WATANO WALALAMIKIWA
KAMATI YA MAADILI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewalalamikia wana familia watano wa mpira
wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika mtihani wa
utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.
Riziki
Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na Samwel
Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha mtihani huo kinyume
cha taratibu.
Naye
Sabri Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na
Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya usajili wa mchezaji
Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
Kwa
mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo
itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuna kesi ndipo
walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.
TWIGA STARS,
ZAMBIA KUCHEZA MACHI 2
Mechi
ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya
Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2 mwaka huu
Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga
Stars tayari imeingia kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia
saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya
mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo
ule wa Azam Complex.
Shepolopolo
iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14
mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo
Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati
ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.
Wachezaji
wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina
Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe
Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma
Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma
Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili,
Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
STAND UNITED
YAIKATIA RUFANI KANEMBWA JKT
Stand
United ya Shinyanga imekata rufani Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
ikipinga Kanembwa JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji waliosajiliwa katika
dirisha dogo kwenye mechi ya kiporo iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi
hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari 16 mwaka
huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Kanembwa JKT
iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika
rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT ilichezesha
wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume na maelekezo
kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo
hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji
wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu Juma,
Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji Ismail,
Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David Sabugowiga.
Dirisha
dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo Stand
United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao matatu kwa
Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali
mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga,
na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT kugomea pigo la
penalti dhidi yao.
RAIS MALINZI
AENDA KUJITAMBUSHA CAF
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameondoka leo
(Februari 17 mwaka huu) kwenye Cairo, Misri kujitambulisha kwa uongozi wa juu
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Akiwa
Cairo, Rais Malinzi ambaye alichaguliwa Oktoba 28 mwaka jana atakutana na Rais
wa CAF, Issa Hayatou pamoja na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Hicham El Amrani.
WATATU WAOMBEWA UHAMISHO WA KIMATAIFA
Wachezaji watatu wanaocheza mpira wa
miguu nchini Tanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili
wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
Mchezaji Khamis Mroki Jamal aliyekuwa na
timu ya Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam ameombewa ITC na Chama cha
Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC
Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa
Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika
ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania itatoa ITC hizo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Hili sakata la Okwi mbona linafanana na lilie la Drogba aliyeamua kuikacha timu ya Shanghai Shenhua ya China na kwenda zake Galatasaray baada ya timu hiyo ya China kutomlipa mishahara yake.FIFA ilimpa Drogba provisional licence kucheza Galatasaray na hata Schalke 04 ya ujerumani ilipowakatia rufaa Galatasaray kwa kumchezesha Drogba katika mechi baina yao UEFA ilipiga chini rufaa hiyo.Ipo mifano mingi ya kutumia katika kesi hii kama vile Godfrey Walusimbi dhidi ya Don Bosco ya DRC ambye FIFA ilimpa provisional clearance kuchezaURA huku akiwa na mkataba na Don Bosco na sasa ameuzwa Gor Mahia.Mfano mwingine ni wa Olanrewaju Kayode wa Netanya ya Israel ambaye alikuwa na mkataba na Asec hadi juni 2014 lakini akenda Heartlad kwa provisional clearance na sasa amepelekwa kwa mkopo Netanya.Mbona suala hili linakuwa nongwa kwa Okwi?
ReplyDeleteUsimba na Uyanga naona utalifikisha soka letu pabayakuanzia tff mpaka kwa ninyi waandishi.hivi kama yanga walikamilisha masuala ya tms na itc kutakuwa na kitu cha kumfanya huo mjumbe aonekane kadanganya? mizengwe imeanza baada yausajili wake kuwa published.kwa uwelewa wangu pingamizi linakuja baada ya kinachopingwa kuanza.sasa huyu mjumbe anashtakiwa kwa kipi?hili suala linachujuliwa kishabiki kiasi cha kukera.Kwa okwi ana kitu gani mpaka mizengwe inazushwa kila kukicha juu yake?tuache unazi kwa maendeleo ya soka letu.
ReplyDeleteHuyo mwajiriwa wa TFF ni mwanafamilia wa soka kweli?kesi yake inastahili kushughulikiwa na mamlaka yake ya ajira/nidhamu ambayo ni Katibu Mkuu wa TFF na siyo kaMATI YA MAADILi
ReplyDeleteHao walioweka pingamizi mbona hawakuwahi kulalamika kwamba pingamizi lao halikusikilizwa?Nina wasiwasi huenda pingamizi hilo limepikwa hivi sasa baada ya kuona hata FIFA wamekubali hakuna kipingamizi cha Okwi kucheza Yanga. baadhi ya watu waliongia TFF kwenye uchaguzi wa 2013 kama Kaburu na Kidao pamoja na wale walioteuliwa na Malinzi kwenye kamati ya Sheria kama Hanspope ndio wanaoendekeza ujinga huu kwani bado ni wachanga katika uongozi wa ngazi ya kitaifa kama tff
ReplyDeleteOngeeni mambo mengine achaneni na hayo ya Okwi , mchezaji mwenyewe kwanza
ReplyDeleteumri umeenda,hebu toeni mawazo jinsi ya kujenga timu yetu ya Taifa.
Yanga hata mkimsajili Okwi zile goli tano hazitarudi OKWI wa 2012 sio wa 2014 Ameshazeeka.
ReplyDelete