Search This Blog
Monday, February 24, 2014
MAKALA: SABABU KWA NINI MASHABIKI WA MAN UNITED WANAHITAJI KUMPA MUDA MOYES
Imeandikwa na
King Gwajeson Gwaje.
SABABU KWA NINI TUNAHITAJI KUMPA MUDA MOYES:
1. ANAJUA TATIZO LA UNITED:Kipindi ambacho anaingia alisema anahitaji wachezaji wa daraja la juu wa3 au wa5 baadhi ya mashabiki wakaponda wakisema mbona FERGIE alichukua ubingwa na kikosi alichokikuta,hapa tulisahau kuwa kila kocha ana falsafa zake,mfumo na mipango yake,lakini now raia wamekubali kweli kuna baadhi ya wachezaji UNITED sio mahala pao yaani hawana uwezo wa kuichezea UNITED.
2. UJIO WA JUAN MATA:Kufanikisha dili ya MATA,hii inaonyesha na kutupa taswira kuwa jamaa ni mwepesi kufungua pochi hasa kwa mchezaji muhimu kwa muda muafaka,hilo limejithibitisha tunaona matunda ya ujio wa MATA,japo bado tatizo halijatatuka kwa asilimia kubwa lakini angalau kidogo afadhali,kwani tatizo ni MKABAJI na sio MCHEZESHAJI.
3.KUMBAKIZA WAYNE ROONEY:Kiukweli kila shabiki wa mpira duniani aliamini huu ndo ulikua mwisho wa muheshimiwa ROONEY pale UNITED,hasa kutokana na matokeo mabaya ya timu kwa msimu huu tulioanza,lakini kitendo cha kocha kuchangia kumbakiza ROONEY hii inatupa taswira kuwa MOYES ana ushawishi mkubwa sana kwa wachezaji,tulisikia mengi yameongewa kama BIFU la ROONEY na MOYES walipokua EVERTON lakini at the end ndo amekua mtu wake wa karibu.
5.HANA MUDA NA MITANDAO:Kiukweli jamaa kama angekuwa bize na mambo ya mitandao naaamini pressure ingekuwa kubwa zaidi coz mengi yanaongelewa huko lakini sijapata kusikia amejibu vibaya au kuwa bize na mitandao hii imemsaidia pia.
6.SAPOTI YA WACHEZAJI WA SASA NA WAZAMANI:Hili pia linaonyesha kuwa ndani ya uwanja wa carrington kuna uweleano mzuri baina ya kocha na wachezaji ukiacha hizi habari za udaku udaku za nje,mfano juzi juzi tu ROBIN VAN PERSIE alitamka kuwa kocha mzuri ila tumpe muda,bado kama hii haitoshi kapteni wetu wa zamani muheshimiwa ROY KEAN nae alisapoti uwepo wake na akisisitiza kuwa UNITED ilianza kumong'onyoka tangu enzi za FERGIE mwaka 2009,kama hiyo haitoshi pia DAVID BECKHAM nae alimsapoti na bado tena PAUL SCHOLES nae juzi tu katoka kulizungumza hili kuwa anahitaji muda.
7. MANAGEMENT IMEMKUBALI:Ukiacha SIR ALEX FERGUSON aliyetuchagulia kuna mtu mnene anaitwa SIR BOBBY CHARTON a.k.a kibabu chetu huyu jamaa anaushawishi mkubwa na ndiye anayeongoza kwenda kila sehemu na UNITED japo umri umekwenda sana lakini anaheshimika kwa makubwa aliyoyafanya akiwa UNITED,huyu ameonyesha kumkubali MOYES aliposema kuwa "..ni vigumu kwa mara ya kwanza kuwa hapa lakini kadri muda unavyokwenda inakuwa rahisi na yenye manufaa zaidi.." hapo alionyesha kumsapoti moyes na kutoa rai kwa watu kuwa ni vigumu kuwa na mazuri kwa muda mfupi UNITED lakini baadae inakuwa rahisi na yenye manufaa...mfano FERGIE alipoingia UNITED ilikua vigumu mpaka raia wakaandamana atimuliwe lakini what next???mpaka sanamu kajengewa kwa aliyoyafanya.
8. JASIRI,HAKATI TAMAA,ANA MOYO WA "CHUMA":Hii imeonekana mara kwa mara pindi anapofanyiwa interview mbali mbali mfano baada ya mechi huwa anazungumza kiujasiri,hatetereki wala hafichi kitu,kama amezidiwanasema kama kuna mapungufu ya mtu anasema wazi na daima anaonyesha sio mtu wa kukata tamaa hii inasaidia kwa wachezaji pia kwani kama kiongozi akionyesha udhaifu wa kukata tamaa je walio nyuma yake itakuaje hapo???
9.ANAIJUA LIGI YA EPL:Hili halina kificho ameishi hapo miaka mingi anaijua vilivyo ligi hiyo anajua mbinu chafu na safi imemsaidia pindi alipokua na EVERTON hajawahi kushuka kwenye 10 bora.
10. MATOKEO MAZURI YA KLABU BINGWA:Hilo pia liko wazi ukitoa UNITED ni timu mbili tu ndo hajizafungwa mpaka sasa kwenye mashindano hayo makubwa barani ulaya,UNITED haijapoteza hata mchezo mmoja na ipo hatua ya 16 bora kuna haja ya kupima uwezo wa kocha hapo???
11. BARAKA ZA FERGUSON:Wahenga wnasemaga "mkubwa anaona mbali" sio kiurefu au kiupana anajua mengi kuliko wewe mdgogo ameona mengi mpaka anafikia hatua ya ukubwa hivyo kuna mambo ameyaona kwa moyes na ndo maana kamchagua na hapa ndo likapatikana jina la "The choosen One" hivyo tuheshimu mawazo ya babu yetu la sivyo yatatukuta yale ya "usiposikia la mkuu...utavunjika guu.."
12. UNITED TUNAHITAJI KOCHA WA MUDA MREFU:Hapa namaanisha hatuhitaji wale makocha wa muda mfupi kisha wanatukimbia,mfano wa akina JOSE MAURINHO,akichukua ubingwa tu anasepa..sawa atakua ametupa mafanikio lakini sio ya muda mrefu kwa sababu akishaondoka anayekuja atakuja na falsafa zake na huyo akiondoka pia atakuja mwengine na faslafa zake pia kwa hiyo means kila baada ya miaka 4 au 3 tunabadilisha falsafa ya timu,kama tungehitaji kocha wa dizaini hiyo basi hapana shaka shavu lilikua la MOURINHO,GUARDIOLA au kocha mwenye sifa hizo lakini kwa kuona mbali hilo ndo maana amechaguliwa jamaa(moyes) hapa wanasema "..mateso kwa muda mfupi...mafanikio kwa muda mrefu.."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment