Watanzania
wanane wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya
awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC)
zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Waamuzi
hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Israel
Mujuni atakayechezesha mechi ya CL kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC
Leopards de Dolisie ya Congo itakayofanyika jijini Kigali.
Mujuni
atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.
Naye
Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya CC kati ya FC MK ya
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi
hiyo itachezwa jijini Kinshasa.
Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.
WASOMALI KUCHEZESHA YANGA, WACOMORO
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia
kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na
Komorozine Sports ya Comoro.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati
ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani
Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi
Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo
atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu
ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe
(Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif
Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo
mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na
Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya
Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi
hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed
Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi
hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano
itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu
zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni
Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri),
Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy
(Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).
No comments:
Post a Comment