Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua kikosi cha makocha 40 kutoka sehemu
mbalimbali, Tanzania Bara na Zanzibar ili kung’amua vipaji katika mpango wa
kuboresha timu ya Taifa (Taifa Stars).
Makocha
hao ambao watafanya kazi hiyo katika michuano maalumu ya mikoa wanatakiwa kuripoti
katika ofisi za TFF siku ya Jumamosi (Februari 8 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa
ajili ya kupewa maelekezo zaidi.
Walioteuliwa
ni Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Abdul Mingange (Dar es Salaam), Ali Bushiri
(Zanzibar), Ali Mayay (Dar es Salaam), Ally Mtumwa (Arusha), Ayoub Selemani
(Zanzibar), Boniface Pawasa (Dar es Salaam), Dan Korosso (Mbeya), Dk. Mshindo
Msolla (Dar es Salaam) na Edward Hiza (Morogoro).
Elly
Mzozo (Dar es Salaam), Fred Minziro (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), Hafidh
Badru (Zanzibar), Hamimu Mawazo (Mtwara), Idd Simba (Mwanza), Jabir Seleman (Zanzibar),
John Tegete (Mwanza), Juma Mgunda (Tanga) na Kanali mstaafu Idd Kipingu (Dar es
Salaam).
Kenny
Mwaisabula (Dar es Salaam), Khalid Abeid (Dar es Salaam), Madaraka Bendera
(Arusha), Madaraka Selemani (Dar es Salaam), Mbarouk Nyenga (Pwani), Mohamed
Mwameja (Dar es Salaam), Musa Kissoki (Dar es Salaam), Nicholas Mihayo (Dar es
Salaam), Patrick Rweyemamu (Dar es Salaam) na Peter Magomba (Singida).
Peter
Mhina (Songea), Salvatory Edward (Dar es Salaam), Salum Mayanga (Morogoro), Sebastian
Nkoma (Dar es Salaam), Sekilojo Chambua (Dar es Salaam), Shaban Ramadhan
(Zanzibar), Steven Nemes (Dar es Salaam), Sunday Manara (Dar es Salaam), Tiborowa
Jonas (Dar es Salaam), Yusuf Macho (Dar es Salaam), Zamoyoni Mogela (Dar es
Salaam),
tunajaribu kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.Hakuna njia za mkato katika mafanikio ya soka bali ni programu za muda mrefu na uwekezaji katika nyanja za uongozi wa soka,programu za kuendeleza makocha na,soka la vijana,miundombinu na uwajibikaji katika kila ngazi ya FA na vilabu vya soka na kila mdau wa soka.Hapa wataalamu halisi wameachwa pembeni na wanachukuliwa watu kama kina Mogela,Sunday Manara,Mayayi,Pawasa,Mwameja na Khalid Abeid ambao sijui ni kigezo gani kimetumika na sidhani kama wanao utaalamu wa kazi waliyopewa zaidi ya kuwahi kucheza soka tu.Tunapoamua kushughulikia jambo la kitaalamu ni vema tukawa makini na kuweka pembeni urafiki na umaarufu wa dezo na kuwaachia wataalam watushauri.Mchezaji mzuri wa soka wa kuchezea Taifa Stars leo au kesho hawezi kujificha lazima ataonekana na timu za madaraja ya kwanza na ligi kuu lakini mchezaji wa miaka mitano ijayo ndiyo unaweza kumpata kwa utaratibu huu wa TFF.Mwaka 2002 FAT ilijaribu utaratibu huu kwa kuwashirikisha makocha wengi chini ya Dk Mshindo Msola na katika muda mfupi tuliishia kuchapwa 5-0 na Kenya lakini katika muda mrefu waliopatikana ndio waliokuja kutamba kama vile Mwaikimba,Nsajigwa,Sosy Manyasi,Ulimboka nk
ReplyDeleteHivi kweli ni practical kuwa na msururu wa watu kung'amua vipaji? Eti kwa sababu walicheza mpira zamani! Hivi na wenzetu waliondelea kwenye mpira wanatumia utaratibu huu? Haya!!
ReplyDeleteYes unatumika utaratibu huu! Hasa hapa uk wachezaji wa zamani ndio wanaopewa bafasi sio hyo tu hata ktk utangazaji wa michezo ya sports ya ya kila aina waloliokuwa wamepitus awali! Sasa utafute mtu ambaye hajapitia ktk mchezo wowote unadhani atafanya nini?? Wewe angalia kama kina Gary Lineker, na wengine wengi wamepewa nafasi!! Mimi kwa mtazamo wangu naona ni jambo zuri kabisa!!
ReplyDelete