Search This Blog

Sunday, February 2, 2014

JULIAN DRAXLER: SCHALKE WALIZUIA UHAMISHO WANGU KWENYE DIRISHA DOGO LA USAJILI


Julian Draxler amefunguka na kusema kwamba klabu yake ya Schalke ilizuiwa uhamisho wake wa kwenda Arsenal wakati wa dirisha dogo la usajili la January.

Maofisa wawakilishi wa wa Arsenal walisafiri mpaka Ujerumani ili kujadiliana na Schalke juu ya uhamisho wa kiungo huyo mwenye miaka 20 lakini hakuwa tayari kulipa kiasi cha £37.2 million.

"Ukweli ni kwamba mkurugenzi mkuu Horst Heldt alikuwa na ofa kadhaa za kwangu katika dirisha la usajili," Draxler aliiambia Sky Germany.

“Nina furaha kuhusu hilo. Kwa upande mwingine jambo hilo linaonyesha heshima ninayopewa kwenye klabu hii,hata kama Heldt alikataa kuniuza bila hata kuniuliza."

Alipoulizwa kama ataondoka Ujerumani dirisha kubwa litakapofunguliwa, Draxler alijibu "Sijafikiria kuhusu hilo."

“Miezi mitatu itakuwa migumu sana, nataka kucheza vizuri sana katka nusu ya msimu iliyobakia na Schalke kwa sababu nataka kupata nafasi katika kikosi cha Ujerumani World Cup. Hilo ndilo lengo kuu."

No comments:

Post a Comment