Search This Blog

Tuesday, February 18, 2014

NIONAVYO MIMI:HESHIMA YA WENGER ITARUDISHWA NA MATAJI.

Na Oscar Oscar Jr
0789-784858.
Haustahili kupata heshima kwenye mchezo wa soka kama hushindi mataji.Ufalme wa Pep Gaudiola Duniani haukuletwa na staili yake tu ya "Tiki-taka" bali mataji lukuki aliyoshinda akiwa na Barcelona.Jose Mourinho pamoja na kuhama hama timu lakini anapewa heshima kokote anakokwenda kwa sababu tu ya mataji aliyoshinda akiwa na klabu ya Porto,Chelsea,Inter Millan na Real Madrid.

Sir Alex Ferguson pamoja na uzee wake aliona ni bora astaafu soka akiwa kaipatia man united ubingwa wa 20 ili kutunza heshima yake kwa wababe hao wa Old Trafford.Kama Ferguson angestaafu muda ule alipotetemeka mikono baada ya kupigwa na Barcelona kwenye fainali ya UCL pengine angekuwa amestaafu vibaya ingawa heshima yake ingebaki pale pale.

Arsene wenger ametimiza miaka 17 sasa akiiongoza klabu ya arsenal na kuvunja rekodi mbalimbali za makocha wenzie waliomtangulia kwenye timu hiyo ya London.wenger akiwa na arsenal ameshinda mataji 11 na kati ya hayo,ubingwa wa EPL ameupata mara tatu 1997/1998,2001/2002 na ubingwa wa kihistoria alioupata msimu wa 2003/2004 bila kupoteza mchezo wowote. Amewafanya Gunners wawe na uwanja ukubwa(Emirates) na mambo mengi mazuri ambayo kocha Arsene Wenger anastahili pongezi lakini hayo yote kwa sasa ni historia!

Kama arsene wenger asingefanya ile "biashara kichaa" ya kuwauza Gayel Clichy,Samir Nasri kwenda manchester city,Alex Song na Cesc Fabregas kwenda Barcelona na Roben Van Persie kwenda manchester united,msimu wa 2012/2013 ninauhakika usingepita bila Gunners kupata taji lolote.

Sera ya Wenger ya kununua vijana wadogo kwa pesa kiduchu na baadae kuwafanya wachezaji wakubwa Duniani iliyompatia umaarufu na mafanikio,kwa sasa naiona inaingia kwenye mazingira magumu kwa sababu kuu mbili.Kwanaza,vijana wengi wenye vipaji kwa sasa wanauzwa bei ghali sana ambayo wenger hawezi kuwanunua na pili,timu nyingi kwa sasa zinawahitaji vijana hao na hivyo kufanya zoezi la kuwanasa kuwa na ushindani mkubwa.

Soka la Italia na Ujerumani walikuwa wanatumia zaidi wachezaji wenye umri mkubwa lakini kwa sasa huenda ndio wanaongoza kwa kuwa na vijana wengi klabuni.Ukienda Ligi ya Italia unakutana na kina Paul Pogba,Jose Callejon,Stephen El Shaaraway na wengine kibao.Ukienda Ujerumani unawakuta kina Marco Reus,Mario Gotze,Julian Draxler.Hawa wote ni washindani wa sera ya wenger na hawaoni hasara kutoa Euro 45m kumnunua mtu kama Serge Gnabry wa Arsenal.Wenger anaweza ushindani?

Wenger aliwanunua Theo Walcott na Alex Oxlade Chamberlain kutoka timu ya vijana ya Sauthampton kwa bei poa kabisa lakini kwa sasa,hawezi kumnunua beki kinda wa Sauthampton Luke Shaw wala keptain fundi wa timu hiyo Adam Lallana unajua sababu? Wenger bado anaamini anaweza kumpata beki wa aina ya Luke shaw kwa paundi 5M bila kujua kwamba zama zimebadilika na bila kitita cha paundi 25M,kinda huyo atamsikia kwenye bomba tu.

Arsene wenger na bodi yake bado wanalipa mishahara kiduchu sana kitu ambacho ni vigumu kuwanasa wachezaji wakubwa na wenye ubora.Wyne Rooney kwa sasa yuko kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuongeza mkataba ili abakie na man united na inasemekana atakuwa akilipwa mshahara wa Paundi 300,000 kwa wiki.Pale Arsenal,Mesut Ozil ndiye anayelipwa mshahara mkubwa paund 160,00 huku Podolski akipata paund 107,Per Metersacker paundi 60,000,Laurent Conscienly paundi 50,000 huku golikipa Wojciech Szczesny akiambulia paundi 50,000 kwa juma.

Ukitazama kikosi kilichompata ubingwa wa EPL 2003/2004 kocha arsene wenger kwa kucheza mechi 49 bila kupoteza huku wakishinda michezo 36 na kutoka sare michezo 13 ukilinganisha na kikosi chake cha msimu huu,utagundua kwamba havifanani hata kidogo.Sol Campbell na Kolo Toure wakicheza beki ya kati pengine hapa kidogo wanafanana na Per Matersacker ambaye anacheza na Laurent Conscienly.

Sehemu ya kiungo ambayo ilikuwa inaendeshwa na Patrick Vieira na Roberto Pires haipo kwa sasa wala safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Thierry Henry na Dennies Bergkamp huwezi kuiona kwenye arsenal ya sasa.Namuheshimu sana Mesut Ozil lakini ukweli utabaki pale pale,hakuna mtu anayefanananae kati ya hao niliyowataja hapo juu.

Ni kweli kwamba wachezaji hao wasingeweza kucheza milele lakini kumfanya Yaya Sanogo kuwa Thierry Henry mpya wa Arsenal au Thomas Esfied kuwa kama Dennis Bergkamp,naona kabisa Arsene wenger ananidanganya.Kumfanaya Alex Song kuwa Patrick Vieira ingewezekana na kumfanya Cesc Fabregas kuwa Dennis Bergkamp pia ingewezekana lakini,kila mzee huyu anapokaribia kuijenga timu ya ushindani,anauza wachezaji wawili na kununua watoto wa chekechea!

wenger kamaliza misimu nane akiwa mikono mitupu na sasa ameanza msimu wa tisa,klabu kama Swansea na kocha wake Michael Laudrap kabla hajatimuliwa wameandika historia ya kutwaa kombe la Ligi,Kocha kama Alex Mcleish alimfunga wenger mwenyewe na kutwaa taji la ligi akiwa na Birmingham city huku,Roberto Martinez akitwaa kombe la FA akiwa na timu iliyoshuka daraja ya Wigan Athletic.Hawa wote wametwaa mataji na vikosi ambavyo pengine sio bora kama cha Arsenal,sasa wenger anasubiri nini?

Sifa anazopewa Sir Alex Ferguson sio kwa kukaa miaka 27 na man united tu,mafanikio yake ndani ya muda huo ndiyo kumbukumbu ya kudumu aliyowaachia mashabiki wa man united na dunia ya wapenda soka.Ni vigumu kumpata kocha kama arsene wenger kwa ulimwengu wa soka wa sasa lakini wapo wanaoweza kuipatia mataji arsenal na kubadili sera zake ambazo naziona kama zimeanza kushindwa kuzaa matunda.

Kama Wenger atashindwa kutwaa taji lolote msimu huu na akagoma kubadili sera zake kwenye dirisha la usajili msimu ujao,nadhani itakuwa ni muda muafaka kwa wamiliki wa timu hiyo Alisher Usmanov na Stan Kroenke kumtimua kazi.Kama wenger hatokubali kwenda na wakati,David Moyes,Brendan Rogers wataanza kushinda kombe la EPL kabla yake.

3 comments:

  1. Moyes kakaa muda gani everton. Na kashinda kombe gani? Na kwanini leo umamuona atashinda? Kama wenger aliweza kuchukua mataji 11 .imekuaje muda mrefu hajachukua? Haujui hata dimateo ndie aliechukua c.league na chalsea. Unajua timu ngapi kazifundisha na akashindwa? Kwa kifupi ndugu yao waachie soka lao. Mambo hayo yanataka wataalam

    ReplyDelete
  2. Ndugu yetu tuandikie story zetu za kina mbeyacity. Arsenal wanamuhitaji wenger kuliko yeye anaivyoihitaji arsenal. Na vilabu vya wenzetu kocha anataha majina ya wachezaji anaotaka. Mambo ya kusajili na kulipa mishara ni ya gazid na madirector wenzake. Na tunavyojua media ya uingereza ni anti arsenal. Moyes hajasahili halaumiwi analaumiwa director. Hata brendan alimvyotaka yule mchezaji toka ukrain. Tuliambuwa kaenda director kukamilisha usajili. Ikashindikana. Hata manu walivyokua kwenye matayarisho far east. Tuliambiwa director kaenda kujaribu kumsajili fabregas. Sasa imekuaje wenger ndie tajiri au kaajilwa..pia usmanov inajulikana hana maamuzi yeyote arsenal zaidi ya kroenke. Na kwasisi tunaofuatilia epl tuko enzi hizo toka kaja wenger arsenal ndio wameanza kukua.kama hauna pesa utaangukia kama leeds na portsmouth. Ozil ni mwanzo. Sasa angalia kitimtim kitachoanza arsenal. Hawana na madeni tena

    ReplyDelete
  3. We mshamba acha kutuchufua hapa. Ni sera za arsene au za arsenal chini ya kraonke. Toka lini kocha alikataa mchezaji mzuri. Yani apewe mesi amkatae. Au amlee vanpersie halafu amuuze. Kila mtu anajua wachezaji wanafuta pesa tu.. onyo .. na uwalipe ziwe pesa zako . Sio za kukopa. Utachukua kombe lakini utaishia pabaya

    ReplyDelete