KAMATI
ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
ilifanya kikao chake cha kwanza chini ya uenyekiti wa Juma Pinto juzi Jumatatu
Machi 10, 2010 jijini Dar es Salaam na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali.
1;
MAFUNZO
Kikao
kilikubaliana kuelekeza nguvu katika mafunzo kwa wanachama wake na kwa kuanzia
kamati iliagiza sekreterieti ya TASWA ihakikishe inasimamia hilo kwa nguvu zote
ili kuboresha uwezo wa namna ya kuripoti michezo mbalimbali hasa kwa waandishi
chipukizi.
Katika
hilo bajeti maalum itaandaliwa kwa ajili ya kuona namna ya kushirikiana na
wadau mbalimbali watakaosaidia mafunzo hayo ikiwemo Chama cha Kimataifa cha
Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS).
2;Media Day
Kama
inavyojulikana kwamba kila mwaka TASWA inaandaa bonanza maalum likihusisha
waandishi na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Mwaka
huu Kamati ya Utendaji imepanga lifanyike Mei 10 jijini Dar es Salaam katika
eneo ambalo lina fukwe nzuri. Hivyo tayari watu maalum wameshateuliwa kufanya
utaratibu wa mahali litakapofanyika.
Pia
mazungumzo na wadhamini mbalimbali kuhusu bonanza hilo litakaloenda sambamba na
sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yameanza na yana
muelekeo mzuri, ambapo litashirikisha waandishi wa habari na wafanyakazi wa
vyombo mbalimbali vya habari 2,000.
3;Tuzo za Wanamichezo Bora
TASWA
imeunda kamati maalum ya kusimamia tuzo hiyo na kuifanya iwe bora pengine
kuliko za miaka iliyopita. Majina ya kamati hiyo tutayatangaza baada ya wote
kuwa wameshapatiwa barua zao za uteuzi na kuzijibu. Tarehe ya tuzo ni baada ya
kamati kukutana na ndiyo itakayopendekeza kulingana na majukumu iliyopewa.
4; Marekebisho ya Katiba
Pia
kikao kilikubaliana kuelekeza nguvu katika marekebisho ya katiba ya chama.
Katika kufanikisha hilo imeundwa kamati maalum kwa ajili ya jambo hilo. Majina
ya kamati hiyo pia yatatangazwa baada ya wote kuwa wameshapewa barua zao na
kujibu kwa maandishi.
5;SACCO’S
Kwa kuwa suala hili lilishapitishwa kwenye Mkutano
Mkuu wa chama Desemba 2012, kikao kilikubaliana lifanyiwe kazi na utekelezaji
uanze sasa.
Utaratibu
unaandaliwa kuhusiana na jambo hilo baada ya kupata mwongozo kutoka vyama vya
ushirika, kisha wanachama wa TASWA watajulishwa na wale watakaopenda kujiunga
watapewa maelekezo kwani hilo ni jambo la hiyari kwa yule atakayependa.
6: Uhai wa chama
Suala
la uhai wa chama lilichukua nafasi kubwa, hivyo utaratibu maalum utawekwa
kuhamasisha waandishi wa habari za michezo hasa wale wa mikoani kujiunga na chama.
Ili
kuweka mkazo jambo hilo, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA na
baadhi ya wanachama watapewa fursa kwa ufadhili wa chama kusafiri maeneo
mbalimbali mikoani kuhamasisha waandishi wa huko kujiunga na chama.
Ahsante.
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
12/03/2014
No comments:
Post a Comment