Timu ya Watoto
wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini
Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali imetambulishwa leo (Aprili
11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
Baadaye
timu hiyo leo itapata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mizengo Pinda. Saa 10 jioni itatembeza kombe hilo katika maeneo
mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi.
Jioni
imeandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini Dodoma
ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.
Fenella Mukangara.
MWENYEKITI WA CECAFA KUZUNGUMZA
NA WAANDISHI
Mwenyekiti
wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),
Leodegar Tenga atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Jumatatu (Aprili 14
mwaka huu).
Mkutano
huo utafanyika kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
zilizopo Ghorofa ya 3, Jengo la PPF Tower mtaa wa Ohio/Garden Avenue kuanzia
saa 5 kamili asubuhi.
CHACHA KUCHEZESHA MICHUANO YA AYG
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua
mwamuzi msaidizi wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA), Ferdinand Chacha ameteuliwa kuchezesha michezo ya Vijana ya
Afrika (AYG- African Youth Games).
Michezo hiyo ya kwanza ya Afrika itachezesha jijini
Gaborone, Botswana kuanzia Mei 22-31 mwaka huu. Tanzania pia itashiriki katika
mashindano hayo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
wakati hao madogo wanaungaunga kwenda kwenye michuano TFF ilikuwa na mchango gani kwao!!??..waache kujitia viherehere... UNAFKI ULIOPITILIZA
ReplyDelete