Search This Blog

Monday, March 24, 2014

SIMBA CHINI YA MTU MWEREVU IMEKUWA JAMVI LA WAGENI


Na Baraka Mbolembole" Mkuu wa zamani, mkuu, mkuu! Baba! Makumazahn, mzee mwindaji, muuaji wa tembo! Mla simba, mwerevu! Akeshaye!Hodari! Mwepesi !, ambaye risasi zake hakikosi shabaha, apigaye shabaha ya kweli, rafiki mwaminifu. 

Mkuu! Baba! Ile methali ya kikwetu isemayo ' Milima haikutani, lakini wanadamu hukutana', ni ya kweli kabisa na yenye
busara.... Tazama tarishi amekuja kutoka Natal, akalia, ' Makumazahn, amefariki. 
Nchini haitamwona Makumazahn tena'. Haya yalitokea zamani
sana. Na sasa, tazama hapa katika nchi ngeni ya harufu mbaya namwona tena makumazahn, rafiki yangu. 
Ndiye bila shaka. Manyoya ya mzee mbweha yameingia mvi: lakini macho yake na meno yake ni makali kama zamani. Hahaha! Makumazahn, unakumbuka namna ulivyoipeleka risasi
katila jicho la nyati aliyekuwa akishambuli- unakumbuka' "

Ni maneno ya Umslopogaas, mtu mrefu, ambaye hadithi zake nyingi zinasimuliwa na Sir Henry Curtis. Umslopogaas alikuwa mtu mrefu mkubwa, mwenye nguvu ambaye aliitwa ' Inkubu' yaani Tembo. Mfalme wa nchi ya Wazulu alikuwa ameshangazwa na kukutana tena na rafiki yake waliyepotezana miaka mingi huku akiamini kuwa ameshapoteza maisha.


Ulimwona, Haroun Chanongo?. Anakosa bao la wazi kisha anageuka anawatazama wachezaji wenzake, Anacheka!. Inafurahisha nini? Kukosa kwake bao kunamuumiza nani? Huyu ni mmoja tu. Simba imezungukwa na 'watumishi wa watu'.
 
Simba meshikwa na makundi mawili, Hakuna umoja.
Simba inahujumiwa na wachezaji wake! Simba, imekuwa jamvi la wageni! Simba hii ' mbofu mbofu' chini ya mwenyekiti ' muongo, muongo'. Simba, iliyo taabani kutokana na tamaa za watu. Mengi yamezungumzwa kuhusu Simba.

Nini twaweza andika tena kuhusu ' mtu mwerevu' Mh. Ismail Aden Rage, kiongozi jemedari, mwenye akili nyingi, jasiri na mtu mwenye tamaa ya madaraka?. Jamani, Simba imeporomoka. Chini ya mtu huyu haina msingi, Itasongaje mbele?
 Ndani ya uwanja kuna mambo yanaumiza sana, safu ya mashambulizi haifungi mabao, uliona nafasi tano za wazi walizokosa kina Chanongo wakati walipofungwa na wale ' watoto wa Coastal Union'?.
Safu ya ulinzi inaruhusu mabao ya kipuuzi, Uliona bao walilofungwa jana ya yule kinda wa Coastal Union?

Henry Joseph ni mchezaji ambaye ananishawishi siku zote kuwa kocha, Logarusic ni kocha anayeweza kuwafunza mambo mengi Simba. Joseph kwa mara nyingine alitolewa uwanjani baada ya kucheza dakika 23 tu. 
Si mara ya kwanza Joseph kutolewa uwanjani na kocha wake, Loga. Joseph ni mchezaji anayecheza Simba kwa kufuata maelekezo kutoka upande fulani, Anaujua yeye mwenyewe. Je, Simba mpya inatakiwa kuwa na wachezaji kama Joseph?.

Wakati mwingine ndiyo, wakati mwingine hapana. Majibu haya ni kwa wale wanaotumia muda wao kuhakikisha mambo hayawi shwari. Lakini wakati, Joseph akiingia uwanjani na maelekezo fulani kutoka kwa ' mabwana zake', Loga anaweza kuisafisha Simba, Loga ni kiboko yao wachezaji kama Joseph , apewe muda zaidi awakomeshe. 
Unafikiri ni mashabiki pekee wanao umizwa na matokeo ya Simba?.

Ramadhani Singano alilia sana katika vyumba vya kubadilishia nguo. Kwa nini mchezaji huyo alikuwa akilia, je ni machozi ya furaha ambayo yamekuja baada ya kupendezwa na matokeo ya timu yake kuchapwa?.
Singano alikuwa akilia machozi ya uchungu. 'Kwani nini hivi- kwa nini anafanya vile' . Inasikitisha, hakuna anayepingana na kufungwa kwa timu ya Simba. Ila, heshima ya timu hiyo iko wapi sasa. 
Simba inafungwa na timu ambazo zimetoka kufungwa rundo la mabao.

Simba imekuwa jamvi la wageni. Ilichapwa na JKT Ruvu, na wamechapwa tena na Coastal ndani ya uwanja wa Taifa, wakati timu hizo zilitoka ' kubugizwa mabao 10-0 ' na timu za Tanzania Prisons na Azam FC, kwa nyakati tofauti. 
JKT Ruvu iliifunga Simba, baada ya kutoka kufungwa 6-0 na Prisons, na Coastal wameichapa Simba, wakitoka kufungwa 4-0 na
Azam. Timu nyingine zimeanzisha tabia ya kutua matatizo yao kwa muda kwa Simba. 
Simba ambayo hata mchezaji anashindwa kufunga goli katika
nafasi ya wazi.

Hapa, namzungumzia mchezaji kama Chanongo ambaye kupoteza kwake nafasi kunamliza, Singano. Chanongo ni mchezaji kijana, lakini ameonesha hasiyeweza kufikia malengo yake binafsi. Huyu, mchezaji anatumika na matumizi yake hayana na maslai kwake, au kwa timu yake zaidi kwa ' mabwana zake'. 
Mchezaji gani wa timu ya Taifa kama Chanongo?. Alianza vizuri kuwashika wapenzi wa timu ya Simba wakati akianza kuaminiwa na kupewa nafasi na kocha wa zamani, Mfaransa, Patric Liewig ambaye alianza mkakati wa kuwaondoa wachezaji ' watumishi wa watu' msimu uliopita. Naye mwaka mmoja sasa amekuwa zaidi
ya wale waliondoshwa.

Singano alilia kwa sababu, Chanongo aliinyima makusudi ushindi au sare timu yake. Loga, alimtoa nje Joseph sababu mchezaji huyo alikuwa anataka kufungisha timu. Naamini, kocha huyo anaumizwa sana na matokeo ya kikosi chake, ila atafanya nini, kina Joseph na Chanongo ndiyo wachezaji alionao. Yaani, hata wale watoto wa Coastal wamepumzika katika jamvi la Simba!


Kama ni mchezaji, na unahitaji heshima kutoka kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wa klabu yako, basi huna budi kuwa ' mchezaji wa klabu'.
Kutambua uwepo wako mahali husika ni kwa maslai yako na klabu pia. Wachezaji wa klabu waliheshimika na wanaendelea kuthaminiwa na klabu zao hadi sasa. 

Unamfahamu, Mzee Hamis Kilomoni?. Bahati mbaya wakati
mwingine jamii inashindwa kufahamu vizuri kuhusu wachezaji wa zamani kama, Mzee Kilomoni, ila kwa mdomo wake mwenyewe aliwahi kuniambia kuwa, pamoja na mabadiliko mengi yanayoonekana katika soka la kisasa, huku maslahi yakiwa na unafuu, bado wachezaji wa nyakati hizi ni hawajitumi ipasavyo, hawajui thamani ya Simba, hawajui Simba inabeba
uhai wa watu wangapi.
 Hawajitumi uwanjani, wanapenda starehe nje ya uwanja, na hawajui thamani ya mchezo wenyewe wa soka na ile ya klabu
yake. Kilomoni, alikuwa katibu mkuu msaidizi wa Simba akiwa na miaka 28 tu. Ndani ya uwanja alikuwa mfungaji hatari wa klabu hiyo na timu ya Taifa. Muacheni, Loga aisuke, Simba Mpya, chini ya utawala mpya


Umslopogaas, alikuwa Mfalme wa Wazulu, watu wake walikuwa wakipenda kumuita ' gogota' na ' mchinjaji', muda wote alikuwa akitembea na 'shoka lake refu la vita', ambalo kipini chake ni kipande kizuri cha pembe ya kifaru. Ila mwisho wa siku watu waligawana ng'ombe wake, wakawachuku wake zake, watoto wake hawautambui uso wake.
 Ila bado alikuwa na imani kuwa shoka lake litamsaidia kupita njia nyingine hadi kurudi katika sifa za Ufalme. Kuzmahn, alimwambia rafikiye, mfalme wa zamani, kuwa wao walikuwa safari kuelekea mlima Kenya na kuingia nchi isiyofahamika.

Hawakuwa na habari za mambo ya huko waendako zaidi ya kwenda kutafuta matendo ya ujasiri, na kutazama mahali papya kwa kuwa walikuwa wamechoka kukaa bure, na kuzungukwa na mambo yale yale ya siku zote.
Hivyo kama alihitaji kuambatana nao na kubahatisha ajali, wapo tayari kumkaribisha katika safari yao. Kuanzia, kwa Aden hadi kamati ya utendaji ni watu wachache sana wapo kwa ajili ya Simba. 
Nafikiri, Simba itasafishwa na Loga, Aachwe atumie ' shoka lake' kuwaondoa wachezaji vimeo Msimbazi. Mwenyekiti si hamtaki, kocha. Mwenyekiti si ana bifu na ninyi kamati ya utendaji, sasa naye anawakomesha kwa namna ile ile ya siku zote. 
Msingi wa matokeo mabaya ya Simba ni Aden, wachezaji pia wanahusika. Kutoka nafasi ya tatu msimu uliopita, hadi.... msimu huu. Masikini Simba, wapo chini ya utawala wa Makumazahn na Umslopogaas imekuwa jamvi la wageni.
0714 08 43 08

8 comments:

  1. Maneno yanatia uchungu hasa kwetu tunaoipenda Simba. Hakuna cha kujivunia tena. Lazima mtu mmoja au kikundi cha watu kiondoke ili timu ibaki na heshima yake.

    ReplyDelete
  2. Hivi ni siku gani na mwezi gani pamoja mwaka gani simba na yanga hazitakuwa na migogoro ili tufaidi uhondo wa mpira huu wa miguu? Tumekuwa tukiona migogoro mingi ktk club hizi km c simba kuna mgogoro basi ni yanga,migogoro imekuwa ni ya kupokezana km mwaka huu ni simba basi mwaka unaofuat ni yanga, na km mwaka huu ni yanga basi mwaka unaofuata ni simba, tumeona jinsi yanga alivyopigwa 5 -0 na Simba wakati walivyokuwa na mgogoro inngawa simba haijafungwa na yanga bao nyingi wakati wakiwa na mgogoro. Lkn nauliza ni lini Simba na Yanga hawatakuwa na migogoro tuone kambumbu zuri?

    ReplyDelete
  3. Wakiokosa mabao ni wachezaji wengi.ramadhan singano alikosa goli na muda huohuo mpiira ukaisha yeye wewe mwandishi umemuona shujaa na machoxi yake yamekufariji kwa sababu tu.unampenda na harun chanongo na henry unawachukia acha hizo issue iko wazi wanachama ni dhaifu.viongozi ni dhaifu.

    ReplyDelete
  4. Migogoro itaisha siku timu hizi zitakapoongozwa na watu wachache wenye fedha zao,kwa maana ya kwamba wenye hisa kubwa ndio wawe na sauti.Klabu hizi zikubali mabadiliko katika mifumo ya uendeshaji ili kuhamia kwenye mifumo itakayoleta tija badala ya kung'ang'ania mifumo iliyopitwa na wakati ambayo haijaleta tija zaidi ya kuviachia umaskini wa kujitakiia vilabu hivi huku ikineemesha wajanja wachache wanaotumia umbumbumbu wa wanachama wengi.Haingii akilini kwamba karne ya 21 bado katiba ya klabu inataka wachezaji wapewe asilimia 60 ya mapato timu inaposhinda mechi.Huu ulikuwa utaratibu mzuri wakati ule ambao wachezaji walikuwa hawalipwi mishahara na soka lilikuwa ridhaa.Sasa hivi maslahi ya wmchezaji yanaainishwa kwenye mkataba na sio katiba kwani kama klabu haina fedha itashindwa kutekeleza majukumu yake ya kikatiba.

    ReplyDelete
  5. Hiv hao costal, jkt ruvu sio timu?ulitaka simba ama yanga zifunge timu zote za ligi? Wacha habar za mtaan

    ReplyDelete
  6. Kwa nn baraka unapenda kuandika mambo ambayo huna ushahidi mayo??!!!..hivi kwa maneno haya unawajengea picha gani washabiki wa simba kwa wachezaji uliowasema kwenye makala haya?!!nna wsws we ndo unaetumiwa!maneno yako ni ya uchochezi dhahiri pasina Dhaka..na kwa maneno haya sitoshangaa kusikia wachezaji tajwa wakishambuliwa tena hata kuukizwa wao na familia zao kisa maneno kama haya..timu hizi 2 zinabeba hisia kubwa sn kwa mashabiki wao hapa nchini na hata nje ya nchi na ndo mana hata majuzi juzi tu hapa taifa Kuna mtu amepoteza maisha kwa hisia kali kwa timu anayoshabikia..uwe unaangalia mambo ya kuandika..we ndo unaetumiwa na kina kaburu matata wa afrika kusini!

    ReplyDelete
  7. Baraka tumekuelewa lakini kibaraka huyo uliyemtaja kafunga goli la ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, wote tumeiona me chi ya coast na nashukuru nimeirekodi hakuna kipande kinachoonyesha chanongo anacheka sawa yy hakufunga na Tuangalie nafasi ngapi alitengeneza acha unafiki jaribu kuwa Huwezi ujenge kilicho bora kwani kila anayelia Ana machungu jaribu kutafakari kwanza kabla hujaandika hotuba zako za uchochezi

    ReplyDelete
  8. comment za maana.. ila mbolembole naye ameona kitu ambacho hata KING alikiona..

    Mbolembole umekuwa ni muwazi mno.. ila unaandika vizuri sana! waandishi wengi wa siku hizi hawana fani ya uandishi kama ulivyo wewe ukiwa unatumia vizuri lugha na panctuations na uandishi unaohamasisha kuendelea kusoma habari bila kuchoka

    ReplyDelete