Jopo wa wang’amuzi vipaji limetangaza majina ya
wachezaji 36 waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars
ulioshirikisha mechi za mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143
katika mchakato, lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu.
Amewataja wachezaji waliochaguliwa katika mchakato
huo kwa upande wa makipa ni Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar
Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali
(Kaskazini Unguja).
Kwa upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika
mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward
Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba
(Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki wa kati ni Abbas Ali Haji (Kaskazini
Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke), Hussein Juma Akilimali
(Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus Henrico (Ilala), Miraji Maka
(Mwanza), Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini
Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).
Viungo wapo Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim
Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga),
Ryna Mgonyike (Temeke) na Yusuf Mpilipili (Temeke).
Washambuliaji ni Abdallah Kagumbwa (Temeke), Abrahman
Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu
(Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo
Mussa (Tanga), Michael David Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar
Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto
(Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).
Amesema wastani wa umri wa wachezaji hao ambao watafanyiwa
vipimo vya afya Machi 19 na 20 mwaka huu kabla ya kambini Machi 21 mwaka huu,
Tukuyu mkoani Mbeya ni miaka 21.
Timu hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na
makocha Hafidh Badru, Salum Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu
utafanyika mchujo ili kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa
Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki
mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani
nchini Morocco.
Home grown solutions?angalau kuwe na utafiti kwanza.Soka sio rahisi kihivyo,yaani ukusanye wachezaji mchangani halafu wakupeleke AFCON 2015?Uwashinde nchi nyingine zilizofuata programu za kitaalamu za maendeleo ya soka?hakuna shortcut kwenye soka.Cape Verde,Burkina Fasso,Ivory Coast,Mali,Angola,Msumbiji,Senegal etc tulikuwa nao level moja lakini sasa wametuacha.Kumbuka tulipokwenda fainali za AFCON 1980 kule Nigeria tulitoka sare na Ivory Coast.Hawa makocha wanamtapeli Malinzi kwa vile hajui mpira.Kwanza wametumia vigezo gani kuwapata hao wang'amuzi wa vipaji?CV zao zikoje?rafiki zake Kidao kina Pawasa,Mayai?Yaani wale jamaa waliokaa Zanzibar na kutoa ushauri huu ndio hao hao wamejigeuza tena kuwa wang'amuzi wa vipaji?Nchi hii nzuri sana wewe,hawa wachambuzi wa soka wanaondika makala kwenye magazeti ndio hao hao leo hii wameonekana wanafaa kuwa wang'amuzi wa vipaji,kuchambua wapi kung'amua vipaji wapi?ndio maana wakati fulani miaka ya 1990 washabkiki na wanachama wa Simba sc walitaka Dr Liki Abdallah awe kocha wa Simba kisa uchambuzi wake.Kufundisha soka ni kitu kimoja,kuchambua soka ni kitu kingine tofauti na ,kung;amua vipaji ni kitu kingine tofauti kabisa haviwezi kufanywa na mtu mmoja
ReplyDeleteumesema vizuri sana mdau,watanzania wapenda soka tutajuta kumkabidhi zamana ya mpira wetu mtu wa boxing( rejea DJB promotions Enzi za kina Rashid Matumla),ataendelea kudanganywa sana cuz sio mtu wa mpira
Delete