Search This Blog

Monday, December 16, 2013

OKWI NA BERKO KIELELEZO CHA USAJILI MBOVU SIMBA NA YANGA


Na baraka mbolembole

Mwishoni mwa mwaka 2003, aliyekuwa mlinzi wa kushoto wa klabu ya soka ya Simba, Mrundi, Ramadhani Wasso Ramadhani, aliiomba klabu yake aliyokuwa ameichezea kwa miaka miwili mfululizo kutomuongezea mkataba mwingine kwa madai ya kupata timu ya kuichezea soka la kulipwa nchini, Ubelgiji. Bila hiana, Simba ilikubalia na madai hayo ya Wasso, huku wakimtakia kila la heri katika safari yake.

Nini ambacho kilikuja kutokea?. Ni Wasso kujiunga na Yanga , na
hakukuwa na safari yoyote ya kucheza soka Ubelgiji. Ulikuwa usajili wa kukomoana zaidi wakati huo. Kwani hakuna upande ambao ulifaidika na dili hilo, kwa Wasso hakuwa yule tena aliyeng'ara katika ulinzi wa kushoto katika timu ya Simba/

Kwa, wapenzi wa kandanda wa Tanzania bila shaka wanakumbuka habari ya Wasso. Majuzi, Yanga wamemsaini kiungo-mshambuliaji, Mganda, Emmanuel Okwi ambaye alikuwa akiitumikia timu iliyomlea, SC Villa kwa mkopo
akitokea, Etoile du Sahel ya Tunisia. Awali, Okwi aliitumikia Simba kwa misimu mitatu na nusu tangu, julai, 2009 hadi, Januari, 2013 alipouzwa kwa Etoille du Sahel.

Wakati, Mganda huyo akiitumikia Simba alikuwa na mchango mkubwa sana uwanjani, japo wakati mwingine alikuwa mtovu wa nidhamu, alikuwa msumbufu kwa uongozi, mwenye kuchelewa kambini hata wakati timu ikiwa katika maandalizi ya michezo muhimu. Ni, mchezaji mzuri sana na kiwango alichokionesha akiwa na timu ya taifa ya Uganda katika michuano ya Challenge ni moja ya sababu za kusajiliwa kwake Yanga.

' KULWA na DOTTO'
Usajili wa Simba, ulikuwa ni wa lazima kutokana na hali halisi ambayo timu imekuwa ikionesha uwanjani, ila nani ambaye ameamua kuwarundika makipa hawa, Ivo, Dhaira, na Berko?. Kwa, michezo 13 ya mzunguko wa pili wa ligi kuu, Ivo angetosha, na wakati Dhaira akiwa amepoteza kiwango chake, klabu isingekuwa na wasiwasi wa mchezaji gani ambaye anatakiwa kupunguzwa ili kuendena na kanuni mpya ya wachezaji watatu wa kigeni kuanzia msimu ujao. 

Pesa, ambayo klabu imetumia kuwasaini, Berko na Donald ingeweza kufanya mambo mengine au pengine kusajili wachezaji wazawa. Sheria mpya ya usajili kwa wageni inatakiwa kuungwa mkono na kutekelezwa kikwelikweli ili kupunguza wachezaji wanaosajiliwa bila kuwa na sababu za msingi, tena wakiwa wakigeni.

YANGA WANASAJILI KAMA TP MAZEMBE
Juma Kaseja, Said Dilunga, na sasa Okwi, wachezaji hawa watatu
wamesajiliwa wakati wa dirisha dogo, ni sehemu ya kuhimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya vilabu barani Afrika, 2014 , ambayo Yanga wataiwakilisha Tanzania katika klabu bingwa.

Ikiwa tayari na wachezaji wa kutosha, Mrisho Ngassa, Saimon Msuva, Jerry Tegete, Said Bahanunzi, Hussein Javu, Shaaban Kondo, Didier Kavumbagu, na Hamis Kizza, Yanga, timu yenye kushambulia kwa mtindo wa moja kwa moja, itakuwa na nguvu zaidi na kasi katika mashambulizi, kwa kuwa Okwi ni mchezaji ambaye anaweza kuisaidia na kuifanya Yanga kuwa na kasi zaidi. 

Sina shaka kuhusu ubora wa Okwi, ila ni mchezaji asiye na mahusiano mazuri na wachezaji wenzake.


NGOME YAO
Nahodha, Nadir yupo katija maji marefu kwa kuwa kiwango kimekuwa si cha kuridhisha, kuna wakati anakuwa akicheza vizuri na wakati mwingine akicheza akiwa na wasiwasi mkubwa, mabao waliyofunga KMKM, yalikuwa mazuri na yenye kiwango cha juu, ila ni walinzi wenyewe wa Yanga walioandaa mazingira ya kuadhibiwa. 
Hawajipangi vizuri na inapotokea wanashambuliwa walinzi wa kati wanakuwa dhaifu kimaamuzi, kujipanga, kukaba, na si wazuri kwa mipira ya ' tackling', ni Kelvin Yondan pekee anaweza kuwa juu na kucheza akiwa timilifu, ila makosa ya kujipanga hovyo kwa patna wake yamekuwa yakimfanya kuwa na hali ya kupaniki. 

Twite, kiasili ni mlinzi mahiri wa kati, wakati anaporudi katika nafasi hiyo, ila si wakati akicheza na Nadir. Waliruhusu mabao mawili ya kizembe dhidi ya KMKM, wikiendi iliyopita wakiwa na Juma Abdul, David Luhende, Mbuyu na Nadir.

Ni namna gani, Yanga wanaweza kujiendesha uwanjani, itegemea na kocha Ernie Brandts atakavyoamua kuwacheza mastaa wake. Timu kubwa zinahitaji,' wachezaji wakubwa', mtazamo mkubwa, mafanikio ya kutosheleza. Ila, hawa wafanyabiashara katika soka la Tanzania, wana sifa ya kuwa wafanyabiashara wa kimataifa?.

Nakumbuka, wakati Tom wakati alipoamua kuwapanga, Chuji, Twite, na Kelvin katika safu ya kati ya ulinzi katika mchezo wake wa pili tu wa ligi kuu msimu uliopita, akapigwa 3-0 na Mtibwa Sugar, akaambiwa uwezo wake ni mdogo, akaondoshwa.

 Ila wakati wa utetezi wake alimwambia, mwenyekiti wa klabu yake,' wewe ni mfanyabiara, na nina uhakika si
mfanyabiashara wa kimataifa, niache nifanye kazi yangu'

Nafikiri, Brandts alihitaji kufanya usajili wa kushinikiza wa mlinzi wa kati kama Said Mourad, na pengine kiungo-mlinzi mwenye uwezo wa kuanzisha move nzuri kutoka kwa walinzi hadi kwa safu ya kiungo wa mashambulizi, katika soko hakuna kiungo wa nafasi hii ambaye anaweza kufit katika mtindo wa uchezaji wa Yanga, mahali hapo ni kwa Chuji, kwa kuwa wengine wengi wameshindwa jukumu hilo, uwezo wa kukaba, unyang'anya mipira, kuchezesha timu wa Chuji umekuwa msaada mkubwa kwa Yanga. 

Bado naipa nafasi ya kwanza kushinda pambano lijalo la ' Nani Mtani Jembe', katika uchambuzi wa kufikirika, ila katika uhalisia, naitazama Simba kutawala mchezo na kushinda. Kwa, nini nasema hivyo, Simba kwa sasa ina kikosi kizuri, wanahitaji utulivu tu.


DONALD MOSOTI OMEUWA NA MIAKA 32  

Usajili wa mlinda mlango, Ivo Mapunda katika klabu ya soka ya Simba, umekuja siku chache baada ya kuwasili klabuni hapo kwa kipa, Mghana, Yaw Berko. 

Usajili huo ni kama kuwasukuma nje ya lango makipa wa awali, Mganda, Abel Dhaira, na wasaidi wake, Andrew Ntara na chipukizi Abou Hashim.

Ivo, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba, na Berko yeye kwa upande amesaidi mkataba wa muda mfupi wa miezi sita. Usajili wa Ivo ni mzuri na unaweza kuwa na faida nyingi kwa Simba, kwa wakati huu ambao soka la Tanzania likionekana kuwa na uhaba wa makipa wa viwango vya juu. 

Bahati nzuri ni mapendekezo ya kocha mpya wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic ambaye aliwahi kufanya nae kazi katika timu ya Gor Mahia ya Kenya.

13 comments:

  1. Nafikiri hauna uhakika na uyasemayo. Sababu kichwa cha habari hakiendani na ulichoandika. Na pia umepotosha.Unapenda kuandika lakini yawezekana umesha kuwa na fikra mgando tangu siku nyingi. Unaandika kwa mazoea na si ukweli na uhalisia. Hujaonyesha vipi yanga haimuhitaji OKWI badala yake unaonyesha kusajiliwa beki wa kati. Kichwa cha habari kilipaswa kisiwe hicho kwa maelezo uliyotoa. Pili kuhusu Okwi kutofanya vizuri au kufanya vizuri; ulipaswa kuwa na mitazamo miwili. Huwezi ukawa unategemea kufanya vibaya peke yake na kwa makusudi eti hutegemei kama atafanya vizuri. Chukua mfano wa ATHUMANI IDD (CHUJI). Aliwahi kuwa na kiwango bora kisha akachuja na akarudi tena kwenye kiwango bora hadi hivi sasa. Na kubwa zaidi anaendana vizuri na wenziwe katika timu.
    Nakushauri kuandika kwa ukweli na ukiwa HURU kiakili na kifikra badala ya kupenda kukosoa ovyo kila linalofanywa na SIMBA AU YANGA. na kwa muktadha huu hapa ni Yanga. Hata kama una chuki zako binafsi na viongozi au jina la timu unapaswa kukumbuka kuwa maneno hayo yatasomwa na watu wengi wenye uelewa tofauti na wengine wenye uelewa mkubwa kukuzidi wewe.
    BADILIKA!

    ReplyDelete
    Replies
    1. asante sana. mleta story anaonekana anashida fulani hivi. au hukufundishwa vizuri kuandika insha kidato cha pili

      Delete
  2. Kinacho onekana na si mara yako ya kwanza, uNAPENDA KUANDIKA RONGORONGO USIZO NA UHAKIKA NAZO,KWANZA MABAO WALIO FUNGA KMKM JUZI CANAVARO ALIKUWA AMESHA TOKA,YANGA HAIHITAJI MLINZI WA KATI ILA WANAHITAJI BEKI WA KULIA.

    ReplyDelete
  3. Hayo ya hapo juu yote ni sahihi

    ReplyDelete
  4. Tatizo lako huzingatii maadili ya kazi ya uandishi(ethics).Unaonekana kusukumwa zaidi na emotions as opposed to logical thiking. "Impartiality" ni ethical principal muhimu sana katika taaluma ya uandishi. Uliyoyaandika ni matokeo ya kutozingatia ethics na kusukumwa na ushabiki au mapenzi yako kwenye timu fulani. Hapana shaka kwamba umeumia sana baada ya kusikia Okwi kasajiliwa Yanga hadi ukashindwa ku-controll EMOTIONS zako na kujikuta ukiandika vitu vya hovyo hovyo ambavyo havina mashiko. Inamaana ulikua hujui kama wakati KMKM wanafunga yale magoli mawili akina Kanavaro na wenzake walikua wameshatolewa? Yanga ilifanya mabadiliko ya wachezaji zaidi ya wanne kwa mpigo na lengo ilikua kuwajaribu wachezaji ambao wamekua hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara, hivyo swala la kufungwa haikua issue. Kumbuka coacher anajua zaidi kuliko wewe na wala yanga haina hayo matatizo uliyoyadadavua. Makosa ni kitu cha kawaida na si kutokea mara moja ndo liwe gonjwa. Zingatia ethics za taaluma ya uandishi na kabla hujaandika hakikisha EMOTIONS zako ziko sawa kwani maamuzi yoyote yanayokua influenced na EMOTIONS huwa ni mabovu kama ulivyofanya hapo juu.

    ReplyDelete
  5. HUYO JAMAA SIJUI MWAJIRIWA KTK HII BROG YA SHAFFIH, KAWA MZEMBE HADI ANATIA SHAKA UELEWA ALIONAO

    ReplyDelete
  6. Jamaa huyu kavulugwa na bila shaka ni mshabiki wa simba kutokana na yanga kumpata okwi wachambuzi wengine ovyo sana

    ReplyDelete
  7. Mwandishi haeleweki analenga nini, kichwa cha habari tofauti na blah blah alizoandika....!

    ReplyDelete
  8. Halafu hana pointi ya msingi ni kama anaweweseka na kubwabwaja mambo mengi yan hajui anazungumzia nn.

    ReplyDelete
  9. Mwandishi wa hii makala ana shida kichwani..He is not a Journalist rather a football politician..kichwa cha habari na maada ndani ni vitu viwili tofauti..next time before postin your article try to read it again and give it to another writer or editor to re-read it..Otherwise bwana mkubwa utaishia kua Kanjanja...Jifunze sababu muda unao..nia ya kua mwandishi bora unayo na ni imaini yangu kua hata uwezo Unao pia..

    ReplyDelete
  10. shaffii dnt allow weak sports writers turnish ur blog..hebu chek headin na theme nzima duh,kweli huyo mzaramo..

    ReplyDelete
  11. okwi ni mchezaji wa kawaida sana sio okwi wa zamani, la msingi simba jipange vizuri mna kikosi bora. Msibabaikie wachezaji watovu wa nidhamu na wasumbuvu ila jitahidi kutumia wazawa zaidi.

    ReplyDelete