Search This Blog

Monday, February 10, 2014

TAKWIMU: MAN UNITED YAWEKA REKODI - KROSI 82 - 18 TU NDIO SAHIHI NYINGINE FYONGO...

Klabu ya Manchester United imeweka rekodi ya kuwa timu iliyopiga krosi nyingi zaidi katika mchezo mmoja wa Premier League tangu takwimu za mechi zilipoanza kukusanywa na OPTA mnamo mwaka 2006.
Picha inaonyesha namna United walivyoshambulia lango la Fulham kwa krosi tasa.
Kikosi cha Moyes kilipiga jumla ya krosi 82 ukilinganisha na 4 tu za Fulham, lakini katika krosi hizo zote za United langoni mwa Fulham, ni krosi 18 tu zilizowafikia wachezaji wao.

Pia katika mchezo wa leo United walipiga pasi nyingi zaidi kuliko mechi yoyote msimu huu - walipiga jumla ya 649 dhidi ya 216 za Fulham.
United walijaribu kufunga mara 31 dhidi ya mara 6 za Fulham - majaribio hayo 31 ni tisa tu yaliyolenga goli, huku Fulham walilenga goli mara 3, mawili yakiwa mabao waliyofunga.


Kwa matokeo ya leo, United imeendelea kubaki nafasi ya saba, wakiwa nyuma kwa pointi 9 kutoka kwa Liverpool wanaoshika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi. Everton na Spurs wapo juu yao katika nafasi ya 6 na 5. 

Jumatano wiki hii United wanaenda Emirates Stadium kucheza na Arsenal waliojeruhiwa na mikuki mitano na Liverpool jana jioni.

No comments:

Post a Comment