Kocha wa Yanga,Hans Van Pluijm amesema hatabadili mfumo uliotumika
Dar Es Salaam kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahly,
‘’Kwenye mchezo wa Dar Ahly waliwatumia wachezaji tisa nyuma ya mpira na bado tulifanikiwa
kutengeneza nafasi nyingi,naamini kwenye mchezo wa marudiano watalazimika
kutushambulia nasisi tutatumia mwanya huo huo kuwashambulia.
Napendelea mchezo wa kushambulia,kama unataka kushinda mechi
ni lazima ufunge magoli,lakini pia timu yetu ni nzuri sana kwenye idara ya
ushambuliaji kuliko idara ya ulinzi,ningependelea mchezo wa kushambulia lakini wachezaji
wanahitaji kuwa na nidhamu kubwa ya kufuata maelekezo’’.
Van Pluijm pia amesema kikosi chake kipo vizuri na hakiogopi
majina makubwa ya wachezaji wa Ahly, ‘’Majina hayachezi mpira bali timu ndio
inacheza, kinachotakiwa ni wachezaji kujiamini na kuamini wanaweza,wakifanikiwa
katika hilo naamini tutawashangaza ‘’.
Shaffih tunaomba live coverage baadae jioni.Kila la kheri
ReplyDeleteMungu ibariki dar yng africa,
ReplyDelete