WACHEZAJI WA TIMU YA AZAM FC WAANZA KUJIFUA GYM LEO
Kocha wa makipa wa timu ya Azam FC Idd Abubakary akiwaelekeza makipa wa timu hiyo wakati wa mazoezi ya Gym, yaliyoanza kufanywa na wachezaji wa timu hiyo leo kwenye Gym ya Fitness Center Kinondoni jijini Dar es salaam, kulia ni golikipa Mwadini Ali Mwadini ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa ya Zanzibar na kushoto ni kipa Daud Mwaisongwe.
Timu hiyo imeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza mwezi Agosti mwaka huu nchini.
Mchezaji wa timu ya Azam FC kutoka nchini Ivory Coast Kipre Helman Cheche akifanya mazoezi katika Gym iliyopo Finess Center iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
No comments:
Post a Comment