Search This Blog
Friday, August 24, 2012
JOSE MOURINHO: PORTO ILIPOIFUNGA MAN UNITED NILIPATA FUNZO KUBWA SANA KUTOKA KWA SIR ALEX FERGUSON
Mapema wiki iliyopita kabla ya msimu mpya wa soka barani ulaya ulaya haujaanza Mtangazaji wa BBC Radio 5 Dj Spoony alikaa chini ya kufanya mazungumzo mafupi na Jose Mourinho kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu career yake na mchezo wa soka kwa ujumla.
SPOONY: Kitu gani kinachokusukuma na kukufanya utake kufanya vizuri zaidi ?
MOURINHO: Klabu yenyewe kuwa juu ya kila kitu. Ninapoenda kwenye timu, na kuvaa shati ya nembo ya timu, nahisi ile shati kama ndio ya kwanza au ya mwisho kwangu. Huwa nahisi kwamba mashabiki wa klabu kama sehemu ya maisha yangu. Ninakuwa na uhusiano wa ndania na mashabiki.
Kwa haraka zaidi na mimi nakuwa mmoja wao huku nikiwa na nafasi ya juu ya kuipigania nembo ya klabu na kujaribu kuleta furaha kwetu sote kwa kushinda kila mechi.
SPOONY: Je kutokana na mtazamo wako huu wa kishabiki zaidi unaweza ukawa moja ya sababu zinazopelekea uwepo wa matatzio baina yako na wamiliki wa vilabu, kwa sababu hawana mtazamo kama walionao mashabiki?
MOURINHO: Rudi nyuma na uangalie historia yangu tangu naanza kufundisha siku ya kwanza mpaka sasa sijawahi kuwa na matatizo na wamiliki wa timu.
Pale Chelsea, sikutaka kuendelea kukaana kuacha vitu viende katika muelekeo ambao wote tulihisi haukuwa muelekeo mzuri.
Tulihisi ulikuwa ni uamuzi mzuri, na kwa sababu hiyo mpaka sasa tumebaki kuwa marafiki. Hakuna matatizo kati yangu na Roman.
SPOONY: Je utarudi Chelsea?
MOURINHO: Nitaenda mahali ambapo watu wananitaka. Lakini inabidi nirudie hili: Nipo na Real Madrid, bado nataka sana kuwa hapa, nina mkataba mpya, sifikirii kuhusu kuondoka.
SPOONY: Unamuheshimu na kumkubali sana Sir Alex Ferguson.
MOURINHO: Ndio ni kweli. Mara yangu ya kwanza kukutana nae sitokuja kusahau kwa sababu Porto iliifunga Manchester United kwenye champions league. Baada ya mechi alikuja na kutugongea kwenye malngo wetu wa vyumba vya kubadilishia nguo akiwa na Gary Neville, na walikuja pale kwa nia ya kutupongeza.
Hapo nilijifunza na kuelewa kwamba ushindi ni kitu cha kustahili, inabidi uwaheshimu washindi na inabidi ujifundishe kujua kufurahia mafanikio ya wenzako japo kidogo.
Ilitokea msimu uliopita tulipocheza na Bayern na wakatutoa kwenye nusu fainali ya champions league, na mwisho wa mechi nilifanya kile nilichofanyiwa na Fergie. Nilienda kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo na kuwapongeza. Nikakumbuka usiku ule nikiwa na Porto na ndio ukawa mwanzo wa mahusiano yangu mazuri na kocha bora wa soka la Uingereza.
SPOONY: Watu siku zote wanasema Barcelona ndio klabu bora kabisa ambayo tumeishuhudia kwenye kizazi hiki, na bado Real Madrid wamechukua La Liga. Unajisikia fhari sana?
MOURINHO: Tulishinda ubingwa, tena kwa pengo la pointi tisa. hawakushinda ubingwa kwa sababu walikuwa na msimu mbaya, kwa sababu muda mwingine timu kubwa zinakuwa na wakati mbaya na zinapoteza pointi.
Walikuwa na pointi 91, na unapokuwa na pointi 91 unakuwa bingwa wa ligi yoyote. Lakini tatizo ni kwamba Real Madrid walikuwa na pointi 100. Tulivunja kila rekodi kwenye ligi nchini Hispania na kwa maana hiyo tulishinda kwa sababu tulikuwa bora, na pia tulikuwa na msimu mzuri.
SPOONY: Sir Bobby Robson ni hazina ya nchi ya Uingereza na wewe ulikuwa msaidiz wake wa karibu. Ulijifunza kiasi gani kutoka kwake?
MOURINHO: Nilipata bahati kwa sababu alinichukua wakati nikiwa mdogo sana. Nilikaa miaka mitano na Sir Bobby, na kwa kweli alikuwa muhimu sana kwangu. Ni mmoja ya watu walionifanya kuwa the "Special One".
SPOONY: Umesaini mkataba mpya na Real Madrid unaoisha 2016, lakini kuna tuhuma kwamba wewe unaangalia ushindi tu na hujali kuhusu vipaji vinavyochipukia kuweza kuisadia klabu mbeleni. So nini plan yako kuu kwa Real Madrid?
MOURINHO: Unajua, kwanza changamoto kubwa niliyokuja nayo haoa ni kushinda, na sio kuusimamisha utawala wa Barcelona katika soka la Spain, na mpaka sasa tumeshashinda vikombe na sio viaya kusema "kazi imefanyika vizuri". Wote tunataka kuendelea kushinda. Real Madrid ilikuwa ndio klabu bora kabisa katika karne iliyopita kwa sababu ya kupata matokeo na mie lengo lengu ni kutaka kuifanya Madrid klabu bora kwa kupata matokeo katika karne ya 21.
SPOONY: Na kabla hatumaliza, unadhani au unajiona siku moja ukifundisha timu ya taifa. Je utaifundisha timu ya kimataifa hata kama sio Ureno?
MOURINHO: Kwa wakati huu sioni uwezekano huo, kwa sababu ni kazi tofauti kabisa na ninayoifanya sasa. Kwenye klabu tunacheza mechi 60 kwa msimu, kimataifa timu inacheza labda mechi 10, hivyo hiyo sio kazi ninayotaka kuifanya wakati huu.
Lakini ni kazi ambayo inawapa watu fahari sana, tena hasa ikiwa unaifanya kwa ajili ya nchi yako, na kama kuja kuifanya nitaifanya na Ureno kwa sababu nafikiri watu wa Ureno hawatonielewa kama nitakifanya kazi hiyo kwa nchi nyingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment