Baada ya swali hilo, wanachama
waliofurika katika ukumbi huo, walisimama na kushangilia na kumfanya Makamu
Mwenyekiti Clement Sanga aliyekuwa akiongoza Mkutano huo kukabidhi rungu hilo
kwa Manji baada ya yeye kutoa ufafanuzi kuwa, Katiba ya Yanga hakuna kifungu
kinachowapa mamlaka wazee kuzungumza.
“Katiba ya Yanga haiwatambui wazee
kabisa, na mtu akinielewa vibaya sawa tu, kwani hakuna sehemu ya katiba
inazungumzia wazee, kwani Msemaji Mkuu katika klabu ya Yanga ni Mwenyekiti,
Ofisa habari na hata mimi nazungumza endapo Mwenyekiti akiwa hayupo au
ameniagiza,”alisema Sanga.
Aidha baada ya Sanga kujibu hivyo,
alimkabidhi Manji jukumu la kufafanua suala hilo na kusema kuwa, Akilimali ni
Mzee wake lakini anakuwa mvunjifu wa katiba ya Yanga kwa kusema sema katika
vyombo vya habari mambo ambayo hayastaili kuzungumzwa.
“Akilimali anaongea kupita kiasi katika
vyombo vya habari, kwani wewe sio msemaji wa klabu jamani, unavunja katiba ya
Yanga, mambo ya nyumbani unaongea tu, eti Kaseja kafanyaje, jamani acha kufanya
hivyo,”alisema Manji huku akiwaomba ridhaa wanachama waamue nini cha kumfanya
Akilimali na kuwafanya wanachama kushangilia mwanzo mwisho.
Baada ya kusema hayo, Manji alinyanyuka
katika kiti alichokuwa amekaa na kumfuata Akilimali na kuanza kuzungumza naye,
huku wanachama wakishangilia na wengine kuzomea kitendo hicho.
Akizungumzia sakata hilo, Akilimali
alikiri kukiuka katiba ya Yanga, na kusema kuwa, anahisi alipandwa na wazimu
bila kujijua na ndio sababu ya kuongea katika vyombo vya habari bila idhini ya
uongozi wake.
“Mimi kusema kweli sina kinyongo
kabisa, na uongozi wangu, wamenizuia nisiongee katika vyombo vya habari, basi
nitafanya hivyo, naisi ni wazimu tu na ushabiki ulinipanda, nawaheshimu na
kuwasikiliza viongozi wangu, kama wamenipa onyo sawa tu,”alisema.
Huyu mzee ni kilaza sana! Anashndwa kutambua kwamba UZEE NI BUSARA,MVI NI RANGI YA NYWELE TU!!
ReplyDeleteKweli mzee anachonga sana kama kasuku bwana
ReplyDeleteAma Kweli maskini akui,mzee mzima anapelekeshwa na mwenyekiti kisa uwezo wa kifedha...hili tatizo
ReplyDeleteNo sio uwezo wa kifedha ni uwezo wa Katiba ya yanga ambayo akilimali.na wanachama wote wa yanga wameapa kuilinda na kuiheshimu.Katiba ina uwezo sana ndio mana unaona hata simba pale Rage anawapelekesha kwa kutumia uwezo ilionao Katiba ambayo yeye kama mwenyekiti ndio msimamizi mkuu wa hiyo Katiba.Nilitaka kuliweka sawa hilo tu-Katiba ndio mama.
ReplyDelete