Search This Blog

Tuesday, June 26, 2012

MFUMO MZIMA WA SOKA LA ENGLAND NI MBOVU: YASIPOFANYIKA MABADILIKO MACHUNGU YA JUMAPILI YATAKUWA YA MILELE

England walitegemewa na kwa mara nyingine tena wamefeli kupata matokeo.
Inahuzunisha, na kama mshabiki wa dhati kabisa wa timu hii ya taifa, inaniumiza sana kusema kwamba tumepata tulichostahili.
Ndio, kwenye Euro 2012 tulithibitisha kwamba tunayo moja safu bora kabisa za ulinzi kwenye soka, na kipindi hiki hakuna anayeweza kuzungumza umoja uliopo kwenye kikosi chetu.
Lakini kiukweli kabisa unadhani tunaweza kushinda makombe kwa kutegemea kuwa safu bora tu ya ulinzi?
Na nafikiri ligi yetu ya premier league iwe ya kwanza kuangalia tunapoanza kutafuta sababu za kushindwa kwetu, ligi ambayo tumekuwa tukijisifu kwamba ndio bora na kubwa duniani, ambayo inapendwa zaidi duniani.
Nafahamu tumesaini mkataba mpya matangazo ya TV wenye thamani £3billion, lakini inabidi kujiuliza kwanini ligi yetu inakuwa bora?
Wakati hakuna wa kuweza kupinga ubora na burudani inayopatikana kwenye mechi za kila wiki, inabidi tujue ukweli kwanini tumefanikiwa kwa hilo.
Ukweli ni kwa sababu ya kuwa namba kubwa ya wachezaji wa kigeni ambao ni mastaa wakubwa wanaong'ara kuliko wa kwetu.
Iondoe Manchester United wakati unaangalia timu kubwa, kwa sababu United wenyewe wameweza kuwa na wachezaji wengi wazawa - tuwasifie kwa hilo, lakini ukiachana na wao, Chelsea, Manchester City, Arsenal na Tottenham wamejaza wachezaji wengi wa kigeni wakubwa kutoka nje ya nchi.
Sisemi kwamba inabidi tuwaondoe wachezaji wa kigeni kwenye ligi yetu, hapana, lakini tuangalie ni namna gani uwepo wao ni wapi unaiacha England.
Ikiwa tungeweza kupita dhidi ya Italy - lakini hilo nalo lingekuwa aibu kwenye soka ukiangalia namna tulivyocheza - je tungekuwa kwenye hali gani pale ambapo tungekutana na vijana wanaotisha wa kijerumani Alhamisi hii kwenye nusu fainali?
Mungu kaepushia mbali tungekuwa tunakutana nao na kupata aibu nyingine kubwa, kwa sababu, kiukweli, tupo maili millioni moja nyuma yao, Kama ilivyo kwa Spain na Brazil.
Kila mmoja wetu alikuwa akiongelea namna tunavyoweza kuzuia vizuri kwenye michuano hii ya Euro na hilo ni kweli. Lakini ni jinsi gani tulikuwa ovyo linakuja suala la kushambulia?
Ndio tulikuwa tunamsubiria Wayne Rooney arudi, inahuzunisha, haikutokea vile ambavyo tulitegemea kwamba angetoa suluhisho kwenye ushambuliaji. Hilo sio kwa sababu Rooney ni mbovu la hasha hiyo inaonyesha ni kiasi gani namna safu yetu nzima ya ushambuliaji ilivyokosa makali.
Hakuna ubunifu, hatuna uwezo wa kumiliki mpira, hata kupigiana pasi, na hatukuwa na uwezo wa kubadilisha mchezo wetu kutokana na mazingira.
Angalia namna Spain walivyobadilisha mfumo wao na angalia walipo sasa
Wanamiliki mpira jinsi wanavyotaka mpka kuna wengine inawakera kuwaangalia.
Tazama namna tulivyocheza dhidi ya Italia, Jumapili, utaona tofauti kubwa iliyopo na timu nyingine kubwa.
Italia walikuwa na Andrea Pirlo, Azzuri walikuwa na mwanaume aliyefanya kila kitu, tofauti yetu kubwa na wao hatukuweza kuwa na mtu aliyeweza kufanya kazi aliyokuwa akifanya Pirlo kwa Italia.
Siwezi kutoa lawama kwa yoyote lakini ukweli ndio huo - na labda sasa hivi tuache maneno na kuondoa upofu tulionao juu ya ukweli kuhusu uwezo wetu kisoka.
Ofcourse ilikuwa jambo zuri kuona vijana wadogo kama akina Alex Oxlade Chamberlain kwenye level ya kimataifa na pia Danny Welbeck alipata nafasi.
Lakini wapo akina Pirlo, Mesuti Ozil au Andres Iniesta wa kiingereza? Wachezaji ambao kwao kila mapambano yanapozidi ndivyo na viwango vyao vinapozidi.
Wote hawa ni wachezaji wakubwa tena aina yake ambao kwenye michuano hii wameonyesha ukubwa wao.
Kuna wale ambao wamekuwa wakisema kwamba tunapaswa kufurahia kwa kuweza kufikia hatua ya robo fainali lakini mara tu tulipokutana na Italy, tulihadhirika.
Hatukuweza kuwamudu na kupeleka presha  kwenye lango lao, na hilo linakuja kutokana na kukosekana kwa wachezaji wa michuano mikubwa.
Na hilo linanileta kwenye suala linalipigiwa kelele kwamba Jack Wilshare ndio mchezaji ambaye ataleta utofauti kwenye timu na kutufanya tutishe.
Ndio, nakubali kwamba ana kipaji kikubwa, lakini kijana yule amekuwa nje ya dimba kwa msimu mzima, hivyo tumuache aweke umakini katika kurejesha kiwango chake akiwa na Arsenal  - bila kuwepo na presha ya mategemeo makubwa kwenye mabega yake machanga.
Kitu ambacho Boss Roy Hodgson anahitaji kufanya ni kuleta watu aina ya akina Alan Shearer, Gary Lineker, Chris Waddle, John Barnes na wengine ambao walifanya makubwa wakiwa kwenye timu ya taifa na kutumia uzoefu na maarifa yao.
Awaache watu wa aina hiyo kusaidia kufundisha na kukuza vipaji vya vijana wadogo kwa sababu sasa hivi, kijana yoyote mwenye kipaji anaandamwa na kupewa uoga wa mategemeo huku muda mwingine wakishindwa kuelewa namna ya kushughulika na mategemeo hayo.
Wakati Premier League itakapoanza tena, tutaanza tena  kujisifu kuhusu burudani inayopatikana kwenye ligi yetu.
Lakini inabidi tujue kwamba mpaka wakati watu wakubwa wanaongoza soka letu wafanye maamuzi magumu kuhusu ni wapi ligi yetu inaiacha timu ya Taifa, basi maumivu tuliyoyapata usiku wa jumapili yataendelea kuwa ya kawaida.
Klabu vs nchi? Kuna mshindi mmoja kwenye vita hiyo sasa  hivi.
Na kama yasipofanyika mabadiliko kwenye mfumo wa soka letu, kikubwa tunachoweza kupata kutoka kwenye kombe la dunia 2014 nchini Brazil ni marudio ya Euro 2012. Tena hapo kwa mafanikio ya juu kabisa.
Makala ya Ian Wright

No comments:

Post a Comment