Na Baraka Mpenja, Dar
Es Salaam
0712461976
Michuano ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho katika
raundi ya 25 ambapoTanzania Prisons na Rhino Rangers wataumana Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal Union watakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Keshokutwa (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi nyingine tano za kukamilisha raundi hiyo.
Simba watavaana na Ashanti
United Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.
Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Kesho mtandao huu utakupatia uchambuzi mwingine kuelekea mechi hizo za keshokutwa ili kubashiri ni timu gani inaweza kushinda.
SIMBA VS ASHANT UNITED
Hii ni mechi yenye mvuto
kwa kuangalia umuhimu wa matokeo kwa Ashanti United waliopo katika hatari kubwa
ya kushuka daraja.
Ashanti wamecheza mechi 24
na kufanikiwa kushinda mechi 5, sare 7 na kupoteza mechi 12, hivyo kujikusanyia
pointi 22 katika nafasi ya 12.
Mbele ya Ashanti United
wapo Tanzania Prisons waliocheza mechi 24 ambapo wameshinda mechi 4, sare 10 na
kufungwa mechi 10.
Kinachowafanya Prisons wawe
juu ya Ashanti ni wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Prisons wamefunga mabao 21
na kufungwa mabao 30. Ukitoa mabao ya kufunga na kufunga unapata hasi tisa
(-9).
Ashanti wamefunga mabao 19
na kufungwa mabao 38, hivyo ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa unapata hasi
kumi na tisa (-19).
Kwa hesabu hizo, Prisons
wanakuwa juu ya Ashanti hata kama wote wana pointi 22 katika michezo yao 24
waliyoshuka dimbani.
Kwa mazingira haya ya
Ashanti United, mechi ya keshokutwa ni muhimu sana, tena wanahitaji kushinda mabao
mengi zaidi kwasababu hata Prisons watakuwa na mchezo dhidi ya vibonde Rhino
Rangers kutoka mjini Tabora katika uwanja wao wa Sokoine jiji Mbeya.
Simba sc hawana cha
kupoteza mpaka sasa, hawawezi kutwaa ubingwa wala kushika nafasi tatu za juu
kwa pointi zao 37, huku wakibakiza mechi mbili tu.
Endapo Simba sc watashinda
mechi zote watafikisha pointi 43 ambazo zilishavukwa na Mbeya City walioopo
nafasi ya tatu.
Hivyo Simba baishara yao ni
nafasi ya nne ambayo wanapambana na Kagera Sugar wenye pointi 34 katika nafasi
ya tano, huku wakibakiza mechi mbili.
Kama Kagera Sugar
watashinda mechi zote watafikisha pointi 40, na ili kuipata nafasi ya nne
watatakiwa kuwaombea Simba wapoteze mechi zote mbili.
Simba sc kwasasa wanahitaji
heshima tu kwa kushinda mechi zao zilizobaki.
Kwa mazingira hayo bila
shaka wamejiandaa vizuri kuwafunga Ashanti United keshokutwa katika dimba la Taifa.
Kocha Mkuu wa Simba sc,
Mcroatia Dravko Logarusic ataingia uwanjani kwa kusaka ushindi mbele ya kocha
wa Ashanti Abadallal Kibadeni “King Mputa”.
Huu utakuwa mchezo mgumu
zaidi kwa Kibadeni kwasababu matokeo yanayomfaa kwakwe ni ushindi tu.
Kama atashinda mechi ya
keshokutwa itakuwa faida kubwa kwake. Kwa mana hiyo kesho ataingia kwa nia ya
kushambulia na kulinda lango lake kwa muda wote.
Simba na Ashanti wana malengo
tafauti kabisa kwasababu Simba wanahitaji kulinda heshima, wakati Ashanti
wanataka kukwepa kushuka daraja.
Mtumwa zaidi katika mechi
hiyo ni Ashanti kwasababu pointi tatu zitaamua hatima yao, wakati Simba
kwao hata kama wakizikosa hakuna madhara ya kushuka daraja.
Hii itakuwa mechi nzuri ya
kuifuatilia kwani soka la ushindani na maarifa linaweza kuonekana hasa kutoka
kwa Kibadeni ambaye mzunguko wa kwanza alikuwa kocha mkuu wa Simba.
Kwa kiasi fulani Kibadeni
anawafahamu wachezaji wa Simba na utamaduni wao, hivyo inaweza kuwa faida kwake.
Inadhihirika wazi kuwa
kucheza na timu inayokwepa kushuka daraja, mechi inakuwa ngumu zaidi, kwasababu
hiyo, Loga wa Simba sc lazima awe na mipango mizuri na asipoangalia anaweza
kupoteza mechi hiyo.
TANZANIA PRISONS VS RHINO
RANGERS
Wakati Ashanti wakiumiza
kichwa kupata matokeo katika mechi hiyonya jumapili, nao Tanzania Prisons ambao ni
washindani wao kukwepa kushuka daraja watakuwa na vibonde wa ligi hiyo, Rhino
Rangers kutoka mkoani Tabora katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya siku ya kesho.
Pengine mechi hii itakuwa
na unafuu kwa Prisons wanye machungu ya kufungwa mechi mbili zilizopita.
Walifungwa mabao 5-0 dhidi
ya Yanga na wakafungwa mabao 21 na JKT Oljoro mjini Arusha. Sasa kesho wapo
nyumbani kucheza na timu dhaifu ya Rhino Rangers.
Udhaifu unaosemwa hapa ni
matokeo wayapatayo Rhino msimu huu, lakini si jinsi wanavyocheza.
Wanajeshi hawa JWTZ
wanacheza mpira mzuri, lakini katika mpira mshindi na mshindwa lazima
atokee.
Kwa maana hiyo, Prisons
wana kazi kubwa ya kuwafunga vibonde hawa walipo mkiani kwa pointi 16 baada ya
kucheza mechi 24.
Mechi hii haina mvuto hata
kwa mashabiki wa soka jijini Mbeya kutokana na matokeo waliyonayo Prisons na
Rhino, lakini kwa watu wa mpira, hii ni mechi ambayo burudani kubwa inaweza
kuonekana.
Prisons watashinikiza
kushinda, wakati Rhino ambao wameshashuka daraja kwa asilimia zote watakuwa
wanapambana angalau kushuka daraja na ushindi.
COASTAL UNION VS JKT RUVU
Mechi nyingine nzuri ya
kesho ni baina ya Coastal Union dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa CCM
Mkwakwani jijini Tanga.
Coastal walipoteza mechi
iliyopita kwa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo katika uwanja wa Mkwakwani, wakati JKT
Ruvu walipoteza kwa mabao 5-1 kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga ndani ya
uwanja wa Taifa.
Mtazamo wa mechi hii kwa
timu zote mbili unatofautina kabisa.
JKT Ruvu wenye pointi 28
katika nafasi ya 9 baada ya kucheza mechi 24 watakuwa wanahitaji ushindi
ili kufikisha pointi 31 ambazo zitaweza kuwaokoa kushuka daraja.
Hata sare itakuwa na faida
kubwa zaidi kwao, kwasababu watafikisha pointi 29 ambazo hazitaweza kufikiwa na
Ashanti United na Prisons isipokuwa Mgambo waliopo nafasi ya 10 kwa pointi 25
huku wakiwa na michezo miwili mkononi.
Coastal Union wapo nafasi
ya 8 kwa pointi 29 baada ya kucheza mechi 24. Nafasi hii si nzuri kwao
kwasababu ya kikosi chao kuwa na wachezaji wa gharama.
Kikosi cha wagosi wa Kaya
kilitabiriwa kufanya vizuri sana msimu huu, lakini wamegeuka kuwa `mbogo` kwani
wanapoteza mechi mara kwa mara.
Kwahiyo mechi ya Mkwakwani
itakuwa nzuri kwasababu timu zote zinahitaji ushindi ili kuendelea kujiweka
mazingira mazuri zaidi katika msimamo.
Tafadhali endelea kuwa nasi
na usisite kutoa maoni yako.
No comments:
Post a Comment