Anabadilishwa: Tottenham wametangaza kuachana na kocha wao Tim Sherwood mwishoni mwa msimu huu
KIBARUA cha kocha mkuu wa Tottenham,Tim Sherwood kinamalizika mwishoni mwa msimu huu na mikoba yake itachukuliwa na kocha chaguo la kwanza la klabu hiyo, Louis Van Gaal.
KIBARUA cha kocha mkuu wa Tottenham,Tim Sherwood kinamalizika mwishoni mwa msimu huu na mikoba yake itachukuliwa na kocha chaguo la kwanza la klabu hiyo, Louis Van Gaal.
Sherwood alirithi mikoba ya Andre Villas-Boas mwezi desemba mwaka jana na kusaini mkataba wa miezi 18, lakini klabu yake haina mpango naye na inatafuta kocha mpya.
Kocha huyo mwenye miaka 45 amezungumza na mtandao wa michezo wa Sky sports na kusema " siwezi kuzungumza sana kuhusu hilo kwa sasa. Ninachoweza kusema ni kuhusiana na mechi ya leo usiku dhidi ya Sunderland".
"Naiandaa timu kwa ajili ya kushinda mchezo wa leo kwa faida ya klabu na mashabiki wake elfu 35, 000 watakaokuja kuishangilia timu".
'Nitalizungumzia hilo baada ya mechi".
Anarudi kuwa msaidizi? Sherwood anaweza kupewa kibarua cha kufanya kazi chini ya bosi mpya wa Spurs
Kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal ndio chaguo la kwanza la Spurs, japokuwa klabu hiyo pia inamfikiria kocha wa Southampton, Mauricio Pochettino na Carlo Ancelotti kama itatokea anaondoka Real Madrid.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Sherwood atapewa nafasi ya kuwa msaidizi wa kocha mpya ijaye, ingawa haijafahimika bado kama nahodha huyo wa zamani wa Blackburn atakubaliana na hilo.
Van Gaal anategemewa kubwaga manyanga kuifundisha timu ya taifa ya Uholanzi baada ya fainali za kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil.
Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy ameorodhesha majina ya makocha anaowata na hajaweka kuwa siri hata kidogo.
Pochettino wa Southampton naye amekuwa miongoni mwa majina hayo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya katika klabu yake msimu huu.
No comments:
Post a Comment