Search This Blog
Friday, August 24, 2012
MCHAKATO WA SERENGETI FIESTA 2012 WAENDELEA KUPAMBA MOTO NDANI YA JIJI LA TANGA
Mchakato wa Serengeti Fiesta 2012 ndani ya Tanga ukiendelea ndani ya mitaa kadhaa ya jiji hili. Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, hapa vijana wa kazi kutoka Clouds Fm wakiongea na wakazi wa eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 26.8.2012 katika uwanja wa Mkwakwani.
Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu, akiyaendeleza mastori ndani ya kitaa cha Taili tatu eneo la Magaoni, Kata ya Mabawa, Tanga.
Mwanadada Loveness Love akiwa na Gossip Cop Tz, Sudi Brown.
Vijana walijitahidi kuonyesha umahili wao wa kuchana michano.
Clouds Tv nayo haikukosa.
Mazungumzo ya mtaani yakiendelea.
Mtangazaji wa Clouds Fm Adamu Mchomvu na Mwanadada Loveness Love.
Hapa jamaa alikuwa akitiririka machache ndani ya Clouds Fm/Clouds TV.
Producer wa Home record ya Tanga nae akimwaga maneno yake juu ya tamasha fiesta.
Show Love ikiendelea.
Show love ndani ya eneo la Magaoni, Taili Tatu Kata ya Mabawa.
Aha! Mzee wa Habari na Matukio (Kajunason Blog) akiwa na Adamu Mchomvu wakiwakilisha na chama la watoto wa Tanga.
PAUL KAGAME ALIVYOWAKARIBISHA YANGA KWENYE IKULU YA RWANDA
| Raisi wa Rwanda Paul Kagame akisalimiana na Mama Fatma Karume aliyeomgozana na Yanga kwenda nchini Rwanda. |
| Kocha wa Yanga Saintfield akisamiliana na Kagame |
| Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji akisoma risala yake mbele ya Raisi Kagame |
| Wachezaji wa Yanga wakisikiliza kwa makini risala ya mwenyekiti wao |
| Nahodha wa Yanga na kocha wakimkabidhi kombel la Kagame - mdhamini mkuu wa kombe hilo Raisi wa Rwanda Paul Kagame. |
| Mama Karume na Seif Magari wakimkabidhi Kagame jezi ya Yanga |
| Paul Kagame akiongea na Wachezaji wa Yanga |
| Mchezaji Mbuyi Twite akiwa na wachezaji wenzie wa Yanga Ikulu ya Rwanda walipoalikwa na Raisi Paul Kagame. |
| PICHA ZOTE ZIMEPIGWA NA SALEHE ALLY WA CHAMPION |
JOSE MOURINHO: PORTO ILIPOIFUNGA MAN UNITED NILIPATA FUNZO KUBWA SANA KUTOKA KWA SIR ALEX FERGUSON
Mapema wiki iliyopita kabla ya msimu mpya wa soka barani ulaya ulaya haujaanza Mtangazaji wa BBC Radio 5 Dj Spoony alikaa chini ya kufanya mazungumzo mafupi na Jose Mourinho kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu career yake na mchezo wa soka kwa ujumla.
SPOONY: Kitu gani kinachokusukuma na kukufanya utake kufanya vizuri zaidi ?
MOURINHO: Klabu yenyewe kuwa juu ya kila kitu. Ninapoenda kwenye timu, na kuvaa shati ya nembo ya timu, nahisi ile shati kama ndio ya kwanza au ya mwisho kwangu. Huwa nahisi kwamba mashabiki wa klabu kama sehemu ya maisha yangu. Ninakuwa na uhusiano wa ndania na mashabiki.
Kwa haraka zaidi na mimi nakuwa mmoja wao huku nikiwa na nafasi ya juu ya kuipigania nembo ya klabu na kujaribu kuleta furaha kwetu sote kwa kushinda kila mechi.
SPOONY: Je kutokana na mtazamo wako huu wa kishabiki zaidi unaweza ukawa moja ya sababu zinazopelekea uwepo wa matatzio baina yako na wamiliki wa vilabu, kwa sababu hawana mtazamo kama walionao mashabiki?
MOURINHO: Rudi nyuma na uangalie historia yangu tangu naanza kufundisha siku ya kwanza mpaka sasa sijawahi kuwa na matatizo na wamiliki wa timu.
Pale Chelsea, sikutaka kuendelea kukaana kuacha vitu viende katika muelekeo ambao wote tulihisi haukuwa muelekeo mzuri.
Tulihisi ulikuwa ni uamuzi mzuri, na kwa sababu hiyo mpaka sasa tumebaki kuwa marafiki. Hakuna matatizo kati yangu na Roman.
SPOONY: Je utarudi Chelsea?
MOURINHO: Nitaenda mahali ambapo watu wananitaka. Lakini inabidi nirudie hili: Nipo na Real Madrid, bado nataka sana kuwa hapa, nina mkataba mpya, sifikirii kuhusu kuondoka.
SPOONY: Unamuheshimu na kumkubali sana Sir Alex Ferguson.
MOURINHO: Ndio ni kweli. Mara yangu ya kwanza kukutana nae sitokuja kusahau kwa sababu Porto iliifunga Manchester United kwenye champions league. Baada ya mechi alikuja na kutugongea kwenye malngo wetu wa vyumba vya kubadilishia nguo akiwa na Gary Neville, na walikuja pale kwa nia ya kutupongeza.
Hapo nilijifunza na kuelewa kwamba ushindi ni kitu cha kustahili, inabidi uwaheshimu washindi na inabidi ujifundishe kujua kufurahia mafanikio ya wenzako japo kidogo.
Ilitokea msimu uliopita tulipocheza na Bayern na wakatutoa kwenye nusu fainali ya champions league, na mwisho wa mechi nilifanya kile nilichofanyiwa na Fergie. Nilienda kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo na kuwapongeza. Nikakumbuka usiku ule nikiwa na Porto na ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yangu mazuri na kocha bora wa soka la Uingereza.
SPOONY: Watu siku zote wanasema Barcelona ndio klabu bora kabisa ambayo tumeishuhudia kwenye kizazi hiki, na bado Real Madrid wamechukua La Liga. Unajisikia fhari sana?
MOURINHO: Tulishinda ubingwa, tena kwa pengo la pointi tisa. hawakushinda ubingwa kwa sababu walikuwa na msimu mbaya, kwa sababu muda mwingine timu kubwa zinakuwa na wakati mbaya na zinapoteza pointi.
Walikuwa na pointi 91, na unapokuwa na pointi 91 unakuwa bingwa wa ligi yoyote. Lakini tatizo ni kwamba Real Madrid walikuwa na pointi 100. Tulivunja kila rekodi kwenye ligi nchini Hispania na kwa maana hiyo tulishinda kwa sababu tulikuwa bora, na pia tulikuwa na msimu mzuri.
SPOONY: Sir Bobby Robson ni hazina ya nchi ya Uingereza na wewe ulikuwa msaidiz wake wa karibu. Ulijifunza kiasi gani kutoka kwake?
MOURINHO: Nilipata bahati kwa sababu alinichukua wakati nikiwa mdogo sana. Nilikaa miaka mitano na Sir Bobby, na kwa kweli alikuwa muhimu sana kwangu. Ni mmoja ya watu walionifanya kuwa the "Special One".
SPOONY: Umesaini mkataba mpya na Real Madrid unaoisha 2016, lakini kuna tuhuma kwamba wewe unaangalia ushindi tu na hujali kuhusu vipaji vinavyochipukia kuweza kuisadia klabu mbeleni. So nini plan yako kuu kwa Real Madrid?
MOURINHO: Unajua, kwanza changamoto kubwa niliyokuja nayo haoa ni kushinda, na sio kuusimamisha utawala wa Barcelona katika soka la Spain, na mpaka sasa tumeshashinda vikombe na sio viaya kusema "kazi imefanyika vizuri". Wote tunataka kuendelea kushinda. Real Madrid ilikuwa ndio klabu bora kabisa katika karne iliyopita kwa sababu ya kupata matokeo na mie lengo lengu ni kutaka kuifanya Madrid klabu bora kwa kupata matokeo katika karne ya 21.
SPOONY: Na kabla hatumaliza, unadhani au unajiona siku moja ukifundisha timu ya taifa. Je utaifundisha timu ya kimataifa hata kama sio Ureno?
MOURINHO: Kwa wakati huu sioni uwezekano huo, kwa sababu ni kazi tofauti kabisa na ninayoifanya sasa. Kwenye klabu tunacheza mechi 60 kwa msimu, kimataifa timu inacheza labda mechi 10, hivyo hiyo sio kazi ninayotaka kuifanya wakati huu.
Lakini ni kazi ambayo inawapa watu fahari sana, tena hasa ikiwa unaifanya kwa ajili ya nchi yako, na kama kuja kuifanya nitaifanya na Ureno kwa sababu nafikiri watu wa Ureno hawatonielewa kama nitakifanya kazi hiyo kwa nchi nyingine.
Thursday, August 23, 2012
Amsha amsha ya Tamasha la Serengeti Fiesta 29012 yazidi kuwazindua wakazi wa mji wa moshi na vitongoji vyake
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Dr Msengia akiaga baada ya kuitembelea timu Serengeti Fiesta 2012 Mkoa wa Kilimanjaro jioni ya leo. Katikati ni Erick Kussaga ambae ni Mzalishaji wa timu ya Fiesta mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Mheshimiwa Dr Msengi akiwa na Afisa Uhusiano wa Clouds Entertainment Co. LTD kwa upande wa Viongozi wa Taasisi za Serikali na Vyama vya Siasa Ndugu Simalenga Simon wakati Mkuu huyo wa Wilaya alipoitembelea timu ya amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Mkoani Kilimanjaro jioni hii.Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linatarajia kuzinduliwa rasmi kesho katika uwanja wa chuo cha Ushiriki mkoani humo,ambapo msanii nyota kutoka nchini Kenya,CMB Prezoo ataliongoza jahazi la wasanii mbalimbali kutoka hapa nyumbani,katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 5000 kwa kila kichwa.
Mmoja wa washabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta damu akiwa na fulana yake ya tamasha hilo lililowahi kufanyika mjini moshi lililopachikwa jina la jipanguze kama uonavyo pichani.Wanaharakati anuai wa tamasha la serengeti fiesta 2012 leo wameamsha amsha wakazi wa mji huo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Himo,Stendi kuu ya mabasi pamoja na soko la Mbuyuni na kutoa zawadi ya mafuta ya gari/pikipiki na bajaji kutoka kampuni ya Gapco ambayo ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo,kwa watu kadhaa ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za awali ya tamasha lenyewe.
Subscribe to:
Posts (Atom)































