Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye
viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika tathmini ya kina
kabla ya kuendelea tena.
Uamuzi
huo umefikiwa kwa kuzingatia sababu mbalimbali baada ya kikao kati ya
Sekretarieti ya TFF na maofisa wa benki ya CRDB kilichofanyika jana (Februari 3
mwaka huu) katika ofisi za Shirikisho.
Tathmini
hiyo inafanyika ili kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia ufumbuzi
kabla ya kuendelea tena na matumizi hayo, kubwa ikiwa ni hadhari iliyotolewa na
vyombo vya Usalama juu ya misongamano inayotokea uwanjani kutokana na
kutokuwepo mtiririko mzuri wa uingiaji.
Tayari
zipo changamoto za wazi ikiwemo uelewa wa washabiki wa jinsi ya kununua na
kutumia tiketi hizo, milango michache ya kuingilia uwanjani na washabiki wengi
kununua tiketi dakika za mwisho hivyo kuchangia misongamano.
VIONGOZI WA TZ KAMA KAWAIDA YETU TUNAONGOZWA KWA HISIA ZA WATU NA SIYO KANUNI NA TARATIBU...HIVI VIONGOZI WA TFF NA BODI YA LIGI NA CRDB WAMESHINDWA KUTATUA TATIZO HILI WAKATI TUNAENDELEA NA MFUMO HUU...?
ReplyDeleteAU JE HAWAKUWEKA ASSUMPTIONS AND CHALLENGES KAMA HIZI WAKATI WANAPLAN MRADI HUU...?
MALALAMIKO MENGI NI HULKA ILE ILE YA WATANZANIA TULIO WENGI KUTOKUPENDA MIFUMO RASMI.....TUNAPENDA KUISHI KIUJANJA UJANJA TU....
BINAFSI SITAKUBALIANA NA USITISHWAJI WA HUU MFUMO AMBAO UNGEKUWA NI SEHEMU YA KUIMARISHA MAPATO RASMI YA MCHEZO WA SOKA KWA VILABU NA WASIMAMIZI WA MCHEZO HUU.....
NADHARAI ZA MABADILIKO "THEORIES FOR CHANGE" ZIKO WAZI WANAJAMII WANATABIA YA KUTOKUKUBALAIANA NA MABADILIKO NA MABADILIKO YANAPOLETWA SIKU ZOTE HAYAKOSI CHANGAMOTO NA NI LAZIMA TUKUBALAIANE NA CHANGAMOTO ZA MABADILIKO WALA SIYO KUYAKIMBIA MABADILIKO HAYO AMABAYO YANAENDANA NA WAKATI HUSIKA....
NAWASILISHA....
Hii yote ni janja ya watu wachache ambao wameanza kuona wanaathirika na uwepo wa mfumo huu, kwamba unawabana katika wizi wao wa mapato ya milangoni. Changamoto ni lazima zitokee ukizingatia kuwa mfumo ni mpya Tanzania, lakini inaonekana dhahiri kuna jitihada za makusudi za kuukwamisha. TFF lazima iwe makini, isikubali wachache hawa wakafanikiwa.
ReplyDeleteViongozi wapya wa TFF wamehujumu mfumo huu ili wapate nafasi ya kuiba fedha za mapato.Ni dhahiri kwamba walipoingia madarakani walikuwa na muda wa kutosha kufanya majaribio wakati wa mapumziko ya ligi kuu lakini hawakuwa makini kwenye suala hilo na hata majaribio yenyewe wealiyafanyia chamazi ambako hakuna msongamano wa washabiki.Tabia za washabiki WA KITANZANIA kununua tiketi au kwenda uwanjani muda mfupi kabla ya mechi inajulikana na haipaswi kuchukuliwa kama dharula na hivyo hili lilipaswa kuangaliwa tangu awali wakati wa majaribio ya mfumo huu mpya.Nadhani hili ni anguko lingine la Malinzi kwa sababu anaendeshwa na mawazo ya watu wa vijiweni pale Garden Breeze Magomeni ambao hakuna wanachokihitaji kwenye soka zaidi ya kula fedha za TFF.Hujuma inayofuatia sasa hivi ni kuinyang'anya Bodi ya ligi mamlaka ya kuendesha ligi kuu na kuyarudisha TFF kwa sababu inaonekana TFF bila ligi kuu haitakuwa na sauti na pia watakosa sehemu ya kuwachomeka wapambe waliowapigia kampeni wakati wa uchaguzi mkuu wa TFF.nDIO MAANA WAMEJIFANYA KUUNDA kAMTI YA KUTATHMINI MFUMO WA LIGI KUU YA VODACOM
ReplyDelete