Na Mwandishi maalumu, Tukuyu
Wachezani 29 kati ya 34 waliochaguliwa katika programu
maalumu ya marekebisho ya timu ya Taifa inayoendeshwa na TFF wameshaanza
mazoezi makali katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya.
Wachezaji hao, ambao wametokea katika mikoa mabali mbali,
waliingia kambini siku ya Jumamosi huku wakiongozwa na Mwalimu Salum Mayanga
akisaidiwa na Patrick Mwagata, ambaye ni kocha wa makipa, Meja Joakim Mashanga
ambaye ni daktari wa team na Fred Chimela ambaye ni Meneja Vifaa.
Timu ya Taifa, Taifa stars, inayodhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, inatarajiwa kupata
mabadiliko makubwa sana ndani ya miezi miwili ijayo ili ipatikane timu bora
itakayoshiriki katika mechi za kufuzu kupata tiketi ya kucheza Kombe la Afrika.
Makocha wazoefu walikusanyika Lushoto takriban wiki mbili
zilizopita na kufanya zoezi la kuwachagua vijana 34 ambao baadaye watachujwa na
kubali 20.
Watakaochaguliwa watajiunga na Taifa Stars ya siku zote na
kutengeneza timu ya wachezaji 45 ambao watahujwa tena ili ipatikane Timu ya
Taifa yenye wchezaji 25.
Zoezi hili linatarajiwa pamoja na mambo mengine kuimarisha
uzalendo miongoni mwa wachezaji watakaochaguliwa na hili linafanyika kwa
kuhakikisha wachezaji wote wanaimba wimbo wa Taifa kila asubuhi na jioni kabla
ya kuanza mazoezi.
Kila chumba cha wachezaji pia kina bendera ya Taifa,
taratibu za kambi na wimbo wa Tanzania Tanzania ambavyo vinasaidia kuimarisha
uzalendo miongoni mwa wachezaji.
Kocha Mayanga alisema kuwa vijana wote wako salama na
wanategemea kuwapata wachezaji wazuri baada ya kambi hii.
“Tunapongeza wadhamini wetu Kilimanajro Premium Lager ambao
wamefanikisha zoezi hili kwani tuna imani tutapata vipaji vikubwa mno baada ya
zoezi hili na timu yetu ya taifa itakuwa bora zaidi,” alisema.
Wachezaji wamepiga kambi katika hoteli ya Landmark, mjini
Tukuyu na wanafanya mazoezi katika Chuo Cha Ualimu Tukuyu.
Zoezi hili limeleta msisimko mkubwa mjini Tukuyu huku
mashabiki wa mpira wakisema wana imani sasa itapatkana timu bora zaidi kwa
sababu ya utaratibu uliotumika.
Hamna kitu
ReplyDeleteMmmmh!!ni ngumu kidogo lakini,nahofu tutaishia njiani then tukaendelea na mazoea yetu
ReplyDelete