Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) imeiagiza Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ifanyie marejeo (review) uamuzi wake wa kuagiza mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) irudiwe mkoani Tabora.
Maagizo hayo yametolewa na Kamati ya Utendaji iliyokutana jana (Februari 1 mwaka huu) baada ya kupokea vielelezo vipya kuhusiana na mechi hiyo iliyochezwa Novemba 22 mwaka jana mjini Shinyanga.
Mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ilivunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya kupigwa na wachezaji wa Kanembwa JKT.
Pia Kamati ya Nidhamu ya TFF inatarajiwa kukutana wiki ijayo kujadili tukio hilo la Shinyanga wakiwemo wachezaji wanane wa Kanembwa JKT waliripotiwa kumpiga mwamuzi wa mechi hiyo.
Jezi ya Rangi ya Kijani Nuksi. kwa vurugu wapo mbele.
ReplyDeletenadhan ww unamatatizo ya akili kwani wale waliong'oa viti pale taifa walikua wamevaa jez ya rangi ya kijani ??nenda milembe ukatibiwe au urud kwenu ukafundishwe jins ya kuzfahamu rangi na majna yake.
ReplyDeleteHaya maamuzi ya mezani ndiyo yanazidi kuliporomosha soka hapan Africa.Mwaka 2011 kutokana na fitina za waarabu wa Afrika Kaskazini tulishuhudi CAF ikiinyang'anya TP Mazembe ushindi dhidi ya Simba SC katika michuano ya mtoano ya klabu bingwa Afrika na kuipa Simba SC nafasi ya kuendelea na michuano hiyo na kutolewa na Raja Casablanca ya Morocco.Hoja kubwa ya CAF ilikuwa kosa la TP Mazembe kumchezesha Janvie Bokungu ambaye alikuwa bado na mkataba na Esperance ya Tunisia. TP Mazembe ilikata rufaa FIFA ilishinda rufaa hiyo baada ya kamati ya usuluhishi wa migogoro(Dispute Resolution Committee) ya FIFA kuamua kwamba Bokungu alikuwa mchezaji halali wa TP Mazembe.Hata hivyo uamuzi huo uliotolewa April 2012 haukuinufaisha TP Mazembe kwa kuwa mashindano husika yalikuwa yameshapita
ReplyDelete