Search This Blog

Monday, December 16, 2013

16 BORA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL VS BAYERN - CHELSEA KUKUTANA NA AKINA DROGBA, MAN U WAPELEKWA UGIRIKI

Manchester City v Barcelona
Olympiakos v Manchester United
Galatasaray v Chelsea
Arsenal v Bayern Munich
AC Milan v Atletico Madrid
Schalke v Real Madrid
Bayer Leverkusen v PSG
Zenit St. Petersburg v Borussia Dortmund


BREAKING NEWS: MANCHESTER CITY YAPANGWA DHIDI YA BARCELONA 16 BORA CHAMPIONS LEAGUE


BREAKING NEWS: ANDRE VILLAS BOAS AFUKUZWA KAZI TOTTENHAM

Siku moja baada ya kupokea kipigo cha kihistoria cha 5-0 kutoka kwa Liverpool wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, klabu ya Tottenham Hotspur imemtimua kocha mkuu wa timu hiyo Andre Villas Boas.

Tottenham ambao walikuwa ndio timu iliyotumia fedha nyingi kufanya usajili wakati wa dirisha la usajili, wakitumia zaidi ya paundi millioni 100, wameanza vibaya msimu huu na hivyo kufikia maamuzi ya kumtimua AVB ambaye alijiunga na timu hiyo miezi takribani 18 iliyopita.

Majina ya Luis Enrique na Fabio Capello yameanza kutajwa kuja White Hart Lane kuchukua nafasi inayoachwa wazi na kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Porto.

USAJILI WA OKWI KWENDA YANGA,NI MUDA MUAFAKA WA RAGE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI KUTUAMBIA ZILIPO PESA ZA USAJILI WA SAMATTA,OCHAN NA OKWI.



HAPPY BIRTHDAY KIPRE TCHETCHE,KIPRE BALOU NA BRIAN UMONY.






DAUDA TV: MFAHAMU MRISHO NGASSA

OKWI NA BERKO KIELELEZO CHA USAJILI MBOVU SIMBA NA YANGA


Na baraka mbolembole

Mwishoni mwa mwaka 2003, aliyekuwa mlinzi wa kushoto wa klabu ya soka ya Simba, Mrundi, Ramadhani Wasso Ramadhani, aliiomba klabu yake aliyokuwa ameichezea kwa miaka miwili mfululizo kutomuongezea mkataba mwingine kwa madai ya kupata timu ya kuichezea soka la kulipwa nchini, Ubelgiji. Bila hiana, Simba ilikubalia na madai hayo ya Wasso, huku wakimtakia kila la heri katika safari yake.

Nini ambacho kilikuja kutokea?. Ni Wasso kujiunga na Yanga , na
hakukuwa na safari yoyote ya kucheza soka Ubelgiji. Ulikuwa usajili wa kukomoana zaidi wakati huo. Kwani hakuna upande ambao ulifaidika na dili hilo, kwa Wasso hakuwa yule tena aliyeng'ara katika ulinzi wa kushoto katika timu ya Simba/

Kwa, wapenzi wa kandanda wa Tanzania bila shaka wanakumbuka habari ya Wasso. Majuzi, Yanga wamemsaini kiungo-mshambuliaji, Mganda, Emmanuel Okwi ambaye alikuwa akiitumikia timu iliyomlea, SC Villa kwa mkopo
akitokea, Etoile du Sahel ya Tunisia. Awali, Okwi aliitumikia Simba kwa misimu mitatu na nusu tangu, julai, 2009 hadi, Januari, 2013 alipouzwa kwa Etoille du Sahel.

Wakati, Mganda huyo akiitumikia Simba alikuwa na mchango mkubwa sana uwanjani, japo wakati mwingine alikuwa mtovu wa nidhamu, alikuwa msumbufu kwa uongozi, mwenye kuchelewa kambini hata wakati timu ikiwa katika maandalizi ya michezo muhimu. Ni, mchezaji mzuri sana na kiwango alichokionesha akiwa na timu ya taifa ya Uganda katika michuano ya Challenge ni moja ya sababu za kusajiliwa kwake Yanga.

' KULWA na DOTTO'
Usajili wa Simba, ulikuwa ni wa lazima kutokana na hali halisi ambayo timu imekuwa ikionesha uwanjani, ila nani ambaye ameamua kuwarundika makipa hawa, Ivo, Dhaira, na Berko?. Kwa, michezo 13 ya mzunguko wa pili wa ligi kuu, Ivo angetosha, na wakati Dhaira akiwa amepoteza kiwango chake, klabu isingekuwa na wasiwasi wa mchezaji gani ambaye anatakiwa kupunguzwa ili kuendena na kanuni mpya ya wachezaji watatu wa kigeni kuanzia msimu ujao. 

Pesa, ambayo klabu imetumia kuwasaini, Berko na Donald ingeweza kufanya mambo mengine au pengine kusajili wachezaji wazawa. Sheria mpya ya usajili kwa wageni inatakiwa kuungwa mkono na kutekelezwa kikwelikweli ili kupunguza wachezaji wanaosajiliwa bila kuwa na sababu za msingi, tena wakiwa wakigeni.

YANGA WANASAJILI KAMA TP MAZEMBE
Juma Kaseja, Said Dilunga, na sasa Okwi, wachezaji hawa watatu
wamesajiliwa wakati wa dirisha dogo, ni sehemu ya kuhimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya vilabu barani Afrika, 2014 , ambayo Yanga wataiwakilisha Tanzania katika klabu bingwa.

Ikiwa tayari na wachezaji wa kutosha, Mrisho Ngassa, Saimon Msuva, Jerry Tegete, Said Bahanunzi, Hussein Javu, Shaaban Kondo, Didier Kavumbagu, na Hamis Kizza, Yanga, timu yenye kushambulia kwa mtindo wa moja kwa moja, itakuwa na nguvu zaidi na kasi katika mashambulizi, kwa kuwa Okwi ni mchezaji ambaye anaweza kuisaidia na kuifanya Yanga kuwa na kasi zaidi. 

Sina shaka kuhusu ubora wa Okwi, ila ni mchezaji asiye na mahusiano mazuri na wachezaji wenzake.


NGOME YAO
Nahodha, Nadir yupo katija maji marefu kwa kuwa kiwango kimekuwa si cha kuridhisha, kuna wakati anakuwa akicheza vizuri na wakati mwingine akicheza akiwa na wasiwasi mkubwa, mabao waliyofunga KMKM, yalikuwa mazuri na yenye kiwango cha juu, ila ni walinzi wenyewe wa Yanga walioandaa mazingira ya kuadhibiwa. 
Hawajipangi vizuri na inapotokea wanashambuliwa walinzi wa kati wanakuwa dhaifu kimaamuzi, kujipanga, kukaba, na si wazuri kwa mipira ya ' tackling', ni Kelvin Yondan pekee anaweza kuwa juu na kucheza akiwa timilifu, ila makosa ya kujipanga hovyo kwa patna wake yamekuwa yakimfanya kuwa na hali ya kupaniki. 

Twite, kiasili ni mlinzi mahiri wa kati, wakati anaporudi katika nafasi hiyo, ila si wakati akicheza na Nadir. Waliruhusu mabao mawili ya kizembe dhidi ya KMKM, wikiendi iliyopita wakiwa na Juma Abdul, David Luhende, Mbuyu na Nadir.

Ni namna gani, Yanga wanaweza kujiendesha uwanjani, itegemea na kocha Ernie Brandts atakavyoamua kuwacheza mastaa wake. Timu kubwa zinahitaji,' wachezaji wakubwa', mtazamo mkubwa, mafanikio ya kutosheleza. Ila, hawa wafanyabiashara katika soka la Tanzania, wana sifa ya kuwa wafanyabiashara wa kimataifa?.

Nakumbuka, wakati Tom wakati alipoamua kuwapanga, Chuji, Twite, na Kelvin katika safu ya kati ya ulinzi katika mchezo wake wa pili tu wa ligi kuu msimu uliopita, akapigwa 3-0 na Mtibwa Sugar, akaambiwa uwezo wake ni mdogo, akaondoshwa.

 Ila wakati wa utetezi wake alimwambia, mwenyekiti wa klabu yake,' wewe ni mfanyabiara, na nina uhakika si
mfanyabiashara wa kimataifa, niache nifanye kazi yangu'

Nafikiri, Brandts alihitaji kufanya usajili wa kushinikiza wa mlinzi wa kati kama Said Mourad, na pengine kiungo-mlinzi mwenye uwezo wa kuanzisha move nzuri kutoka kwa walinzi hadi kwa safu ya kiungo wa mashambulizi, katika soko hakuna kiungo wa nafasi hii ambaye anaweza kufit katika mtindo wa uchezaji wa Yanga, mahali hapo ni kwa Chuji, kwa kuwa wengine wengi wameshindwa jukumu hilo, uwezo wa kukaba, unyang'anya mipira, kuchezesha timu wa Chuji umekuwa msaada mkubwa kwa Yanga. 

Bado naipa nafasi ya kwanza kushinda pambano lijalo la ' Nani Mtani Jembe', katika uchambuzi wa kufikirika, ila katika uhalisia, naitazama Simba kutawala mchezo na kushinda. Kwa, nini nasema hivyo, Simba kwa sasa ina kikosi kizuri, wanahitaji utulivu tu.


DONALD MOSOTI OMEUWA NA MIAKA 32  

Usajili wa mlinda mlango, Ivo Mapunda katika klabu ya soka ya Simba, umekuja siku chache baada ya kuwasili klabuni hapo kwa kipa, Mghana, Yaw Berko. 

Usajili huo ni kama kuwasukuma nje ya lango makipa wa awali, Mganda, Abel Dhaira, na wasaidi wake, Andrew Ntara na chipukizi Abou Hashim.

Ivo, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba, na Berko yeye kwa upande amesaidi mkataba wa muda mfupi wa miezi sita. Usajili wa Ivo ni mzuri na unaweza kuwa na faida nyingi kwa Simba, kwa wakati huu ambao soka la Tanzania likionekana kuwa na uhaba wa makipa wa viwango vya juu. 

Bahati nzuri ni mapendekezo ya kocha mpya wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic ambaye aliwahi kufanya nae kazi katika timu ya Gor Mahia ya Kenya.

AZAM FC YAENDELEA NA MAZOEZI KUJIANDAA NA KOMBE LA MAPINDUZI.




Picha kwa hisani ya AZAM FC.

JAMAL MALINZI AKABIDHIWA RIPOTI NA KAMATI YA KANAL KIPINGU.






Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, TFF jana lilipokea ripoti maalum kutoka kwenye jopo la baadhi ya wataalam waliokutana hivi karibuni visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutafuta mustakabali wa Tanzania kufuzu michuano ya AFCON 2015 itakayofanyika nchini Morocco.
Ripoti hiyo imewasilishwa kwa Rais wa TFF Jamali Malinzi na mwenyekiti wa jopo hilo Kanali Mstaafu Iddi Kipingu baada ya jopo hilo kukamilisha jukumu walilopewa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo mwenyekiti wa jopo hilo Kanali Mstaafu Kipingu amesema kwamba kazi hiyo wameifanya kwa uzalendo na uadilifu mkubwa.  

MJADALA: NINI MAONI YAKO JUU YA SINEMA YA OKWI KUTOKA SIMBA- ETOILE DU SAHEL-SC VILLA NA SASA YANGA.


Emmanuel Okwi akiweka alama ya Dole Gumba mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Mashindao Musa Katabaro (kushoto) wakati akisaini mkataba wa kuichezea Yanga mpaka mwishoni mwa msimu wa 2015/2016. kulia ni mwanasheria/meneja wa Okwi Bw. Edgar Agaba

Sunday, December 15, 2013

DAUDA TV: HUYU NDIYE EMMANUEL OKWI

LIVERPOOL YAITANDIKA TOTENHAM MABAO 5-0,YABAKISHA POINTI MBILI KUKWEA KILELENI.








USHINDI WA SIMBA WA MABAO 3-1 DHIDI YA KMKM KATIKA PICHA.


 Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akiwapungia mkono mashabiki wa timu hiyo.
Ali Bushir akisalimiana na kocha wa Simba, Zdravko Logarusic
 Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha KMKM
 Uhuru Seleman akimtoka beki wa KMKM ya Zanzibar, Faki Ali Hamad katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. 
 Uniwezi kijana.
 Uhuru Seleman akiambaa na mpira huku Faki Ali Hamad akitambaa.
 Uhuru Seleman akijiandaa kupiga krosi..
 Heka heka katika lango la KMKM.
 Said Ndema akitafuta mbinu za kuwato wachezaji wa KMKM.
 Mashabiki wa Simba.
 Uhuru Selemani akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa KMKM.
Kocha wa KMKM, Ali Bushir akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.

BREAKING NEWS! YANGA YAMSAJILI EMMANUEL OKWI,SC VILLA YALIPWA $ 20,000 KAMA ADA YA UHAMISHO


 
 
Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi kutoka klabu ya SC Villa.

Habari za uhakika ambazo mtandao huu imezipata ni kwamba Yanga wamelipa kiasi cha dola za Kimarekani 20,000 kama ada ya uhamisho na kumsainisha Okwi mkataba wa miaka miwili.

Okwi anatarajia kuwasili nchini hivi karibu akitokea Uganda, ameiomba Yanga abaki nchini Uganda kumalizia kufanya tangazo la kampuni moja ya simu nchini humo.

Hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC ) imepatikana leo saa tisa mchana .

ZOEZI LA KUPANDA NYASI UWANJA WA SOKOINE MBEYA KUANZA KESHO.


Uongozi wa chama cha soka mkoa wa Mbeya umewatoa wasiwasi mashabiki wa soka mkoani humo kwamba wataendelea kushuhudia michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara ya mzunguko wa pili inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
Akithibitisha taarifa hiyo katibu mkuu wa chama cha soka Mbeya Seleman Haroub amesema kwamba ukarabati wa uwanja unaendelea vizuri na kesho wanatarajiwa kuanza zoezi la kupanda nyasi katika sehemu ya kuchezea

MABAVARIA BAYERN MUNICH WAANZA MAANDALIZI YA CHRISTMASS



DAUDA TV: ANGALIA BAO LA MAAJABU LA ALESSANDRO DEL PIERO NA PENATI YA MAAJABU YA HARRY KEWELL

MANCHESTER UTD YAIFUNGA ASTON VILLA MABAO 3:0,FLETCHER AREJEA,CLEVERLY AFUNGA BAO BAADA YA MWAKA


Manchester UTD imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3:0 ugenini dhidi ya Aston Villa kwenye mchezo wa ligi kuu ya England.
Mabao ya Man UTD kwenye mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji Danny Welbeck aliyefunga mawili,bao lingine limefungwa na kiungo Tom Cleverly ikiwa ni baada ya mwaka mmoja kamili tangia alipoifungia timu yake bao la mwisho.
Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni winga raia wa Ecuador Antonio Valencia aliyetengeneza mabao mawili ya Welbeck,kwenye mchezo huo pia tumemshuhudia kiungo Darren Fletcher akicheza dakika 30 za mwisho baada ya kukosekana tangu tarehe 23 mwezi disemba mwaka jana.

OZIL AWAOMBA RADHI MASHABIKI WA ARSENAL.KUTOKANA KITENDO CHAKE CHA JANA.



VIDEO: ARSENAL YAFUNZWA ADABU NA MAN CITY - YAPIGW 6-3, CHELSEA WASHINDA


All Goals - Manchester City 6-3 Arsenal - 14-12... by video4all


Chelsea 2-1 Crystal Palace
Everton 4-1 Fulham
Newcastle United 1-1 Southampton
Cardiff City 1-0 West Brom
West Ham United 0-0 Sunderland