Young Africans imekamlisha ziara ya
kambi yake nchini Uturuki bila ya kupoteza mchezo hata mmoja baada ya leo
kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu
nchini Azerbajain katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jioni ya
leo katika viwanja vya Side Star Hotel Complex Manavgat jijini Antalya Uturuki.
Mchezo wa leo dhidi ya Simurq PIK
ulikuwa ni mchezo wa nne kwa Young Africans tangu kuwasili nchini Uturuki
ambapo imeweza kushinda michezo mwili dhidi ya Ankara Sekerspor 3-0, na Altay
SK 2-0 zote za Ligi Daraja la pili nchini Uturuki kabla ya kutoka sare na timu
ya KS Flamurtari ya Ligi Kuu nchini Albania.
Dakika ya 13 ya mchezo mshambuliaji
wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans
bao la kwanza kufuatia pasi nzuri ya mshambulaji Emmanuel Okwi na Didier
kuukwamisha mpira wavuni na kumuacha mlinda mlango wa Simurq PIK Pawel Kapsa
akiduwaa.
Simuriq PIK walifanya shambulizi
kupitia kwa kwa kiungo wao Stephan Polyak lakini golikipa wa Young Africans
Juma Kaseja alikoa hatari hiyo, huku Tagim Novruzov akishindwa kumalizia mpira
uliotoka sentimeta chache langoni.
Dakika ya 30 ya mchezo Young
Africans ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa kiungo Mrisho Ngasa ambaye
aliwatoka walinzi wa Simurq kufuatia migongeo mizuri katika Niyonzima, Okwi ,
Kavumbagu na kumkuta Ngasa ambaye aliukwamsiha mpira katika nyavu ndogo.
Mpira wa krosi uliopigwa na nahodha
wa Simurq Ruslan Poladov uliwapita walinzi wa Young Africans wakishindwa
kuucheza na kumkuta mlinzi wa kati Anderson Oliveira aliyepanda kusaidia
mashambulizi aliyeipatia timu yake bao la kusawazisha.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha
kwaza, Young Africans 2 - 1 Simurq PIK.
Kipindi cha pili kilianza kwa Young
Africans kufanya mabadiliko ambapo Nadir Haroub "Cannavaro" aliingia
kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani huku kiungo Hamis Thabit akichukua nafasi ya
kiungo mkabaji Frank Domayo "Chumvi".
Dakika ya 56 ya mchezo Simuriq PIK
walipata bao la pili na la kusawazisha kupitia kwa mshambulaji wao Murad
Sattarli baada ya kazi nzuri iiyofanywa na kiungo wao Stephan Polyak na mpira
huo kuwapita walinzi wa Young Africans na kumkuta mfungaji.
Mara baada ya bao hilo, timu zote
ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini mpaka dakika 90 za mchezo
zinamalizika, Young Africans 2 - 2 Simurq PIK.
Mara baada ya mchezo wa leo kocha
mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum amesema vijana wake
wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo, ana muda wa wiki moja lakini tayari
anaona mabadiliko kiuchezaji na kutegemea kufanya vizuri katika mashidano
yatakayotukabili.
"Timu imecheza vizuri
nawapongeza vijana kwa kujituma, hakuna lisilowezekana katika mpira, wachezaji
wangu sasa hivi wanajiamini na wanajua wanatakiwa wafanye nini kwa wakati
muafaka, ilikua mechi nzuri sana hata kocha wa Simurq PIK amefurahi uwezo
wetu" alisema Hans.
Mara baada ya mechi ya leo timu
itaendelea na mazoezi kesho asubuhi kuendelea kujiweka fit kabla ya kuanza
safari ya kurejea nchini katikati ya wiki hii tayari kwa ajili ya mzunguko wa
Pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa.
Young Africans: 1.Juma Kaseja, 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu
Twite, 5.Kelvin Yondani/Nadir Haroub, 6.Frank Domayo/Hamis Thabit, 7.Mrisho
Ngasa/Saimon Msuva, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier Kavumbagu, 10.Emmanuel Okwi,
11.David Luhende/Said Bahanuzi
Simurq PIK: 1.Pawel Kapasa, 2. Ruslan Poladov , 3.Dilaver Zrnanovich,
4.Tural Axundov, 5.Anderson De Oliveira, 6.Tagim Novruzov, 7.Nichat
Kurbanov/Bashir Jamilu, 8.Patrick Osiako, 9.Salif Ballo, 10.Rashad Ayyubov,
11.Stepahn Polyak
Yanga inafaa iwekwe kwenye kitabu cha Guinness Book, Imepoteza muda na pesa kwenda ulaya ya mashariki Uturuki wamefanya kila kitu hapo hapo hotelini mazoezi,mechi etc. Badala ya kuonyesha kuwa wageni wa chama cha soka cha uturuki kama taratibu zinavyotaka kazi yao ikawa kupiga picha na wageni wenzao hotelin kama Robert Carlos.
ReplyDeleteMfano picha hizi hapa juu zinaonyesha kabisa kuwa timu ni ya wazee tena wameokotana na ni mechi hewa haina hadhi ya hata ya ndondo kwani ndondo uwa na ushindani sana na mashabiki wengi.Picha hizi zinaonyesha kuwa Yanga uturuki walikuwa watalii na deal zao tu sio mpira serious kama wanavyotudanganya
Labda hujui taratibu za ulaya kaka. Ww unafikiri kines hiyo. Vitu vingine muwe mnauliza kabla hamjacomment utumbo.
ReplyDeleteUsitake kutudadanganya mtoa comment wa kwanza. Mwaka jana kila mtu aliona mafanikio ya safari ya uturuk. Yanga walibadilika sana mpaka wakawa mabingwa.
ReplyDelete