Search This Blog
Saturday, June 18, 2011
SIMBA WAKIWA KINSHASA
ON THIS DAY: WOZA 10
1) leo ni siku yake ya kuzaliwa ametimiza miaka 64- HAPPY BIRTHDAY CAPELLO
2) Mwaka jana siku kama ya leo alikua anasherehekea miaka 63 ya kuzaliwa kwake lakini pia alikua anakiongoza kikosi cha England kwenye mchezo dhidi ya Algeria kwenye WOZA 2010.
ENGLAND ilishindwa kuifunga ALGERIA na mchezo huo ukamalizika kwa timu hizo kushindwa kufungana.
MAADUI DIMBANI MARAFIKI BATANI
WAKATI WAINGEREZA WAKIENDELEA KULA BATA, DIDIER DROGBA AVUTA JIKO
Goli la Ulimwengu Ugenini dhidi ya Cameroon
GOOOO Goooo Tom Ulimwengu pamoja Mbwana Samatta.
Mbwana Samatta pia alifunga goli ugenini kwenye mchezo wake wa mwisho akiwa na kikosi cha timu kubwa ya Taifa dhidi ya Africa ya Kati, Stars pia ilifungwa 2-1
sasa unapata picha gani kwenye mchezo wa hapo baadae?
Timu ya U23 imewasili salama nchini Nigeria
Boniface Wambura, Lagos
Timu ya U23 imewasili salama hapa saa 6.30 mchana kwa ndege ya Kenya Airways
kabla ya kuunganisha ndege ya Concord Airlines kwenda Benin City ambapo mechi
dhidi ya Nigeria itachezwa kesho kuanzia saa 10 kamili saa za hapa ambapo
nyumbani Tanzania itakuwa saa 12 kamili jioni.
Awali U23 ilikuwa ifike hapa saa 4 kamili asubuhi, lakini ikachelewa kutoka
Nairobi ambapo ilitoka saa 3.30 badala ya saa 1.30 baada ya ndege ya Kenya
Airways kuchelewa kuondoka.
Kocha Jamhuri Kihwelo amesema vijana wake katika hali nzuri ya kupeperusha
bendera ya Tanzania katika mechi hiyo ambapo mshindi baada ya matokeo ya
nyumbani ambapo U23 ilipata ushindi wa bao moja ataingia katika hatua ya makundi
kutafuta tiketi ya kuiwakilisha Afrika katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika
mwakani jijini London, Uingereza.
Amesema timu yake itacheza mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza huku akijaza
viungo wengi kwa lengo la kumiliki mpira kwa muda mrefu, hivyo kuzuia
mashambulizi ya timu pinzani kwa staili.
Kihwelo amesema mbele atatumia washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata.
Wachezaji wengine aliokuja nao hapa ni Jamal Mnyate, Jackson Wandwi, Hussein
Javu, Mohamed Soud, Obadia Mungusa, Abuu Ubwa, Juma Abdul, Abdul Juma, Himid
Mao, Issa Rashid, Khamis Mcha, Salum Abubakar, Shomari Kapombe, Jabir Aziz,
Godfrey Wambura na Awadh Juma.
NATAKA KUONDOKA - MODRIC

Luka Modric amewashangaza mashabiki wa Tottenham baada ya kukiri anataka kuondoka White Hart Lane.
Modric mwenyewe amevunja kuhusu suala la usajili wake baada kusema nataka kuondoka Spurs.
Akiongea na gazeti la Daily Mail, alisema: "Nataka kuondoka Tottenham nikiwa na uhusiano mzuri na klabu, nilifurahia sana uwepo wangu pale lakini huu ni muda sahihi kwangu kuangalia klabu nyingine."
Nimekuwa na makubaliano na mwenyekiti.Nilipokuwa nasaini mkataba alianiambia, ikitokea klabu itakayonitaka wataifikiria ofa."Chelsea ni klabu kubwa na ina mmiliki mwenye ndoto za kufanikiwa.Wana wachezaji wazuri na wenye hamu ya mafanikio kwa kupigana kushinda EPL na Champions League.
"Nataka kubaki London.Nina furaha ndani jiji hili na pia familia yangu wanapapenda hapa."
TOP 20 YA WANAMICHEZO MATAJIRI WA KIMAREKANI MWAKA 2011

Pamoja na kuandamwa na skendo, nafasi yake ya kwanza kuchukuliwa lakini hakuna kinachomzuia mchezaji wa golf maarufu zaidi ulimwenguni Tiger Woods kuendelea kushikilia nafasi ya kwanza kama mwanamichezo wa kimarekani anayeingiza mkwanja mrefu kuliko wote.
1. Tiger Woods $62,294,116 - Golf
2. Phil Mickelson $61,185,933 - Golf
3. LeBron James $44,500,000 - Miami Heat (NBA)
4. Peyton Manning $38,070,000 - Indianapolis Colts (NFL)
5. Alex Rodriguez $36,000,000 - New York Yankees (MLB)
6. Kobe Bryant $34,806,250 - Los Angeles Lakers (NBA)
7. Kevin Garnett $32,832,044 - Boston Celtics (NBA)
8. Matt Ryan $32,700,000 - Atlanta Falcons (NFL)
9. Tom Brady $30,007,280 - New England Patriots (NFL)
10. Dwight Howard $28,647,180 - Orlando Magic (NBA)
11. Dwyane Wade $28,200,000 - Miami Heat (NBA)
12. Sam Bradford $27,250,000 - St. Louis Rams (NFL)
13. Dale Earnhardt Jr. $26,572,930 - Auto racing
14. Darrelle Revis $25,750,000 - New York Jets (NFL)
15. Jim Furyk $25,334,622 - Golf
17. CC Sabathia $23,800,000 - New York Yankees (MLB)
18. Joe Mauer $23,750,000 - Minnesota Twins (MLB)
19. Jeff Gordon $23,703,710 - Auto racing
20. Vernon Wells $23,250,000 - Los Angeles Angels (MLB)
Friday, June 17, 2011
ON THIS DAY: WOZA 2010
ILIKUA NI MECHI KATI YA NIGERIA NA KOREA REPUBLIC.
BOLTON: ARSENAL NA CITY LETENI OFA KWA AJILI YA CAHIL

OWEN COYLE ameziambia Arsenal na Manchester City kupeleka ofa kwa ajili ya Gary Cahil.
The Gunners na City kwa muda mrefu wamekuwa wakipigana vikumbo ili kuweza kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye anacheza katika nafasi ya beki wa kati ndani ya Bolton.
Wanderers kwa muda mrefu wamekuwa wagumu kumuachia beki huyo wa timu ya taifa ya England lakini sasa manager Owen Coyle amewaalika Arsenal Wenger na Roberto Mancini kupeleka ofa rasmi.
Coyle amesema:
"Naamini anaweza kucheza katika klabu yoyote.Kumekuwa na timu nyingi zilizoonyesha kumtaka zikiwemo timu kubwa ndani ya ligi kuu ya England.
"Inawezakana ili kumpata Cahil inabidi timu ilipe fedha nyingi, hivyo klabu zinazo mtaka zipeleke ofa kwa mwenyekiti.Gary sio mchezaji ambaye ningependa kumpoteza, suala lake linaniumiza kichwa lakini hatuna budi kukubali kumuachia kama zitakuja ofa nzuri zitazohusisha pesa nyingi ambazo tutatumia kujenga upya klabu yetu.
Kiukweli ningependa sana abaki hapa.Ni mchezaji mzuri kwa timu hii na sisemi nataka aondoke, lakini kama akiondoka basi naamini itakuwa ni biashara nzuri kwa klabu."
OFFICIAL: CHELSEA KWENYE MAZUNGUMZO YA KUMSAINI LUKAKU

Anderlecht wamethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba wapo kwenye mazungumzo na Chelsea ya kufanya uhamisho wa mshambuliaji Romelu Lukaku kuelekea Stamford Bridge.
Lukaku, 18, amekuwa akihusishwa kujiunga na Chelsea timu ambayo amewahi kukiri kuwa na mapenzi nayo.
Tetesi zilikuwa zinasema kuwa Anderlecht general manager Herman van Holsbeeck alienda London kukutana na kumalizana na Chelsea, na sasa tetesi hizo sasa zimekuwa kweli baada ya timu hiyo ya Ubelgiji kuthibitisha kufanya mazungumzo na Roman Abramovich's team.
Van Holsbeeck aliiambia Sky Sports: "Bado kuna muda kidogo katika kufanya majadiliano.Tupo kwenye mazungumzo na Chelsea lakini pia kuna timu nyingine tumeongea nazo.
OFFICIAL: DEMBA BA AJIUNGA NA NEWCASTLE

DEMBA BA amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Newcastle kwa mkataba wa miaka 3.
The Senegal international ambaye amekuwa kwa miezi sita ndani ya klabu ya West Ham anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Newcastle ndani kipindi hiki cha usajili baada ya Yohan Cabaye.
Ba akiwa na Wagonga Nyundo wa London alifanikiwa kufunga mabao 7 ndani ya mechi 12 baada ya kujiunga na West Ham kutoka Hoffenheim katika kipindi cha usajili mwezi January.
Newcastle boss Alan Pardew amesema: "Demba alifanya mambo makubwa sana akiwa na West Ham msimu uliopita hivyo ni moja kati ya usajili mzuri kwa klabu hii.Ana kasi, ana uwezo mkubwa wa ufundi uwanjani, ni mzuri kwa mipira ya juu na pia ana uwezo wa kufunga mara kwa mara, lakini kikubwa zaidi ya yote ana mapenzi ya kucheza Newcastle."
Ba atapewa jezi 19 msimu ujao.
BARBETOV KUTUMIKA KATIKA DEAL LA KUMSAINI MODRIC
Manchester United wapo tayari kumtoa Dimitar Berbatov kwa Tottenham kama sehemu ya deal la kuwawezesha kuwapiku Chelsea na kumsajili Luka Modric.
The Daily Star linaripoti kuwa Sir Alex Ferguson ni mtu ambaye anamtamani sana Modric na ameweka wazi kuwa kuwa kiungo wa Croatia ni moja ya wachezaji anawataka katika kipindi hiki cha usajili.
Spurs nao ambao juzi walikataa ofa ya paundi millioni 22 kutoka Chelsea kwa ajili ya Modric kupitia kocha wao wamekuwa wakiweka wazi kuwa Luka Modric hauzwi kwa bei yoyote na watafanya kila linalowezekana kumbakisha White Hart Lane.
Lakini kauli ya Spurs haionekani kumsumbua Ferguson ambaye kwa sasa anajipanga kuwapa Tottrnham ofa ya paundi millioni 18 cash + Dimitar Berbatov katika kuhakikisha anamsaini Modric ambaye wengi wanasema ndiye mrithi sahihi wa Paul Scholes.
LAMPARD AMCHUMBIA DEMU WAKE, HUKU ASHLEY COLE, SHAUN WRIGHT PHILIPPS NA ASHLEY YOUNG NA DEMU WAKE WAKILA BATA IN U.S
ASHLEY COLE, SHAUN WRIGHT PHILIPPS PAMOJA NA ZAT KNIGHT WAKILA BATA HUKO BEVERLY HILLS-CALIFORNIA
ASHLEY YOUNG BAADA KUSITISHA NDOA NA MPENZI WAKE SASA WAPO VEGAS 
FRANK LAMPARD NA CHRISTINE BLEAKLEY WAKIWA UWANJA WA NDEGE WA L.A KURUDI HOME BAADA YA KUCHUMBIANA WIKI HII
MALAVIDAVI MPAKA UWANJANINI MUDA WA FABREGAS KUONDOKA ARSENAL

Muda umefika kwa Arsenal Wenger kuwa na maamuzi sahihi kwa kuamua kufanya maamuzi ya kijasiri ya kumuuza Cesc Fabregas.
Naamini kila ambavyo Fabregas anapolilia kurudi Catulunya ndivyo ambavyo uwezo wa kuisadia Arsenal utakavyopungua, kama mchezaji na kiongozi uwanjani.
Ni wazi kabisa kuwa Fabregas anataka kujiunga na timu ambayo imemlea na kumkuza kama mchezaji, hata amejaribu kudhihirisha mapenzi yake kwa Barca kwa kuamua kuchora tattoo ya motto wa Barca 'Mes que un club'.
Fabregas amejaribu kutimiza ndoto yake kuwa kweli katika kipindi cha misimu 3 iliyopita na bado Wenger mara zote amekuwa akisisitiza mchezaji huyo hauzwi.
KWANINI TUWE TUNASIKIA HUU UJINGA KILA UNAPOFIKA WAKATI WA USAJILI
Cesc anazidi kuchanganyikiwa na kukosa umakini katika kuitumikia Arsenal.Wenger alimpa kitambaa cha unaodha Fabregas kuonyesha ni kiasi gani anamuhitaji mchezaji na anapenda aendelee kubaki Emirates na sio kwa sababu Cesc angeweza kuwa kiongozi mzuri.
Ikiwa unajua timu inaongozwa na mchezaji ambaye anapenda kwenda kucheza timu nyingine basi huyo sio kiongozi katika kuwahamasisha wenzie kuipigania timu kwa mapenzi yote.
Fabregas akiwa majeruhi hakujishughulisha hata kidogo kwenda kuiangalia na kuhamasisha wachezaji wa timu anayoiongoza ikicheza mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Fulha, mchezo ambayo kimsingi ilikuwa ni muhimu kwa timu katika kujihakikishia nafasi ya kucheza Champions League, badala yake bwana mkubwa Fabregas aliamua kwenda kuangalia mashindano ya mbio za magari "Spanish Grand Prix".Inaonekana Fabregas hakuwa anajali kama ambavyo nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ambaye pamoja na kuwa timu yake alikuwa imeshakosa nafasi ya kucheza Champions League alienda kuangalia timu yake akicheza dhidi ya Aston Villa.
.
Fabregas aliulizwa wiki hii kuhusu sakata la Samir Nasri kama mfaransa huyo anapaswa kubaki au kuondoka Emirates alisema: "Samir ana furaha hapa lakini sijui ni kitu gani bora kwa ajili yake".Hii ina maana Fabregas anakosa uhalali wa kumwambia Nasri asiondoke wakati yeye mwenyewe(Fabregas) nataka kuihama klabu hiyo.
Hivi juzi Bacary Sagna amesema ni bora Fabregas aondoke: "Cesc anahitaji kurudi kwenye nchi yake, nyumbani kwake, kuungana na familia yake.Anahitaji kucheza katika moja ya vilabu bora duniani ambayo ni Barcelona."
Mashabiki wengi wa Arsenal wanatofautiana kuhusu Fabregas ambaye msimu uliopita hakuwa katika kiwango kizuri na hakuwa timamu kiafya.
Naamini mashabiki watakubaliana na kuuzwa kwa Fabregas akiwa Wenger atatumia pesa na kusajili wachezaji bora,ikizingatiwa ni ukweli kwamba Arsenal haijashinda kombe lolote tangu Fabregas aje ukiacha kombe la FA ambalo walichukua miaka 6 iliyopita.
Sir Alex Ferguson alijua muda sahihi wa kumuuza Cristiano Ronaldo, United hawakuwa na furaha kuwa na kikosi bila Ronaldo na Ferguson kama angeweza angemrudisha mvhezaji huyo hata leo lakini Boss huyo wa Man United anajua kuuzwa kwa Cristiano ulikuwa ni uamuzi chanya kwa kuwa mchezaji alishaonyesha nia ya kutaka kuondoka hivyo kuendelea kumn'ganinia kungeshusha hadhi ya timu.
Wenger anahitaji kuchukua falsafa ya Fergie kuwa hakuna mcheza mkubwa kuliko timu kwa kuamua kumuuza Fabregas na kutumia fedha kushindana kusajili wachezaji bora duniani.
Kuendelea kumng'aninia Fabregas sio uimara bali ni udhaifu na inaonyesha kuwa Wenger hajui ni jinsi gani ataenwesha timu bila mhispania huyo.
Naamini Arsenal imewahi kuwa na wachezaji bora kuliko Fabregas, tuikumbe Gunners ya akina Tony Adams na kizazi bora kabisa ambacho kiliweka historia nzuri katika ulimwengu soka duniani, hakikuwa na Cesc lakini kilipata mafanikio makubwa.Hivyo kuondoka kwa Fabregas kunaweza kumaanisha kuzaliwa upya kwa Arsenal ambayo italeta furaha iliyopotea katika sura za mashabiki wa GUNNERS.
Naomba kuwasilisha.
MICHEAL BALLACK'S TRIBUTE

Saa 24 zilizopita ulimwengu wa soka ulishuhudia Micheal Ballack moja kati ya viungo bora wa soka kuwahi kutokea duniani kutangaza kustaafu soka katika ngazi ya kimataifa.
Ballack ambaye currently anaichezea klabu ya Bayern Leverkusen ni moja kati ya wachezaji waliofunga mabao mengi katika timu ya taifa katika historia ya soka la timu ya taifa ya Ujerumani.
Micheal Ballack ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1976 alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani mwaka 1996 akianzia katika timu ya vijana na baadae mnamo mwaka 1999 aliitwa katika timu ya wakubwa.
Mpaka anaastafu Ballack tayari amefanikiwa kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani mechi 98 na akifunga magoli 42.
Kitu kimoja kinachomtofautisha Ballack na wachezaji wengine wa kijerumani Micheal amefanikiwa kuvaa jezi namba 13 katika kila timu aliyowahi kuichezea isipokuwa Kaiserslautern.
Ballack alikuwa ni moja kati ya wachezaji bora 125 ambao wapo hai waliotajwa na mfalme wa soka ulimwenguni Pele
Micheal Ballack pia ni moja kati ya wachezaji wachache ambao hawana bahati na mechi za fainali akiwa na timu tofauti.
MIKOSI
Msimu wa 2001/02 na 2007/8 - akiwa na Bayern Leverkusen(2001) walifungwa na Real Madrid katika fainali ya UEFA Champions League, mwaka 2008 akiwa Chelsea walifungwa na Man United in uefa champions league.
Mwaka 2002 akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani walifungwa na Brazil katika fainali ya World Cup.
Mwaka 2008 akiwa na Ujerumani walifungwa na Spain katika fainali EURO.
HIZI NI BAADHI AWARDS ALIZOJISHINDIA BINAFSI
UEFA Club Midfielder of the Year in 2002.
German Footballer of the Year award three times – in 2002, 2003 and 2005.
Thursday, June 16, 2011
MAMBO AMBAYO SIMBA INAPASWA KUZINGATIA UGENINI DHIDI YA DC MOTEMA PEMBE.
Moses Basena-Kocha wa SimbaKuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya kombe la shirikisho ambapo wawakilishi pekee waliosalia wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Simba Sports Club watakuwa wanavaana na timu ya Dc Motema Pembe toka Congo ( Jamhuri ya Kidemokrasia) Blog yako maalum kwa masuala ya michezo imeandaa uchambuzi mfupi wa baadhi ya mambo ambayo Simba wanapaswa kuzingatia ili kuingia kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho .
1.Simba wanapaswa kuelewa kuwa huu ni mchezo wa ugenini.
DC Motema Pembe ina wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka pengine hata kuliko wachezaji wengi wa Simba na ninaposema wana uwezo pengine kuwazidi wachezaji wa Simba simaanishi kuwa Simba haina wachezaji wenye uwezo ila kwa mchezo uliochezwa Jumapili iliyopita Dc Motema Pembe walicheza kwa mbinu na ufundi wa hali ya juu mno.
Kila mchezaji anatambua jukumu lake na analitekeleza kwa ufanisi wa asilimia mia moja hamsini. Kama Simba wakitambua kuwa wanacheza na timu yenye uwezo mkubwa wanapaswa kufanya kila liwezekanalo kucheza kama inavyopasa kucheza ukiwa ugenini . Ukirejea nyuma kwenye msimu wa mwaka 2007/2008 ambapo Manchester United walitwaa ubingwa wa ulaya walikutana na Inter Milan kwenye hatua ya Robo Fainali.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa kule Milan Sir Alex Fergusson alipanga kikosi ambacho mtazamo wake ulikuwa ulinzi kwanza , kwa jinsi United ilivyokuwa kwenye fomu kipindi kile wangeweza kushinda mchezo ule lakini haikuwa kwenye mipango ya Fergie kujilipua na kushambulia mwanzo mwisho , alichezesha timu ambayo ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa wavu hauguswi na hilo lilitimia.
Hivyo Simba wanapaswa kwenda wakiwa na jukumu la msingi ambalo ni kuhakikisha Juma Kaseja haokoti mpira ukiwa umeingia wavuni bali analindwa kiufundi .Kwa msimu huu pekee Simba imecheza mechi zisizopungua tatu za kimataifa nje ya mipaka ya Tanzania na ningependa kuamini kuwa wachezaji wa Simba wamejifunza kitu kwenye mechi hizo hivyo ni vyema wakacheza kama inavyopaswa kucheza unapokuwa ugenini .
2. Akili ya ziada ya kucheza soka tofauti na lile walilozoea kwa kawaida.
Simba ni klabu ambayo ina falsafa ya kucheza soka la kuvutia , kushambulia kwa uvumilivu huku wakitumia viungo wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kuuchezea kama watakavyo , lakini kwa mchezo wa ugenini hii haitakuwa jambo la busara sana kwani Dc wana uwezo wa kufanya lolote na kitibua sherehe ambayo Simba wako njiani kuiandaa.
Kwenye mchezo wa Jumapili Simba hawana budi kucheza kwa tahadhari ya hali ya juu sana wakitambua fika kuwa wanatafuta aina Fulani ya matokeo . Mara nyingi mbinu kuu ya ulinzi kwenye soka ni mashambulizi lakini Simba sasa haina Mbwana Samatta mmoja wa wachezaji wachache wenye uwezo wa kufunga pale anapotaka kufanya hivyo ,hivyo kutokana na hazina ya bao moja ambayo ipo ni vyema falsafa ya Simba ikabadilika japo kwa dakika tisini tu.
3. kuchezesha viungo watano.
Ukitazama safu ya kiungo ya Simba kwenye mchezo wa kwanza ilionekana kupwaya sana . Mohamed Banka na Nico Nyagawa walionekana kuelemewa mwishoni mwa mchezo.Sababu kuu ya hili ni ama kukosekana kwa Jerry Santo au umri wao mkubwa unaweza kuwa uliwagalimu viungo hawa.
Santo anacheza kama kiungo wa kukaba alikosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za manjano. Ni vyema kocha akatambua mchango wa Santo kwa Simba na kumpa nafasi yake kwenye kikosi kitakachocheza.
Lakini pia ili kuwanyima mwanya viungo DCMP wakiongozwa na (NDANDA KOSOVO na KANU) ambao walitumia vyema maumbo yao dhidi ya maumbo madogo ya kina Banka na Nyagawa,
Ili simba iweze kuwadhibiti inatakiwa kuwa na viungo watano Amir Maftah acheze kiungo cha kushoto,Shija Mkina kiungo cha kulia,katikati wacheze santo,nyoso na mbele yao acheze Amri Kiemba.
Santo ana umbo kubwa kama la KANU wa Motema Pembe hivyo kama akipewa jukumu la kucheza naye bluzi (kumkaba ng’ado kwa ng’ado yaani ‘zero distance ‘ kama wafanyavyo maharusi wakicheza blues) tatizo kubwa lililoikabili Simba kwenye mchezo wa kwanza litakuwa limesuluhishwa.
4. Kuepuka kutoa mipira na kucheza madhambi karibu na eneo la hatari.
Unaweza ukashangazwa na hili lakini linaweza kuidhuru Simba . Dc motema Pembe wana mtu ambaye anarusha mipira kwa staili ya aina yake .Jamaa anabinuka sarakasi anaporusha na mipira yake inaenda kwa spidi ya hatari kutokana na nguvu za ziada anazozitumia zinazoupa mpira spidi ya ajabu .
Mipira anayorusha huyu jamaa inaenda kama kona vile na kama ikitokea Simba wakawa wanatoa mipira karibu na eneo la hatari wanaweza kujikuta wakiwapa wapinzani faida kwa kuwa mipira inayoweza kusababisha kizaa zaa kwenye lango la Simba,Pia simba wanatakiwa kuwa makini sana na kufanya madhambi karibu na goli lao.
5. Ally Shiboli aanze badala ya Emanuel Okwi.
Hakuna uficho kuwa Emanuel Okwi alikuwa nyota wa mchezo wakati timu hizi mbili zilipokutana wiki iliyopita . Alikuwa akiifanya ngome ya Motema Pembe kama alivyokuwa anataka na kama Simba wangekuwa makini wangeondoka na ushindi mnono zaidi siku ile kutokana na nafasi nyingi alizokuwa anatengeneza okwi.pia Okwi alicheza vizuri dhidi ya TP Mazembe mchezo uliofanyika huko Lubumbashi,
Kwa hakika Motema Pembe lazima watakuwa wamemtazama kwa karibu mganda huyu na kumtengenezea mbinu za kumkabili wakijua kuwa ndiye anayeweza kuwa tishio hiyo Jumapili.
Kama ningekuwa kocha wa Simba ningecheza na akili zao kisaikolojia kama anavyofanya Jose Mourinho au Sir Alex Fergusson. Kwa vyovyote Simba watafanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo hivyo nigeenda na okwi na kumpa nafasi ya kuwa mzungumzaji mkuu na ningemwambia awaeleze waandishi kuwa ataongoza mashambulizi siku ya mchezo . Kwa vyovyote Motema Pembe wataingia na akili ya kumkabili kwa kuwa watatumia muda mwingi kutazama jinsi ya kumkabili lakini siku ya mechi anaanzia benchi na nafasi yake nampa Shiboli ambaye ana kasi na nguvu.
Kwa kifupi Simba wanatakiwa kujua kuwa wanaingia kutupa karata ya mwisho na karata hii ndio yenye uhai wao linapokuja suala la michuano ya kimataifa , michuano ambayo kwa msimu huu ulioisha imewapa Simba faida ya kujipatia fedha nyingi kutokana na mauzo ya Mbwana Samata na Patrick Ochan waliouzwa baada ya kung’aa kwenye mchezo dhidi ya Tp Mazembe . Huwezi jua pengine kuna vilabu vingine vinavyoweza kuwaona kina Kaseja,okwi,Santo ,Amir Maftah na wengine wakiichezea Simba kwenye hatua ya makundi ya kombe la shirikisho , lakini nafasi hii itakuja kutokana na jinsi watakavyocheza siku ya jumapili ,
6.Seleman Matola kuwepo kwenye benchi la ufundi.
Kwenye mchezo wa kwanza moja kati ya matatizo niliyoyaona ni kukosekana mzawa kwenye benchi la ufundi la Simba ambaye anatakiwa kuwa anawasiliana na wachezaji mara kwa mara wakati mchezo ukiendelea.
Kwa mtizamo wangu Seleman Matola ndiye anayefaa kwenye jukumu hilo,akiwa kama nahodha mwenye mafanikio kuliko wote kwenye historia ya Simba,kitu ambacho kinamfanya kuwa na heshima kikosini.
Mungu Ibariki Simba, Mungu Ibariki Tanzania .
KALI YA LEO: GOLIKIPA AKISHANGILIA BAADA YA TIMU YAKE KUPANDA DARAJA SERIE A + MATUSI YA RONALDINHO
Golikipa wa timu ya Novara Jimmy Fontana akishangilia kwa staili ya aina baada ya kushinda mechi ambayo ilisaidia timu yake kupanda daraja na kufanikiwa kucheza ligi kuu ya Italia msimu ujao.
ANGALIA MATUSI YA DINHO
USAJILI WAZIDI KUPAMBA MOTO BARANI ULAYA.

Totenham imeikataa offer ya paundi milioni 25 kutoka chelsea kumsajili kiungo Luca Modric.

Arsenal imeongeza kasi kuwasajili Gary Cahill,Christopher Samba na Gervinho.
Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis amekutana na bosi wa Bolton Phil Gartside kuzungumzia uhamisho wa beki Gry Cahill pia wapo kwenye mazungumzo mazito na Blackburn kuzungumzia uhamisho wa beki Christopher Samba.

Wakti huo huo Arsenal wamekubaliana na mshambuliaji Gervinho na yupo tayari kumwaga wino kuichezea timu hiyo kwa ada ya uhamisho inayokadiliwa kufika euro milioni 12.

Siyabonga Nomvethe amesaini mkataba wa miaka miwil kuendela kuichezea Moroka Swallows
MUDA WA KUHAMIA ENGLAND UMEWADIA: SAMUEL ETO'O

Samuel Eto'o ametoa habari za kuwashtua wapenzi na mashabiki wa Inter Milan baada ya kusema anatamani kujiunga na ligi kuu ya England- Premier Lague.
Ujumbe huu wa Cameroon straiker umekuja masaa 24 baada ya Inter kuthibitisha kuwa kocha wao Leonardo yupo mbioni kujiunga na PSG.
Eto'o ameliambia gazeti la Corriere dello Sport: "Nafikiria kuhusu kuhusu suala hili, nina mwezi mzima wa kuamua juu ya hili ama niondoke au nibaki.Nina umri wa miaka 30 sasa hivyo inabidi nifikirie vizuri kabla sijasaini mkataba mpya. Niliamua vizuri kucheza Italy na sasa akili yangu inaniambia muda wa kucheza England umewadia."
Kauli ya Eto'o inategemea kuzusha mapigano makubwa miongoni mwa vilabu vya England.
Manchester City, Chelsea and Arsenal wanaonekana ndio watakaokuwa wa kwanza kuanza mbio za kumuwania mcameroon huyo.
Hata hivyo Eto'o aliwahoi kukaririwa akisema angependa kufanya kazi na Gunner's coach Asenal Wenger.
WACHEZAJI WALIOACHWA NA VILABU VYAO KWENYE PREMIER LEAGUE

Arsenal
Thomas Cruise, Roarie Deacon, Mark Randall
Aston Villa
Durrell Berry, John Carew, Ellis Deeney, Calum Flanagan, Harry Forrester, Arsenio Halfhuid, Isaiah Osbourne, Robert Pires, Nigel Reo-Coker, Moustapha Salifou
Birmingham City
Marcus Bent, Lee Bowyer, Sebastian Larsson, James McFadden, Mitchell McPike, James O'Shea, Stuart Parnaby, Kevin Phillips, Daniel Preston, Luke Rowe, Robin Shroot, Maik Taylor
Blackburn Rovers
Jordan Bowen, Jason Brown, Zurab Khizanishvili, Benjani Mwaruwari, Michael Potts, Maceo Rigters
Blackpool
David Carney, Daniel Coid, Ishmel Demontagnac, Rob Edwards, Jason Euell, Marlon Harewood, Richard Kingson, Malaury Martin, Paul Rachubka, Andy Reid, Salaheddine Sbai
Bolton Wanderers
Tamir Cohen, Johan Elmander, Ricardo Gardner, Joey O'Brien, Jlloyd Samuel, Samuel Sheridan
Chelsea
Samuel Hutchinson, Carl Magnay, Danny Philliskirk, Jan Sebek, Michael Woods
Everton
Kieran Agard, Hope Akpan, Nathan Craig, Gerard Kinsella, Lee McArdle, Iain Turner
Fulham
Zoltan Gera, Edward Johnson, Diomansy Kamara, John Pantsil, Matthew Saunders
Liverpool
Jason Banton, Deale Chamberlain, Douglas Cooper, Sean Highdale Steven Irwin, Nikola Saric
Manchester City
Javier Garrido, Scott Kay, James Poole, Shaleum Logan, Andrew Tutte, Javan Vidal, Patrick Vieira, James Wood
Manchester United
Conor Devlin, Owen Hargreaves, Gary Neville, Paul Scholes, Edwin van der Sar
Newcastle United
Sol Campbell, Shefki Kuqi, Patrick McLaughlin
Stoke City
Abdoulaye Faye, Eidur Gudjohnsen, Ibrahima Sonko
Sunderland
Michael Kay, Nathan Luscombe, Daniel Madden, Robert Weir, Nathan Wilson, Mvoto Jean-Yves, Bolo Zenden
Tottenham Hotspur
Jonathan Woodgate
West Bromwich Albion
Giles Barnes, Marcus Haber, Dean Kiely, Abdoulaye Méîté
West Ham United
Anthony Edgar, Holmar Eyjolfsson, Daniel Gabbidon, Lars Jacobsen, Filip Modelski, Jonathan Spector, Adam Street, Matthew Upson
Wigan Athletic
Steven Caldwell, Daniel De Ridder, Joseph Holt, Jason Koumas, Thomas Lambert, Thomas Oakes, Francis Pollitt, Abian Serrano Davila
Wolverhampton Wanderers
Adriano Basso, Jody Craddock, John Dunleavy, Marcus Hahnemann, David Jones, Nathan Rooney
ON THIS DAY:
NYAMLANI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA CAF

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani iliyotumwa kwa Nyamlani jana, kikao kinachofuata cha Kamati hiyo kitafanyika Septemba 25 mwaka huu makao makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, Misri. Nyamlani ambaye kitaaluma ni mwanasheria anakuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika kamati hiyo. Pia ni kiongozi wa mpira wa miguu kwa muda mrefu akianzia Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke (TEFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF.
UNITED YATHIBITISHA KUONDOKA KWA MKOPO

Manchester United wamethibitisha kuwa winga wao Bebe anakwenda kucheza kwa mkopo katika klabu ya Basiktas ya Uturuki msimu mzima wa 2011/2012
Bebe alisajiliwa na Sir Alex Ferguson kutoka Vitoria kwa ada ya paundi millioni 7.4 msimu uliopita ingawa na mchezaji huyo hakuwahi kuichezea timu hiyo ya Ureno mechi yoyote.
UDINESE YAMWACHIA UAMUZI WA MWISHO SANCHEZ
Udinese wamethibitisha kuwa klabu tano za Juventus, Inter, Man City, Man United, na Barcelona wametoa ofa ambazo wanakubaliana nazo na sasa uamuzi kumuuza timu gani kati hizo wamemuachia Alexis Sanchez mwenyewe.
Mabingwa Europa Barcelona jana usiku kupitia makamu wa raisi alithibitisha kufanya mazungumzo na Udinese lakini kutokana kuwa na fungu dogo la usajili nafasi ya Sanchez kwenda Nou Camp itategemea na mchezaji mwenyewe.
City ambao wamekuwa wakiongoza mbio za kuwania saini ya mchile huyo kwa kipindi kirefu pamoja na kutoa ofa nzuri sana kwa Udinese lakini Sanchez mwenyewe haonekani kuwa na matamanio ya kujiunga nayo.
United ambao nao juzi walimtuma mkurugenzi mtendaji wao David Gill hadi Spain kwenda kumalizana na raisi wa klabu ya Udinese anayeishi Spain wanaonekana kuwa moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kumnyakua winga huyo, huku kocha Sir Alex Ferguson akionekana hayupo kufanya kosa alilolifanya kwa Ronaldinho kwa kumuacha Alexis Sanchez mchezaji ambayeamekuwa akimtamani kwa zaidi ya miaka 3 aende kwa mahasimu wa ulaya Barcelona.
Inter na Juve nao wamejitutumua kwa kutoa ofa zinazoeleweka lakini mchezaji mwenyewe anasema kama akihama Udinese angependa kwenda kucheza nje ya nchi ya Italy
Udinese's transfer consultant Stefano Antonelli, ambaye ndio anayedili na madili makubwa amethibitisha kuwa kwa sasa wanaaangalia chaguo bora la kumuuza Sanchez huku akisema Alexis mwenyewe atahusishwa na kuchagua wapi pa kwenda.
BLOG HII INAITAKIA SIMBA SAFARI NJEMA!
Magolikipa:
Juma Kaseja,Ally Mustafa
Mabeki:
Salum Kanoni,Juma Jabu,Amir Maftaha,Kelvin Yondani,Juma Nyoso na Meshack Abel
Viungo
Nico Nyagawa ( Nahodha ),Mohamed Banka,Amri Kiemba,Jerry Santo,Abdulhalim Humud
Washambuliaji
Mussa Hassan Mgosi,Emanuel Okwi,Ally Ahmad Shiboli,Kelvin Charles na Shija Mkina.
HATUMUUZI NEYMAR - SANTOS WAIAMBIA CHELSEA

CHELSEA wameambiwa kuwa wanapoteza muda wao kwa kujaribu kumsajili Brazilian wonder kid Neymar.
Onyo hilo limetolewa na na raisi ywa klabu ya Santos Luis Avaro de Oliveira.
The Blues walimtuma na kumpa madaraka wakala maarufu wa wachezaji Pini Zahavi kwenda Brazil kufungua majadiliano ya kumsaini Neymar Chelsea, lakini Santos kupitia raisi wake wameweka wazi kuwa kinda wa hauzwi ingawa Chelsea wanaamini hiyo janja tu Santos kutaka kupandisha bei ya Neymar.
De Oliveira amesisitiza kuwa,: " Kwa sasa tupo katika maongezi na wadhamini wetu wakubwa waweze kutufanikishia mpango wa kuhakikisha Neymay anaendelea kuwa mchezaji wetu kwa kumpa dili nzuri ya kueleweka.Kumekuwa hakuna ofa mpya iliyokuja ndani ya siku kadhaa zilizopita lakini zikija bado tutazikataa."
Neymar mwenyewe amezungumza na kusema kuwa "Ndoto ya wabrazili wengi ni kucheza ulaya na kwangu haipo tofauti."
Wednesday, June 15, 2011
EDMUNDO KWENDA JELA KWA KESI YA MAUAJI

Jaji wa mahakama ya jiji ya Rio De Jeneiro Eduardo Carvalho de Figueirdo ametoa amri ya kukamatwa kwa straiker wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Edmundo kwa kusababisha ajali ya gari ambayo ilichukua maisha ya watu 3 mwaka 1995.
Edmundo ambaye aliwakutwa na hatia ya kufanya mauji bila kukusudia mwaka 1999., lakini akakata rufaa na akashindwa lakini hatua za kisheria dhidi yake hazikuchuliwa mpaka jana Jumanne Jaji Eduardo alipotoa amri ya kukamatwa kwake.
Mawakili wa Edmundo wamesema watakata rufaa tena.Kwa sasa bado Edmundo hajakamatwa.
Edmundo kwa sasa ana umri wa miaka 40 aliwahi kuzichezea klabu 13 tofauti akianzia Vasco Da Gama, Flamengo, Palmeiras, Corinthians, Napoli, Cruzeiro, Fluminense, Fiorentina, Santos, Tokyo Verdy, Urawa Red Diamonds, Nova Iguaçu, na Figueirense.
Katika kipindi cha hivi karibuni Edmundo amekuwa ni commentator wa television nchini Brazil.
JIKUMBUSHE KIDOGO UWEZO WA EDMUNDO THE ANIMAL
HAPPY BITHRDAY OLIVER KAHN NA TORE ANDRE FLO.
TORE ANDRE FLO NA YEYE AMETIMIZA MIAKA 38 SIKU YA LEO.
INTER YATHIBITISHA KUONDOKA KWA LEONARDO-YAMTAKA MARCELO BIESLA

INTER MILAN wamethibitisha kuondoka kwa kocha wao Leonardo na wanamuwania Marcelo Biesla kama mbadala wa mchezaji huyo wa zamani wa Brazil na AC milan.
Leonardo ambaye alikuwa mbadala wa Rafa Benitez ndani ya Inter ameisadia timu hiyo kushika nafasi ya pili kwenye Serie A na pia ameipa timu hiyo ubingwa wa kombe la Italia, lakini Leonardo jana alithibitisha kuwa yupo katika mipango ya kuhamia Paris Saint Germain ya Ufaransa baada ya kufanya mazungumzo na wamiliki wapya wa timu hiyo Qatar Sports Investments.
Inter president Massimo Moratti ambaye mwanzo alikanusha kuondoka kwa Leo" ameandika katika website ya Inter kuwa kocha huyo anaweza kuondoka Guisseppe De Meazza.
"Leonardo ameifundisha timu yetu kwa mapenzi makubwa lakini anaweza asiwe na sisi msimu ujao, ni kitu kizuri ametuambia mapema na sisi tumeanza kujiandaa kutafuta kocha mpya.Anaweza akawa Leonardo kama akiamua kubadilisha mawazo.Hata hivyo tayari tumeshafanya mawasiliano na Biesla kumshawishi ajiunge nasi msimu ujao.
Wakati huo huo taarifa kutoka Italia zinasema kuwa Raisi huyo wa Inter amewaambia Real Madrid wanaweza kumpata Douglas Maicon ikiwa watawapa Sergio Ramos.

Corriere dello Sport limesema kuwa kocha Jose Mourinho yupo tayari kumtoa Marcelo katika dili hilo lakini Morrati amesisitiza kumtaka Ramos.
FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE KUCHEZWA TENA WEMBLEY

Uwanja wa Wembley kesho vunatarajiwa kutangazwa na UEFA kuwa ndio mahali patakapochezwa fainali ya UEFA Champions League mwaka 2013.
Mafanikio ya fainali ya msimu huu kati ya Barcelona na Manchester United yamewafanya UEFA waamue kurudisha fainali ya champions league ndani kiwanja hicho kilichopo London Uingereza.
Uamuzi wa kuupa Wembley uenyeji unatarajiwa kutangazwa kesho na Raisi wa UEFA baada ya mkutano wa kamati kuu ya UEFA katika jiji la Nyon, Switzerland.
Habari zinasema kuwa pamoja na mafanikio ya fainali ya mwaka huu lakini UEFA wameamua kuipeleka fainali ya 2013 pia ili kuenzi sherehe za kutimiza miaka 150 ya chama ya soka cha England.
NI SAHIHI JAVIER PASTORE KUUZWA KWA PAUNDI MILLIONI 44
Hivyo jana usiku Raisi wa Palermo Maurizio Zamparini amesema wazi kabisa kuwa timu itakayotoa kiasi kisichopungua paundi million 44 ndio itakayoshinda mbio za kumsaini kinda hilo la Kiargentina.
JE NI SAHIHI KWA JAVIER PASTORE KUUZWA KWA PAUNDI MIL 44 - ANGALIA VIDEO HII
HISTORIA FUPI JAVIER PASTORE

Javier Pastore ambaye ana umri wa miak 21 alianza kucheza soka la ushindani katika timu ya daraja la pili nchini Argentina katika timu ya Talleres mwaka 2007 ingawa hakuwa anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo kupelekea kwenda kwa mkopo katika timu ya ligi kuu ya Huracan na kwa bahati nzuri akaonyesha kiwango kikubwa kilichompa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza katika timu hiyo.
Mwaka 2009 alisajiliwa na Palermo ambapo upo mpaka sasa, akiwa tayari kashachezea timu hiyo michezo 68 ndani ya misimu miwili na amefanikiwa kufunga magoli 17 na akitoa assists 11.
Javier Pastore ambaye pia mwaka 2010 alichaguliwa "SERIE A YOUNG FOOTBALLER OF THE YEAR" alikuwa moja ya wachezaji katika kikosi cha Diego Maradona ndani ya mshindano ya World Cup 2010 na kuishia robo fainali.
KEVIN NOLAN AFANYIWA VIPIMO WEST HAM

NEWCASTLE skipper Kevin Nolan anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya ili aweze kujiunga na West Ham United mara baada ya Newcastle na West Ham kukubaliana katika dili ambalo halijatajwa.
The Magpies walikataa ofa ya paundi million 3 kwa ajili ya midfielder huyo wiki iliyopita lakini the Hammers hawakukata tamaa.
New Hammers boss Sam Allardyce, ambaye alifanya kazi na Nolan wakiwa Bolton alimtaja mchezaji huyo kama ndio target ya kwanza katika kipindi hiki cha usajili.
Nolan — alikuwa ndio mfungaji bora wa Newcastle akiwa kafunga magoli 12 lakini baada ya ligi kuisha alikataa kusaini mkataba mpya na timu hiyo yenye maskani yake St.James Park.
Wakati huo huo habari za kuondoka kwa Nolan zimemfanya mchezaji mwenzie Joe Barton kukasirika akiandika kwenye ukarasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ---- "Great player, leader, captain, person, trainer and mostly a friend for life. Devastated to see him SOLD! #mejoseandjonasnext."
HAPPY BIRTHDAY LADY JAY DEE SHABIKI WA YANGA NA CHELSEA

LEO TAREHE 15 MWEZI WA JUNE NI SIKU YA KUZALIWA YA GWIJI LA MUZIKI NCHINI TANZANIA KOMANDO LADY JAY DEE.PAMOJA NA KUWA MWANAMUZIKI JAY DEE PIA NI MPENZI MKUBWA SOKA NA BILA KUFICHA SIKU ZOTE AMEKUWA AKIONYESHA MAPENZI MAKUBWA ALIYONAYO KWA TIMU YA YANGA NA CHELSEA YA ENGLAND.
KATIKA KUADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA BLOG HII IMEFANYA INTERVIEW NA QUEEN WA BONGO FLAVA KUHUSU TIMU ZAKE ANAZOZISHABIKIA.
BLOG: KATIKA KIPINDI HIKI CHA USAJILI UNGEPENDA TIMU YAKO YA YANGA IMSAJILI MCHEZAJI GANI?
JAYDEE: KUTOKANA NA KUTOKUWA NA UTALAAM WA KUJUA NI MAHALI GANI PANA MAPUNGUFU KATIKA KIKOSI CHA YANGA SIWEZI KUTOA MAPENDEKEZO NANI ASAJILIWE LAKINI MCHEZAJI AMBAYE SIKU ZOTE NINGEPENDA ARUDI YANGA NI SHABAAN NONDA.
BLOG: ULIANZA KUZISHABIKIA YANGA NA CHELSEA LINI?
JAYDEE: YANGA NIMEIPENDA TANGU NIMEPATA UFAHAMU ILA CHELSEA NI KATIKA MIAKA YA 2000
BLOG: TIMU YA CHELSEA KWA SASA HAINA KOCHA JE UNGEPENDA NANI AWE KOCHA WA CHELSEA MSIMU UJAO?
JAYDEE: HILI SUALA NI LA KIUFUNDI ZAIDI HIVYO NADHANI KOCHA YOYOTE MZURI ATAKAYETEULIWA NA JOPO LA WATAALAM WA CHELSEA ATAFAA KUIFUNDISHA TIMU YETU MSIMU UJAO NA KUWAPOKA UBINGWA MAN UNITED
AZAM WAANZA MAZOEZI
WACHEZAJI WA TIMU YA AZAM FC WAANZA KUJIFUA GYM LEO
Kocha wa makipa wa timu ya Azam FC Idd Abubakary akiwaelekeza makipa wa timu hiyo wakati wa mazoezi ya Gym, yaliyoanza kufanywa na wachezaji wa timu hiyo leo kwenye Gym ya Fitness Center Kinondoni jijini Dar es salaam, kulia ni golikipa Mwadini Ali Mwadini ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Zanzibar na kushoto ni kipa Daud Mwaisongwe.
Mchezaji wa timu ya Azam FC kutoka nchini Ivory Coast Kipre Helman Cheche akifanya mazoezi katika Gym iliyopo Finess Center iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam leo. MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 15, 2011
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubali kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Kagame yanayoshirikisha klabu bingwa za nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Klabu 12 zitashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika nchini kuanzia Juni 25 hadi Julai 9 mwaka huu.
Tumechukua uamuzi huu mgumu wa kuandaa mashindano haya kwa lengo la kuyaokoa. Awali mashindano hayo ambayo yalianzia nchini mwaka 1974 yalikuwa yafanyike Zanzibar ambayo ilijitoa.
Baadaye yalihamishiwa Sudan ambapo napo yalikwama baada ya Serikali ya nchi hiyo kutokuwa tayari kuwa mwenyeji kwa sasa kutokana na sababu mbalimbali.
Hivyo tunaziomba kampuni mbalimbali nchini zijitokeze kwa ajili ya udhamini ambao utawezesha kufanyika kwa ufanisi.
Jumatatu (Juni 20 mwaka huu) tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuelezea taratibu za mashindano hayo ikiwemo timu zitakazoshiriki. Tanzania kwa kuwa mwenyeji itaingiza timu mbili.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
TFF, VILLA SQUAD KUKUTANA KESHO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Juni 16 mwaka huu) atakutana na wadau mbalimbali ili kuangalia mustakabali wa klabu ya Villa Squad ambayo msimu huu itashiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Mkutano huo utafanyika makao makuu ya TFF kuanzia saa 9 kamili.
Mbali ya Rais Tenga na Sekretarieti yake, wadau wengine katika mkutano huo ni wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya Villa Squad na viongozi wa klabu hiyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
POULSEN, MAKOCHA KUTETA JIJINI DAR ES SALAAM
muandishi: JOHN BUKUKU wa FULLSHANGWE BLOGSPOT.











