Search This Blog

Monday, February 10, 2014

TAKWIMU: MCHEZO DHIDI YA LIVERPOOL WAONYESHA UVIVU NA UDHAIFU WA MESUT OZIL - AFUNIKWA VIBAYA NA COUTINHO



Arsene Wenger iliisema timu yake yote kwa kiwango kibovu walichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield, lakini mtu mmoja ambaye anaweza kuwa alicheza ovyo kuliko wote kitakwimu ni Mesut Ozil.
Mchoro unaonyesha Ozil alivyokuwa akijisahau kurudi nyuma kusaidia safu ya ulinzi wakati timu yake ikishambuliwa - Mistari ya blu inamuwakilisha Ozil - alirudi mara nne 4 golini kwake
Alikuwa mvivu mno alipokuwa hana mpira na mdhaifu alipokuwa anao, mjerumani huyo alionekana ni kivuli cha mchezaji aliyekuwa akipewa sifa nyingi baada ya kuhamia England akitokea Spain.

Picha ya upande wa kushoto inayonyesha movements kuelekea mbele - kulia zinaonyesha movemnts za Countinho
Ukifananisha uchezaji wake na kiungo mwenzie mchezeshaji wa Liverpol Coutinho, takwimu zinaonyesha udhaifu mkubwa wa Ozil. Kiungo huyo wa Arsenal aligusa mpira 4 tu katika nusu ya uwanja kwenye lango lao, na hii ilikuwa ni kwa timu ambayo ilikuwa ikishambuliwa mno na matokeo yake kufungwa 5-1. 

Goli la 3 la Liverpool lilianzia kwake, alikutana na Jordan Henderson na wakashindana nguvu na akaporwa mpira kama mtoto, Henderson akakimbia kama yadi 25 na kumpa Suarez aliyepiga krosi kwa Raheem Sterling aliyefunga. 

Goli la nne, Ozil aliupeleka mwenyewe mpira kwa Coutinho, ambaye akampigia pasi Daniel Sturridge Kutoka katika nusu ya goli lao. Mshambuliaji huyo wa England akafunga bao la nne na kumuacha Ozil akiwa na sura nyekundu ya majuto. 

Hata Suarez, mchezaji ambaye anaongoza kwa mabao mengi kwa epl msimu huu, aligusa mpira mara nyingi kwenye nusu ya uwanja kwenye lango lao (Kwa maana alirudi nyuma) kuliko Ozil. Uchezaji wake wa jana unaonyesha nini kinachokosekana kwa mchezaji huyo ghali kabisa katika historia ya Arsenal. 
Suarez alikuwa anarudi na kuchukua mipira na kuwatengenezea wenzie, wakati Ozil akirudi kivivu kuja kuisadia timu yake iliyokuwa imeelemewa. Mwisho wa siku baada ya kucheza ovyo meneja Arsene Wenger alimtoa.

Mwanzoni mwa msimu alionekana kuwa bora na kutopata shida na ligi, ambapo alifanikiwa kutoa assists 8 za mabao katika ligi kuu, lakini amekuwa na kawaida ya kupotea kwenye mechi kubwa.

Huku Arsenal ikiwa inakutana na Manchester United jumatano wiki hii, Liverpool tena wikiendi ijayo, na baada ya hapo Bayern Munich, Ozil itabidi akaze na kujituma, kurudi nyuma kusaidia ulinzi na kuchukua mipira kuanzisha 'moves' katika lango la maadui.

13 comments:

  1. HUO NI UCHAMBUZI WAKO KWA MECHI MOJA TU...MBONA SIKU ZOTE ALIVYOIWEZESHA TIMU KUFANYA VIZURI HAUKUTOA MADHAIFU YAKE....?

    SIYO KILA SIKU MPIRA UNAMKUBALI MCHEZAJI HAPO SASA NDIYO UNATAKIWA UBORA WA KOCHA KUFANYA MABADILIKO YA HARAKA KWA SIKU ARSENAL WANACHEZA NA LIVERPOOL KWA UPANDE WANGU KILA MCHEZAJI ALIKOSA MOLALI YA MCHEZO PALE WALIPOPIGWA GOLI MBILI ZA HARAKA WAMEKUJA KUTUKIA WAKATI LIVER TAYARI WANAMTAJI WA GOLI 4.....KIUJUMLA KIUNGO ILIZIDIWA YOTE SIYO OZIL PEKE YAKE.....KAZOLA HAKUWA MCHEZONI PIA....IKAMLAZIMU WILSHERE ACHEZE KAMA JESHI LA MTU MMOJA NA SIYO KITIMU HAPO ALIHARIBU MFUMO MZIMA...CHEMBERLAIN PIA HAKUWA MCHEZONI....SO IN MY VIEWS IT WAS A MESSUP OF THE WHOLE TEAM WHICH WAS CAUSED BY THE TECHNICAL BENCH KWA KUPANGA TIMU ISIVYOPASWA KULINGANA NA MCHEZO...NA PIA KUSHINDWA KUUSOMA MCHEZO NDANI YA NUSU SAA YA KWANZA........

    ReplyDelete
  2. pamoja na yote mbona hutupi mapungufu ya mata na yanaonekana wazi wazi shaff acha ushabiki fanya kazi

    ReplyDelete
  3. Mi nashindwa kuwaelewa wabongo,,Shafii kazungumza alichokiona. Watu mnatumia muda wenu kuanza kumkosoa na kumuona anachozungumza si sahihi..!! Ni aje kama na nyinyi mkianzisha website zenu na kuzungumza kile mnacho kiona ni sahihi kwenu...na si kuzungumza utumbo kwenye maelezo ya wezenu,,,acheni ushamba. Lazima mkubaliane na ukweli. Msipende kuambiwa uongo ndio mmuone mtu ni mzuri.
    Big up Shaffih kazi yako inaeleweka na welevu.,Ila wasio welevu ndio hao wanaleta Upinzani ni changamoto tu.

    ReplyDelete
  4. ALLY NASSORO KUWA OBJECTIVE KWENYE KUFIKRIA...UKIFUATILIA SIKU ZA NYUMA MTANDAO HUU HUU ULIKUWA MSTARI WA MBELE KUMSIFIA OZIL....NA MTU AKITOA MAONI HAPA HAIMAANISHI KUWA YUKO SAHIHI ASILIMIA ZOTE....HUWEZI KUSEMA MCHEZAJI ANAMAPUNGUFU FULANI KWA MECHI MOJA SIKU HUWA HAZIGANDI NDUGU YANGU MBONA HAKUTUAMBIA MAPUNGUFU YA OZIL KWENYE MECHI MWANZO NA LIVERPOOL AU MECHI ZINGINE WHY ONLY IN THIS GAME....?

    MFANO LAST WIKI MAN CITY WALIPOFUNGWA NA CHELEA UTASIMAMA NA KUSEMA WACHEZJI FULANI WANA MAPUNGUFU...NI KUWA SIKU HIYO MCHEZO ULIGOMA BASI,....,..PENYE UKWELI TUWE WAKWELI KAMA OZIL ALIPUNGUA JE WENGINE WALICOVER NINI PALE UWANJANI...? NDIYO MAANA MIMI NASEMA GAME YA JUZI NI MAKOSA KUANZIA BENCHI LA UFUNDI....HADI WACHEZAJI WOTE...!!

    ReplyDelete
  5. NIMEAMIN KUMBE ATA UWEZO WA KUCHAMBUA SOKA HUA UNAPUNGUA!, BEFORE SHAFII NILIKUA NAKUKUBALI SANA KWA UCHAMBUZI WAKO WA SOKA LAKIN INAWEZEKANA NILIKUA BADO SIJAANZA KUTEMBELEA VYANZO VING VYA HABAR ZA MPIRA. SASA IVI UNACHAMBUA MPIRA SIO KAMA MCHAMBUZI BALI KAMA SHABIKI FLAN AMBAE HANA DATA ZA SOCCER AMBAE AMEANZA KUUUFAHAM MPIRA JUZJUZI TU. YAN UNASHINDWA KUJUA KAMA SOKA NI GAME AMBALO LINA CHANGE ACORDING. YAN UMEFIKIA HATUA YA KUPONDA MPAKA KIWANGO CHA OZIL KWA MATOKEA YA MECHI MOJA WE NI MCHAMBUZI GAN UNAEMDIS MTU KWA GAME MOJA!.JUZI NIMEKUSKIA UKIICHAMBUA MECHI AMBAYO MAN CITY WAMEPOTEZA MPAKA NILIZMA REDIO MAANA HUKUMBUKI AMBACHO HUA UNAONGEA PIND TIM INAPOKUA NA MATOKEO MAZUR, NILISHNGAA KUSKIA UNAIKIPONDA KIKOSI CHA MAN CITY KUA KILIKUA KIBOVU WAKATI NDO KILEKILE KIMETOA VIPIGO HUKO NYUMA.
    KAKA BADILIKA ACHA MAPENZI KWENYE UCHAMBUZI WA SOCCER UTAHARIBU KIPINDI BROO!!...BIG UP KWA JEF MAANA YULE NDO ANAJIKITA KWENYE UCHAMBUZI HALIS.#UNABOA KAKA@SHAFII

    ReplyDelete
  6. Nakuunga mkono Komba hata ukiangalia press conference ya Wenger amesema timu nzima haikucheza vizuri kuanzia mabeki mpaka washambuliaji tena kwa msisitizo kawachambua mmoja baada ya mmoja na akasema mkazo wote anauweka kwa mechi ijayo na Man U

    ReplyDelete
  7. WABONGO WAVIVU SANA KUFIKIRI NA KUELEWA.

    MTU KATOA TATHMINI YA MECHI MOJA LIVER VS ARSENAL NA KWA BAHATI KASEMA OZIL ALIKUWA SI YULE WA KILA SIKU HALAFU BADO TU MNAPINGA DAH!

    ReplyDelete
  8. Ozil hakucheza vizuri. Tuache ushabiki wa kwamba anapoongelewa vbaya mchezaj wa tm fulan hata kama ni ukweli, watu wanaponda 2. Hata washabiki wa arsenal wenye kuijua tm yao wanaelewa the fact. Yeye na Koscielny ndo wamepewa maks chache sana na mitandao ya bleacher report na goal.com kwenye hyo mech... Tunapochambua cku zote tunachambua kwa mech moja, labda inabd ndo tutachambua overall... Kama mata ataharbu tutasema pia.. Bahat nzur mata hajafanya hvo.. Katka mech ilopita ametoa assist na alitengeneza nafas nying 2. So anayesema tumuongelee mata, hayupo sahihi na hamtendei haki mata na ushabiki uliopitiliza...

    ReplyDelete
  9. MUHARAMI ANGALIA TITLE YAKE KASEMA MCHEZO UMEONYESHA UDHAIFU NA UVIVU WA OZIL NA SIYO KWA MECHI HUSIKA MBONA HATUFIKIRII BEYOND...? KATUMIA CASE YA MCHEZO MMOJA KUMJADILI MCEHZAJI AS IF NI MBAYA THROUGHOUT THE SEASON...ALIVYOANDIKA NI KAMA VILE OZIL NI MZAIFU NA MVIVU MUDA WOTE...HALAFU WEWE ANONYMOUS HAPO JUU UNAZUNGUMZIA USHABIKI HAPANA JISNI ALIVYOTOA TATHMINI YAKE UMEMUELWA AU NAWE UMEKURUPUKA TU...? SASA WALIOTOA MAX CHACHE NDIYO WAMETOA TATHMINI YA MCEZO CYO YEYE KUSME AKWAMABA MECHI IMEFICHUA UDHAIFU NA UVIVU WA MCEZAJI....HAPANA NDIYO HICHO NINA MKATALIA KUGENERALIZE TABIA AU FOMU YA MCHEZAJI KWA MECHI MOJA HILO SIYO KWELI.....SIKU HAZIGANDI....!! NA KUNA FACTORS NYINGI ZINAWEZA KUMFANYA MCHEZAJI AKAWA HIVYO ALIVYO...TUKIENDA HUKO NADHANI TUTAKUCHANGANYA ZAIDI.....!!

    ReplyDelete
  10. unajua shida n kuwa kuna watu wana mahaba ya mpira huwa hawatak kukubali ukwel

    ReplyDelete
  11. shafii unatoa analysis kwa kulinganisha mchezaji na mchezaji au mchezaji aliyecheza vibaya kwa siku husika,
    General Arsenal wote walicheza vibaya labda kipa na mashabiki tu ndio walikuwa katika form. ila wapo waliocheza vibaya zaidi ya Ozil. kiuongo yeyote wa arsenal akuna aliyecheza vizuri zaidi ya kiungo yeyote wa liverpool. (your case study iko so obvious) huitaji uchambuzi juu la hilo.
    Uchambuzi huu ni wa kiwango cha chini kwa match kama ile. sababu ilo swala liko wazi kabisa.
    Sorry i can't buy this.

    ReplyDelete
  12. Mr Komba acha Ushabiki hebu soma hicho kichwa cha habari,, na nimeamua kucopy tena hapa: TAKWIMU: MCHEZO DHIDI YA LIVERPOOL WAONYESHA UVIVU NA UDHAIFU WA MESUT OZIL - AFUNIKWA VIBAYA NA COUTINHO. Amesema mchezo dhidi ya LIVERPOOL na kamlinganisha na nani ??? na Continho. sawaaaa.

    Haya Sasa niambie ni wapi amesema takwimu hiyo ni ya ujumla kwa Ozil.!! Tuache kulalama kwa maneno tusiyokuwa na uhakika. Shaffih ameongea yake na kwa ushahidi tosha wa michoro. Unapoamua kumkosoa hebu jaribu kuonyesha Ushahidi na wewe na sio kuanza kuongea tu, bila ushahidi. itakuwa ngumu kukuelewa.

    Kama Unabisha alichoongea Shaffih toa maelezo yako yenye ushahidi watu tukuelewe na sio kusema shaffih hajui halafu umemaliza...!!, Na wewe tiririka kwa maelezo ya kumuelezea Ozil alichokifanya siku ya Liverpool,,na sio kwa Maelezo ya kumzungumzia Shaffih.

    T

    ReplyDelete