Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Silas Mwakibinga
Na Moses Ng’wat,Mbeya.
Katika kile kinachoonekana uvumilivu kumshinda, Meneja wa
uwanja wa CCM Sokoine, Modestus Mwaluka, ameamua kutapika nyongo na kuituhumu
bodi ya ligi na TFF kuhusika na uvujaji wa mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwaluka amesema kwa
namna moja au nyingine kuna baadhi ya viongozi wa TFF na bodi ya ligi
walihusika na hujuma ya mapato katika mchezo wa Mbeya City na Simba.
Amesema katika mchezo huo uliochezwa Februari 15 katika
uwanja wa CCM Sokoine na timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1, licha
kuvuna kiasi cha shilingi milioni 105 na kuvunja rekodi ya mapato ndani uwanja
huo, lakini kiasi kikubwa cha fedha kiliishia mikononi mwa wachache.
Amesema akiwa kama Meneja wa uwanja alipokea taarifa ya
kuwepo kwa tiketi feki walizouziwa mashabiki, lakini alipojaribu kutoa taarifa
kwa msimamizi wa kitua aliishia
kuambulia majibu yasiyo na tija.
“Zaidi ya tiketi 30 zililetwa kwangu zikiwa hazijagongwa
muhuri na nilipolifikisha suala hilo kwa wasimamizi wa mchezo kutoka bodi ya
ligi walidai kuwa tiketi hizo hazikugongwa muhuri kwa bahati mbaya ”.
Ameongeza kuwa hata kama kweli tiketi hizo zilipita bila
kugongwa wakati wa zoezi hilo la kugonga muhuri, zisingeweza kuwa nyingi kwa
kiasi kilichoonekana mlangoni siku hiyo ya mpambano.
Amesema kutokana na hali hiyo, viongozi hao hawana sababu ya
kumshika mtu uchawi katika ufujaji wa mapato hususani katika mechi kubwa bali
waanze wao kwanza kujitazama.
Amesema ni wazi kwa tukio hilo la mpambano huo wa Mbeya City
na Simba hujuma kubwa ya mapato ilifanywa na baadhi ya viongozi wa taasisi
hiyo.
Bodi ya ligi hivi karibuni ilionekana kulalamikia ufinyu wa
mapato katika michezo mikubwa inayochezwa katika uwanja wa Sokoine, ikiwemo
pambano la Mbeya City na Yanga, pamoja na Mtibwa Sugar.
Hii ndio bongo yetu!! Tulikataa tulikataa kutumia tiketi za kielectronic eti kisa mashabiki hawauelewi mfumo!! Yaani sababu za kijinga tuu!! Kwa mechi ya MBY city na simba naamini zilipatikana zaidi ya million 200!!
ReplyDelete