Zawadi za fedha taslimu kwa washindi wa
Kilimanjaro Marathon 2014 zimeongezwa hadi zaidi ya shilingi milioni 40 na
kuifanya mbio hii kuwa kati ya m io kubwa zaidi barani Afrika.
Waandaaji wa
mbio hizo wametangaza kuwa washindi wa wa Kilimanjaro Marathon 2014 watajipatia
zaidi ya shilingi milioni 40 fedha taslimu kama zawadi.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild
Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari jana kuwa mbali na washindi kujinyakulia zaidi ya shilingi milioni 40
pia watapata fursa ya kujishindia zawadi nyingine kabambe za kuvutia kutoka wadhamini
wakuu Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na wadhamini shirikishi
Alisema washindi wa mbio ndefu za marathon
ya kilomita 42 watajishindia jumla ya shilingi milioni 20, na zawadi ya fedha
taslimu shilingi milioni 10 kwa washindi wa nusu marathon huku washindi wa mbio
za walemavu maarufu kama GAPCO 10km Marathon wakijishindia kiasi cha shilingi
milioni 6. Washiriki wote watakaomaliza mbio za kujifurahisha za Vodacom 5km
Fun Run wataweza kujishindia zawadi mbalimbali.
Addison alisema kuwa mbio za mwaka huu
zimesheheeni motisha mbalimbali za kuvutia ili kuongeza idadi ya washiriki. Washindi
wa kwanza kwenye mbio ndefu za kilomita 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon)
wanawake kwa wanaume watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 4 kila mmoja,
shilingi milioni mbili kwa washindi wa pili na shilingi milioni 1 kwa washindi
wa tatu. Washindi wa kwanza kwenye mbio ndefu za nusu marathon (km 21) wanawake kwa wanaume
watajinyakulia kiasi cha shilingi milioni 2 kila mmoja, shilingi milioni 1 kwa
washindi wa pili na shilingi 500,000 kwa washindi wa tatu.
Addison aliongeza kuwa medali na t-shirt
zitatolewa kwa wanariadha 500 wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42,
wanariadha 2,200 wa kwanza kumaliza mbio za nusu marathon na wanariadha 80 wa
kwanza kumaliza mbio za walemavu. Washiriki 3,000 wa kwanza kumaliza mbio za
kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run watapewa t-shirts baada ya kumaliza mbio
na watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali za kuvutia kupitia droo.
Ili kuwapa hamasa wanariadha wa Tanzania
kufanya vizuri katika mbio hizi, Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha
shilingi milioni 2 bama bonsai kwa wanariadha Watanzania watakaovunja rekodi
katika mbio hizi.
Mbio hizi zinaratibiwa na kwa kushirikiana
na Riadha Tanzania, Chama cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro na Kilimanjaro
Marathon Club huku zikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom
Tanzania, GAPCO, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,
TanzaniteOne, CMC Automobiles Ltd, Kibo Palace Hotel, RwandAir, FNB Tanzania,
UNFPA na Kilimanjaro Water.
No comments:
Post a Comment