mbili zote, kikwazo kikubwa kimekuwa ni bei ambayo Tottenhma Hotspur wamekuwa wakiitaka £40million kwa Croatia huyo na United kugoma kulipa au kushindwa kumudu bei ambayo inapingana na sera zao za usajili.

Modric angekuwa mtu sahihi kwenye kikosi cha United. Mrithi halisia wa Paul Scholes ambaye anaweza kuimudu nafasi ya kiungo wakati, mchezaji huyo wa zamani wa Dinamo Zagreb sasa kuna uwezekanao mkubwa akajiunga na Real Madrid, huku kuondoka kwake White Hart Lane kukionekana hakuzuiliki.

Hali hii imekuwa ya kawaida kwa United tangu kuwasili kwa kwa wamiliki wapya wa klabu hiyo mwaka 2005. Wakati mabingwa hao wa mara 19 wa soka la England wakiwa na historia kubwa na ubora wa kikosi chao, mikataba ya mamilioni ikiendelea kumiminika na umaarufu ukizidi kukua miongoni mwa mashabiki wa soka duniani.

Ferguson alitumaini jambo hili lingebadilika msimu huu, lakini kuchelewa kwa mipango ya wamiliki wa klabu kuingia kwenye soko la hisa la Singapore kumewafanya United kukosa fedha nyingi za kupambana kwenye soko la usajili.

Ferguson amekuwa akiongea juu ya kukosekana kwa thamani ya ukweli kwenye soko la usajili, lakini mashabiki wa United wanakumbuka wakati Mscotland huyo alivyokuwa akifurahia kuvunja rekodi za usajili wakati alipokuwa akiwanunua akina Jaap Stam, Juan Sebastian Veron na Rio Ferdinand.

Dimitar Berbatov, alisajilia kutoka Spurs kwa ada ya £30.75million mwaka 2008, labda ndio pekee ambaye tunaweza kumtoa kwenye listi kwa kuwemo ndani ya kipindi cha utawala wa Glazers lakini United hawakuwa na upinzani mkubwa kwa ajili saini yake na mahitaji yake binafsi ya mshahara yalifikia sera ya usajili na bajeti ya Manchester United.

Hilo hilo haliwezi kusemwa kwa Eden Hazard, mbelgiji ambaye alikata United na majirani zao City na kusajili Chelsea mwezi uliopita.

United walihisi wapo kwenye nafasi nzuri ya kumsaini Hazard kutoka Lille, lakini hawakuwa radhi kumlipa mchezaji zaidi ya £130,000 kwa wiki achilia mbali fedha ya wakala wake £6million.

Chelsea wakawazidi United kwa kutoa ofa ya £200,000 kwa wiki na kukubali kulipa fedha za wakala, wakawalazimisha United kumgeukia mchezaji aliyekuwa kwenye plan B na wakamsajili Shinji Kagawa kutoka Borussia Dortmund.

Kiangazi kilichopita, United walishindwa tena na mahasimu wao Manchester City katika mbio za kumsaini Samir Nasri kutoka Arsenal kwa kushindwa kutoa ofa ya mkataba wa £170,000 kwa wiki. Wesley Sneijder, target mwingine wa usajili, alikataa kukubali kushusha mahitaji yake ya kupata mshahara wa £200,000 na akabaki Inter Milan.

Mara nyingine zimekuwa sababu za kisoka kwa United kuwakosa wachezaji wanaowataka. Ferguson alikuwa akimuimbisha Karim Benzema kwa takribani miaka miwili lakini mshambuliaji huyo wa kifaransa alikuwa ameweka nia ya kuichezea Real Madrid, wakati David Villa alikuwa hayupo radhi kuondoka Spain na akasaini kuichezea Barelona akitokea Valencia mwaka 2010.

Lakini wachezaji hawa wa hadhi ya juu - miongoni mwa walio bora duniani kwenye nafasi zao ndio ambao United wanahitaji kama ikiwa wanataka kuurudisha ubingwa wa England kwenye kabati la makombe pale Old Trafford na kuweza kutoa ushindani kwenye michuano ya Ulaya.

Ni vipi Ferguson anaweza kuongelea bei kubwa za wachezaji wakati yeye ni mmoja ya watu waliochangia hilo hasa ukizingatia alimuuza Cristiano Ronaldo kwa bei £80million cash kwenda Real Madrid 2009? Hi ni bei ambayo kwa wakati ule angeweza kuinunua klabu nzima ya Newcastle.

Fergie anajua vizuri thamani ya wachezaji wa kisasa kwenye soko la usajili - na anajua kwamba hana fedha za kuwasajili kulingana na bajeti anayopangia na mabosi wake.

United wana deni linalokaribia £500million pamoja na riba yanaizuia klabu hiyo kwenye kushindana kwa fedha na klabu kama City, Chelsea na mabwana wawili wa ligi ya Spain.

Manchester United hawahitaji sugar daddy kama ilivyo kwa Chelsea na City - mapato yao ni hatari, ni fedha nyingi sana - lakini deni kubwa walilonalo wamiliki linaikabaka klabu hiyo shingoni. Na ukweli bila kupata uwekezaji mkubwa kuna hatari City watawapa taabu sana na hata kuwashinda kama klabu inayoongoza England kwenye miaka kadhaa ijayo mbeleni.

TAMASHA LA FIESTA 2012 LAZINDULIWA DAR

Meneja Mipango na Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta 2012, Sebastian Maganga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Kushoto Meneja kampeni wa kampuni ya Push Mobile Media, Rugambo Roeney, Meneja wa Bia ya Serengeti, Allan Chonjo na Mkuu wa Masoko Gapco, Ben Temu.  
Barbara Hassan 
 Wadau
 Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Mwasiti Almasi akihojiwa na mtangazaji wa Clouds Tv,  Millard Ayo
 Baadhi ya zawadi 
 Meneja Mipango na Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta 2012, Sebastian Maganga
 Meneja kampeni wa kampuni ya Push Mobile Media, Rugambo Roeney  akimkabidhi mtangazaji wa Radio Clouds, Barbara Hassan namba 15555 zitakazotumika wakati wa kutuma ujumbe mfupi kwa ajili ya kushindania magari na pikipiki, wakati wa uzinduzi wa tamasha la fiesta 2012 uliofanyika katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam
 Millard Ayo akifanya mahojiano na wadau waliofika katika viwanja vya Leaders kushuhudia uzinduzi wa  tamasha la fiesta 2012
 Barbara Hassan

 Wadau
 Meneja wa Bia ya serengeti, allan Chonjo (kati)
                                                                                        Millard Ayo 

OFFICIAL: JORDI AITOSA MAN UNITED - KUJIUNGA NA BARCELONA WIKI IJAYO


 
Barcelona wametangaza kwenye mtandao wao rasmi kwamba wamekubalina na Valencia juu ya ada ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Spain Jordi Alba.

Barca ambao wamekuwa wakihusishwa na beki huyo wa kushoto kwa muda mrefu sasa, wamepiga hatua kubwa kuelekea kukamilisha dili hilo lenye thamani ya ‹€14 million.

Alba atakwenda Barcelona kufanya vipimo wiki ijayo, na kusaini dili la mkataba wa miaka 5 mara tu atakapofaulu vipimo vya afya.

"Barcelona wametangaza kwamba makubaliano rasmi yamefikiwa juu ya ada ya uhamisho wa Jordi Alba, kilichobaki ni vipimo vya afya ambavyo mchezaji huyo atafanyiwa wiki ijayo jijini Barcelona." Uliandika mtandao huo wa Barca.

"Gharama za uhamisho huu ni €14million na mchezaji atasaini mkataba wa miaka 5."

Alba mwenye miaka 25 ni zao la chuo cha soka cha Barcelona La Masia, lakini alifeli kufanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza pale Nou Camp na akaondoka mwaka 2005.

Jordi Alba alipokuwa La Masia

Sasa atarudi nyumbani alipolelelewa baada ya kucheza kwenye vilabu vya Cornella, Gimnastic na Valencia.

Habari hii ya Jordi Alba kwa vyoyote itakuwa sio nzuri kwa Manchester United ambao wamekuwa wakihusishwa kumtaka mhispania huyo ili aje ambadili Patrice Evra ambaye umri unamtupa mkono.

FABREGAS AIPELEKA SPAIN FAINALI - RONALDO NA URENO WAFUNGASHA VIRAGO


Portugal v Spain 2-4 Full Match Highlights Euro... by kofiswag

KALI YA LEO: ANGALIA WIMBO WA MCHEZAJI MPYA WA ARSENAL PODOLSKI

MUSSA MUDDE KUWASILI SIMBA KESHO - DANNY MRWANDA KUANZA MAZOEZI

Siku mbili baada ya kocha wa Milovan Cirkovic kutimba nchini, klabu ya Simba kesho inatarajia kumkaribisha mchezaji wao mpya kutoka nchini Kenya Mussa Mudde.

Musa Mudde ambaye amesaini Simba kwa mkataba wa miaka miwili, ni raia wa Uganda ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiichezea klabu ya Sofapaka ya Kenya.

Mude alisaini Simba takribani mwezi mmoja uliopita na sasa anakuja kwenye klabu hiyo ya mtaa wa msimbazi kuungana na mganda mwenzie anayecheza nae timu ya Taifa ya Uganda Cranes, Emmanuel Okwi.

Wakati huo huo mshambuliaji wa kimataifa aliyekuwa akicheza Vetnam ambaye msimu huu amejiunga na Simba anatarajia kuanza mazoezi kesho na klabu yake hiyo mpya. 


Wednesday, June 27, 2012

KOCHA WA UHOLANZI VAN MARWIJK AJIUZULU

Bert van Marwijk amejiuzulu kuwa kocha wa Uholanzi kufuatiwa timu ya wadachi kutofanya vizuri kwenye michuano ya Euro 2012.

Van Marwijk na vijana wake walienda Poland na Ukraine wakiwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kufuatia kuwa na mafanikio kwenye World Cup 2010 nchini South Africa.

Lakini walishindwa kufikia mategemeo yaliyokuwepo baada ya kufungwa kwenye mechi zote 3 za Group B dhidi ya Denmark, Ujerumani na Portugal.

Kocha huyo wa zamani wa Feyenoord na Borussia Dortmund aliichukua Uholanzi kutoka kwa Marco van Basten baada ya Euro 2008.

Alisaini mkataba wa muda mrefu na chama cha soka cha Uholanzi (KNVB) mwezi wa 12 mwaka jana ambao ungeisha mwaka 2016.

Lakini kufuatia kufanya vibaya kwenye Euro, huku ripoti zikisema kwamba hakuwa kwenye mahusiano mazuri na wachezaji wakubwa kwenye timu kumepelekea Van Marwijk awe historia.

EXCLUSIVE: SELEMAN MATOLA KOCHA MPYA AFRICAN LYON

Hatimaye leo mchana mchezaji wa zamani na nahodha wa klabu ya Simba Selemani Matola amejiunga rasmi na klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam kama bosi wa benchi la ufundi.

Matola ambaye pia alikuwa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba amejiunga na klabu hiyo ambayo kwenye msimu uliopita ilinusurika kushuka daraja.

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba anaenda African Lyon kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha aliyetimuliwa Jumanne Chale ambaye aliiongoza timu hiyo msimu uliopita.

DODOMA YAITAMBIA MBEYA COPA COCA-COLA 2012

Dodoma imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Juni 27 mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha mkoani Pwani.

Mabao ya Dodoma katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupachika bao la pili.

Nayo Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.

Mechi za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati ya Arusha na Kusini Pemba kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora kwenye Uwanja wa Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na kutokuwepo mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro Road) kutoka mkoani Pwani kuingia Dar es Salaam.

Leo jioni kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Ruvuma (Tanganyika Packers), Mwanza na Tanga (Nyumbu), Kaskazini Unguja na Mara (Tamco) na Singida na Kagera (Karume).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

POLISI MORO YAACHA 17, TZ PRISONS 11

Klabu tano za Ligi Kuu ya Tanzania zimewasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) majina ya wachezaji ambao zimewakatishia mikataba/mikataba yao kumalizika au kuwaacha kwa ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa 2012/2013.

Kwa mujibu wa klabu hizo, Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11. Azam imekatisha mikataba ya wachezaji watatu.

Wachezaji 12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar wakati wakati kwa upande wa Simba wachezaji waliomaliza mikataba ni wanne huku ikionesha nia ya kuwatoa kwa mkopo wengine wanne.

Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.

Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

Wachezaji walioachwa Polisi Morogoro ni Abdul Ibadi, Ally Moshi, Benedict Kitangita, Hassan Kodo, Hussein Lutaweangu, Hussein Sheikh, Juma Maboga, Mafwimbo Lutty, Makungu Slim, Mbaraka Masenga, Method Andrew, Moses Mtitu, Ramadhan Kilumbanga, Ramadhan Toyoyo, Said Kawambwa, Salum Juma na Thobias John.

Tanzania Prisons imewaacha Adam Mtumwa, Dickson Oswald, Exavery Mapunda, Ismail Selemani, Lwitiko Joseph, Mbega Daffa, Mwamba Mkumbwa, Musa Kidodo, Rajab Ally, Richard Mwakalinga na Sweetbert Ajiro.

Wachezaji waliomaliza mikataba yao kwa mujibu wa Kagera Sugar ni Cassian Ponera, Hamis Msafiri, Hussein Swedi, Ibrahim Mamba, Martin Muganyizi, Mike Katende, Moses Musome, Msafiri Davo, Said Ahmed, Said Dilunga, Steven Mazanda na Yona Ndabila.

Azam imewasitishia mikataba wachezaji Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino Augustino. Wachezaji waliomaliza mikataba Simba kwa mujibu wa klabu hiyo ni Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago, Juma Jabu wakati Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu.

Wachezaji ambao Simba inakusudia kuwatoa kwa mkopo ni Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina. 

JERRY SANTO KUTUA COASTAL UNION MUDA WOWOTE!

Tegemea hot news kuhusu Jerry Santo na Coastal Union very soon. tehe tehe tehe.....kaeni mkao wa kula jamani....habari kamili itatoka hivi karibuni...

Photo: Tegemea hot news kuhusu Jerry Santo na Coastal Union very soon. tehe tehe tehe.....kaeni mkao wa kula jamani....habari kamili itatoka hivi karibuni...

LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA MITANO TANGU AMINA CHIFUPA ATANGULIE MBELE YA HAKI


Marehemu Amina Chifupa

Amina Chifupa alipenda michezo hali iliyompelekea mara kwa mara kutoa misaada mbalimbali ya vifaa vya michezo. Hapa ilikuwa katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke, akikabidhi vifaa hivyo kwa Mh. Nchimbi wakati huo akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
Amina Chifupa akiteta jambo na Mwanasiasa Mkongwe nchini, Alnoor Kassum katika moja ya shughuli za kitaifa enzi za uhai wake. Hapa ilikuwa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Foundation jijini Dar.
Siku Amina Chifupa alipokula kiapo bungeni mjini Dodoma.
Amina (wa pili kushoto), akiwa na wabunge wenzake siku walipotembelea katika Nyumba ya Vipaji ya THT, wakati ikiwa pale Kinondoni katikati ya Biafra na Moroco.
Amina alikuwa mpenzi wa muziki pia hapa ilikuwa wakati huo ikiitwa Sheraton Hotel kwa sasa ni Serena, Bendi ya Twanga walikuwa wakitumbuiza katika hafla moja.
Amina alipiga vita matumizi ya dawa za kulevya na hapa alikuwa mgeni rasmi katika semina iliyotolewa kwa wanafunzi kuhusu madhara ya dawa hizo.
Amina Chifupa alipenda sana watoto hali iliyomfanya kujikita katika utoaji wa misaada katika vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima na waliokatika mazingira magumu. Hapa ilikuwa baada ya kutoa msaada katika kituo kimoja kilichopo Sinza.
Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Amina aliweza kuandaa futari na kukaribisha watu mbalimbali. Hapa ilkuwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar, akijadiliana jambo na Bi. Shyrose Bhanji ambaye sasa ni Mbunge wa Afrika Mashariki.

PHOTO CREDITS:http://bongostaz.blogspot.com/

CAPELLO: ROONEY ANACHEZA VIZURI AKIWA MANCHESTER UNITED TU - ANAELEWA LUGHA YA FERGIE TU

Fabio Capello jana usiku amemtupia vijembe Wayne Rooney na kumlaumu mshambuliaji huyo wa Manchester United kwa England kutolewa mapema kwenye Euro 2012.

Kocha huyo wa zamani wa Three Lions alikasirishwa na maoni ya Rooney kwamba ufundishaji wake kwa wachezaji ulikuwa una shida kuwafikia wachezaji kwa sababu ya lugha kwa kuwa muitaliano huyo hakuwa muongeaji mzuri wa kiingereza.

Lakini baada ya Roy Hodgson kukiri kwamba kwamba kiwango cha Rooney kwenye robo fainali dhidi ya Italia  kilichangia kwa kiasi kikubwa England kutolewa mapema na sasa Capello nae kapata kwa kusemea.

"Baada ya kuangalia mchezo wa England dhidi ya Italia nafikiri Rooney anaelewa ki-scotland  pekee," alisema Capello.

"Hilo ni kwa sababu anacheza vizuri akiwa na Manchester United tu, mahala anapofundishwa na Sir Alex Ferguson ambaye anaongea kiscottish."

Tuesday, June 26, 2012

ALIYEWATUKANA ASHLEY YOUNG NA COLE KWENYE TWITTER AKAMATWA

Haya ndio matusi ya kibaguzi ambayo bwana Steve raia wa Uingereza aliwatukana wachezaji wawili wa England ambao weusi Ashley Young wa Manchester United na Ashley Cole anayeichezea Chelsea.

Mtu huyo tayari ameshakamatwa na polisi nchini Uingereza na muda wowote atapelekwa mahakamami.

EXCLUSIVE: ALI AFIF -EPISODE 2

MFUMO MZIMA WA SOKA LA ENGLAND NI MBOVU: YASIPOFANYIKA MABADILIKO MACHUNGU YA JUMAPILI YATAKUWA YA MILELE

England walitegemewa na kwa mara nyingine tena wamefeli kupata matokeo.
Inahuzunisha, na kama mshabiki wa dhati kabisa wa timu hii ya taifa, inaniumiza sana kusema kwamba tumepata tulichostahili.
Ndio, kwenye Euro 2012 tulithibitisha kwamba tunayo moja safu bora kabisa za ulinzi kwenye soka, na kipindi hiki hakuna anayeweza kuzungumza umoja uliopo kwenye kikosi chetu.
Lakini kiukweli kabisa unadhani tunaweza kushinda makombe kwa kutegemea kuwa safu bora tu ya ulinzi?
Na nafikiri ligi yetu ya premier league iwe ya kwanza kuangalia tunapoanza kutafuta sababu za kushindwa kwetu, ligi ambayo tumekuwa tukijisifu kwamba ndio bora na kubwa duniani, ambayo inapendwa zaidi duniani.
Nafahamu tumesaini mkataba mpya matangazo ya TV wenye thamani £3billion, lakini inabidi kujiuliza kwanini ligi yetu inakuwa bora?
Wakati hakuna wa kuweza kupinga ubora na burudani inayopatikana kwenye mechi za kila wiki, inabidi tujue ukweli kwanini tumefanikiwa kwa hilo.
Ukweli ni kwa sababu ya kuwa namba kubwa ya wachezaji wa kigeni ambao ni mastaa wakubwa wanaong'ara kuliko wa kwetu.
Iondoe Manchester United wakati unaangalia timu kubwa, kwa sababu United wenyewe wameweza kuwa na wachezaji wengi wazawa - tuwasifie kwa hilo, lakini ukiachana na wao, Chelsea, Manchester City, Arsenal na Tottenham wamejaza wachezaji wengi wa kigeni wakubwa kutoka nje ya nchi.
Sisemi kwamba inabidi tuwaondoe wachezaji wa kigeni kwenye ligi yetu, hapana, lakini tuangalie ni namna gani uwepo wao ni wapi unaiacha England.
Ikiwa tungeweza kupita dhidi ya Italy - lakini hilo nalo lingekuwa aibu kwenye soka ukiangalia namna tulivyocheza - je tungekuwa kwenye hali gani pale ambapo tungekutana na vijana wanaotisha wa kijerumani Alhamisi hii kwenye nusu fainali?
Mungu kaepushia mbali tungekuwa tunakutana nao na kupata aibu nyingine kubwa, kwa sababu, kiukweli, tupo maili millioni moja nyuma yao, Kama ilivyo kwa Spain na Brazil.
Kila mmoja wetu alikuwa akiongelea namna tunavyoweza kuzuia vizuri kwenye michuano hii ya Euro na hilo ni kweli. Lakini ni jinsi gani tulikuwa ovyo linakuja suala la kushambulia?
Ndio tulikuwa tunamsubiria Wayne Rooney arudi, inahuzunisha, haikutokea vile ambavyo tulitegemea kwamba angetoa suluhisho kwenye ushambuliaji. Hilo sio kwa sababu Rooney ni mbovu la hasha hiyo inaonyesha ni kiasi gani namna safu yetu nzima ya ushambuliaji ilivyokosa makali.
Hakuna ubunifu, hatuna uwezo wa kumiliki mpira, hata kupigiana pasi, na hatukuwa na uwezo wa kubadilisha mchezo wetu kutokana na mazingira.
Angalia namna Spain walivyobadilisha mfumo wao na angalia walipo sasa
Wanamiliki mpira jinsi wanavyotaka mpka kuna wengine inawakera kuwaangalia.
Tazama namna tulivyocheza dhidi ya Italia, Jumapili, utaona tofauti kubwa iliyopo na timu nyingine kubwa.
Italia walikuwa na Andrea Pirlo, Azzuri walikuwa na mwanaume aliyefanya kila kitu, tofauti yetu kubwa na wao hatukuweza kuwa na mtu aliyeweza kufanya kazi aliyokuwa akifanya Pirlo kwa Italia.
Siwezi kutoa lawama kwa yoyote lakini ukweli ndio huo - na labda sasa hivi tuache maneno na kuondoa upofu tulionao juu ya ukweli kuhusu uwezo wetu kisoka.
Ofcourse ilikuwa jambo zuri kuona vijana wadogo kama akina Alex Oxlade Chamberlain kwenye level ya kimataifa na pia Danny Welbeck alipata nafasi.
Lakini wapo akina Pirlo, Mesuti Ozil au Andres Iniesta wa kiingereza? Wachezaji ambao kwao kila mapambano yanapozidi ndivyo na viwango vyao vinapozidi.
Wote hawa ni wachezaji wakubwa tena aina yake ambao kwenye michuano hii wameonyesha ukubwa wao.
Kuna wale ambao wamekuwa wakisema kwamba tunapaswa kufurahia kwa kuweza kufikia hatua ya robo fainali lakini mara tu tulipokutana na Italy, tulihadhirika.
Hatukuweza kuwamudu na kupeleka presha  kwenye lango lao, na hilo linakuja kutokana na kukosekana kwa wachezaji wa michuano mikubwa.
Na hilo linanileta kwenye suala linalipigiwa kelele kwamba Jack Wilshare ndio mchezaji ambaye ataleta utofauti kwenye timu na kutufanya tutishe.
Ndio, nakubali kwamba ana kipaji kikubwa, lakini kijana yule amekuwa nje ya dimba kwa msimu mzima, hivyo tumuache aweke umakini katika kurejesha kiwango chake akiwa na Arsenal  - bila kuwepo na presha ya mategemeo makubwa kwenye mabega yake machanga.
Kitu ambacho Boss Roy Hodgson anahitaji kufanya ni kuleta watu aina ya akina Alan Shearer, Gary Lineker, Chris Waddle, John Barnes na wengine ambao walifanya makubwa wakiwa kwenye timu ya taifa na kutumia uzoefu na maarifa yao.
Awaache watu wa aina hiyo kusaidia kufundisha na kukuza vipaji vya vijana wadogo kwa sababu sasa hivi, kijana yoyote mwenye kipaji anaandamwa na kupewa uoga wa mategemeo huku muda mwingine wakishindwa kuelewa namna ya kushughulika na mategemeo hayo.
Wakati Premier League itakapoanza tena, tutaanza tena  kujisifu kuhusu burudani inayopatikana kwenye ligi yetu.
Lakini inabidi tujue kwamba mpaka wakati watu wakubwa wanaongoza soka letu wafanye maamuzi magumu kuhusu ni wapi ligi yetu inaiacha timu ya Taifa, basi maumivu tuliyoyapata usiku wa jumapili yataendelea kuwa ya kawaida.
Klabu vs nchi? Kuna mshindi mmoja kwenye vita hiyo sasa  hivi.
Na kama yasipofanyika mabadiliko kwenye mfumo wa soka letu, kikubwa tunachoweza kupata kutoka kwenye kombe la dunia 2014 nchini Brazil ni marudio ya Euro 2012. Tena hapo kwa mafanikio ya juu kabisa.
Makala ya Ian Wright

MSIKILIZE KELVINI YONDANI MARA BAADA YA KUJIUNGA NA YANGA!

TOP 10 YA MADEMU WA WACHEZAJI KWENYE EURO 2012 AMBAO WAMEKUWA VIVUTIO

Netherlands - Yolanthe Sneijder (Wesley Sneijder)

Don't feel too sorry for Wes after a hard day at the office, at least he's got something to look forward to!


Spain - Sara Carbonero (Iker Casillas)

No footballer likes a microphone shoved in their face at full time, but when it's Sara's, it's fair game

Ireland - Claudine Keane (Robbie Keane)

A woman with a rhyming name and blonde locks? Claudine is made for the LA lifestyle

Czech Republic - Radka Kocurova (Tomas Rosicky)

No, this isn't Tomas without the goatee - it's his delightful wife Radka

Germany - Aida Yespica (Mesut Ozil)

Ozil will look to follow in Aida's footsteps on Sunday and hold a cup of his own!

Spain - Lara Alvarez (Sergio Ramos)

Ramos will hope to avoid another Copa del Rey moment by keeping a tight grip on the lovely Lara

Germany - Sarah Brandner (Bastian Schweinsteiger)

Sarah Brandner completes the world's longest Mexican wave, spanning from Gdansk to the Costa del Sol

Italy - Alena Seredova (Gianluigi Buffon)

Nobody was more frustrated than Gigi when Italy-England went to penalties, delaying his bed time even further

Portugal - Irina Shayk (Cristiano Ronaldo)
Because sometimes two big guys up top does work...

Spain - Shakira (Gerard Pique)

Sorry, Sepp, but those hips probably are lying to you