Huu utakua ni mchezo wa tatu wa Young Africans wa kujipima nguvu dhidi ya timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Albani baada ya kuwa imeshacheza michezo miwili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor na 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van Der Plyum ameendelea na mazoezi leo asubuhi na jioni ataendelea na mazoezi pia kuwaandaa vijana wake kuwa tayari kwa mchezo huo, lakini pia kuwaweka tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Baada ya mchezo dhidi ya timu KS Flamurtari Vlore kesho, Young Africans itakamilisha ziara yake ya kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kucheza na timu ya Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan katikati ya wiki ijayo kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania.
Hali ya hewa jijini Manavgat ni nzuri na sio ya baridi kali kiasi kwamba haiwalazimu wachezaji kuwaa vifaa vya michezo vya baridi kwani hali inawaruhusu kuweza kufanya mazoezi na kucheza bila kuwa na mataitzo yoyote.
Mpaka sasa hakuna katika kambi ya klabu ya Young Africans nchini Uturuki hakuna mchezaji yoyote majeruhi isipokuwa kiungo Hassan Dilunga ambaye anasumbuliwa na malaria na tayari anaendelea vizuri baada ya kupatiwa tiba na daktari wa timu Dr. Suphian Juma.
No comments:
Post a Comment